Marais/Viongozi wa Tanzania watakumbukwa kwa kipi ktk Historia ya TZ?

Leornado

JF-Expert Member
Nov 12, 2010
1,529
196
Mwl J.K Nyerere, muasisi wa taifa hili na amani tuliyonayo hadi leo hii. Japo alichemka kidogo kwenye siasa ya ujamaa na kujitegenea lakini alikuwa analitakia mema taifa hili. Hakukuwa na ufisadi enzi zake.

Ali Hassan Mwinyi, mzee ruksa. Aliruhusu vitu vingi japo sina cha kukumbuka enzi zake.

B. W. Mkapa, Mzee wa utandawazi na ubinafsishaji, enzi zake alibinafsisha karibia kila kitu hadi watu tukashtuka na alikuwa mwenyekiti wa utandawazi... Pia kauchumi kalikua kwa kiasi flani...

Ndugu Mrisho Kikwete....huyu ana mengi saana yaliyotokea katika kipindi chake na bado kuna mengi yanakuja. Kikubwa nilichokiona kwa Kikwete ni shutuma za ufisadi wa kutisha ambao hatukuwahi kuushuhudia tangu tupate uhuru.....

Kuna mengi ambayo yamefanywa na mawaziri na viongozi mbali mbali wa taifa hili. Mnadhani yana faida hasi au chanya kwenye historia ya TZ na tufanye nini ili vizazi vijavyo visidumbukie kwenye jehanamu tuliofikishwa na viongozi wa awamu hii.
Historia ni muhimu kwa vizazi vijavyo.
Nyerere is and will continue to be the Hero of the Nation.
 
kIKWETE NTAMKUMBUKA KWA KUWA RAIS ALIYENITESA SANA KWENYE SUALA LA MFUMUKO WA BEI... SI MAJANI YA CHAI, MKATE, MAJI, UMEME, CHAPATI, UGALI, CHIPS, NGUO, MAFUTA, ARDHI, NYUMBA, HADI HATA KUPATA MAKABURI MAENEO KAMA KINONDONI NA SINZA

Mimi ntamkumbuka kwa kuninyanganya hata kile kidogo nilichokuwa nacho. Lakini wakati wake utapita so tuvumulie tuu hivyo hivyo hii miaka mitano ya shida na kusaga meno.
 
Mimi ntamkumbuka kwa kuninyanganya hata kile kidogo nilichokuwa nacho. Lakini wakati wake utapita so tuvumulie tuu hivyo hivyo hii miaka mitano ya shida na kusaga meno.
kuvumilia pekee haitoshi kwani ya kesho ajuaye mola;
 
Mwinyi aalilifanyia makubwa taifa hili.
Bila yeye,hakuna tv,radio stn binafsi wala magari tunayoyaona leo.
Mkapa alifanya makubwa mengi, lakini tumkumbuke kwa kuzuia mfumuko mkubwa wa bei za vitu, ni kipindi cha mkapa pamoja na kubana wafanyabiashara kwa kodi, lakini watu waliweza kujiletea maendeleo makubwa ambayo hayakuwahi kutokea tz.
Kikwete hajamaliza ngwe yake lakini atakumbukwa kwa ahadi nzuri zenye matamanio lakini zilizo shindwa kutekelezwa lakini kubwa zaidi amewafikisha watuhumiwa wa ufisadi mahakamani.
Mengi zaidi tusubiri ngwe yake ya mwisho.
 
Hivi awamu ya kwanza kuna chochote JK alichotekeleza ktk ahadi zake ???nahofia awamu ya pili manake ahadi zake nyingi hazitekelezeki. Na hao watuhumiwa mahakamani sio changa la macho kweli?? hatukawii kuambiwa ushaidi hamna na wakaachiwa huru.
 
Labda tuwakumbuke Kwa kujilimbikizia Mali za Watanzania maana waliifanya nchi ni yao ila Hayati Baba wa Taifa tunamkumbuka sana Mungu ampe pumziko LA milele
 
Mtoa hoja umechemka sehemu moja tu,Nyerere "alichemka kwa siasa ya ujamaa na kujitegemea" Unamsifia Mkapa kwa kuuza mali zilizoundwa na nani? Wapuuzi na wenye akili ndogo humshangilia kaka yao anapouza mali zilizotafutwa na marehemu baba yao ili wale pilau kwa muda mfupi,zikiisha wanaanza kulalamika. Nani katuloga?

JK mimi nitamkumbuka kwa kuhakikisha kuwa mhuni hapiti kihuni kama alivyopitishwa yeye kuikalia ikulu.Itawaudhi wengi lakini ndicho nitakachomkumbuka daima.
 
Back
Top Bottom