Marais na wageni mashuhuri waliokuwa wakifika na kulala Chato walikuwa 'Accomodated' wapi?

mngony

JF-Expert Member
Jul 27, 2012
5,193
6,381
Baada ya kuonaa Waziri Mkuu akitua katika kiwanja cha kimataifa cha Chato kufunga kongamano la vijana nimekumbuka ziara za Marais awamu aliyopita huko Chato

Bila shaka tunakumbuka kuwa awamu iliyopita Chato ilipokea marais na wageni mashuhuri kadhaa waliokuwa wakikutana ma mwenyeji wao Hayati Magufuli kijijni kwake Chato

Tunakumbuka Marais kadhaa wamewahi kufika hapo wakiwemo wa Uganda, Rwanda, Kenya, Ethiopia na kama sikosei Waziri au naibu waziri wa mambo ya nje wa Jamhuri ya watu wa China

Swali ni kwamba walikuwa wakifikia kulala na kuhudumiwa wapi? Wao pamoja na misafara yao? Hata viongozi na watumishi wa Serikali walikuwa wakilala wapi wakati Mh akihamishia shughuli za kitaifa kule?

Ni kweli kulijengwa Hotel yenye hadhi ya nyota 4/5 na Presidential Suits kuweza kuwapokea, kuwalaza na kuwahudumia Marais na viongozi mashuhuli pamoja watu waliombatana nao ? Mbona hatukuwhai kuoneshwa haya maendeleo?

Hata msiba wa kitaifa ulifanyika nyumbani kwa aliyekuwa Baba wa Hayati, lakini hatukuwahi kuoneshwa makazi yake rasmi wakati akiwa kama Rais na maendeleo yaliyopo kama hotel zenye hadhi za ku 'accomodate' marais.
 
Walilala kwenye Hekalu za Mkulu...... Mpaka anaekufa halikuonyeshwa kwa sababu ya hofu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom