Marais, Mawaziri wakuu wastaafu kutaneni kwa dharula kuna kitu hakipo sawa na mkikaa kimya ni hatari

Kuhujumiwa gani tatizo wafuasi wake anaishi nao kwa kuwatisha na kuwachimba mikwala, sometime anawatumbua live mbele ya camera.

Sasa ushirikiano gani wampe?

Hili joto linalozidi kupanda ndani ya nchi asilichekee kwa sababu likikuta ghala la mabomu hapatakalika nchini.

Ninachoona hata mawaziri wamemzilia aendeshe nchi hata PM naona kapunguza speed amebaki anamuangalia.

Inashangaza upo na viongozi wenzio wakubwa unalopoka maneno ya ajabu juu yao eti "ningepiga hadi shangazi zao"
 
Kama ukipewa nafasi ya kumsaidia au kumshauri ni nini cha kumsaidia au kumshauri kwa upande wako
1.Aache ukibuli na majigambo kuanzia kwa wazungu na watoa misaada wa nchi hii
2.Aite wataalam wa uchumi wakae chini ili kuboost exportation la sivyo hela letu litashuka
3.Apunguze kodi na makato yasiyo ya msingi kwenye biashara ili kunusulu sector ya biashara nchini.
4.Atengeneze sera nzuri za kufanya wawekezaji haswa wa kutoka nje ya nchi waone ni sehemu salama kwa wao kuwekeza mitaji yao hapa nchini sio kila muwekezaji anamtafsiri kama mwizi mpaka kupelekea kumlimbikizia makodi mpaka anafunga kiwanda.Raia wanakosa ajira baada ya kiwanda kufungwa.
5.Aache kuingilia sector,unakuta wizara ina waziri husika na naibu na viongozi wengine ila yeye anaingilia kutoa maamuzi kwa kuonesha mabavu yake kuwa yeye ndo rais
 
Nyerere alisema ukitaka kufanya jambo kubwa kwa Taifa lako usisikilize kelele kutoka nyuma yako
Utawasikia tu hao hao hao
We songa tu
Watazidi kupiga ukelele hao hao hao
We songa tu
Awataacha kupiga kelele hao hao hao
Ukigeuka nyuma utageuka jiwe na wao nia yao ni kukukwamisha na kisha kukucheka kiko wapi sasa
Dawa yao hakuna kumsikiliza mtu we piga kazi tu...
Huyo Nyerere wako yalimfika shingoni akajiuzulu. Huwezi kwenda tuuuu kama kichaa asiyepima anakoelekea. Madikteta wote duniani, hata akina Hitler walikuwa wanaambiwa na wapambe wao kuwa kila anayewapinga anatumwa au anataka kuwakwamisha.
 
Hao wastaafu ndio wale walio kopa nssf?? Walio jimilikisha mali za nchi?? Waliobariki rushwa?? , waliokuwa wanajua jinsi ya kuishi na mwenyekiti wa maisha
Ukweli ni kuwa hao hawawezi kusema chochote , wanapiga 80% ya actings. Wanaishi maisha ya peponi . Hawana shida hao
 
]Acha ahujumiwe,malipo ni hapa hapa Duniani,yeye kahujumu roho ngapi za watu?

1.Yuko wapi Mawazo?
2.Yuko wapi Azori?
3.Yuko wapi Saanane?
4.Yuko wapi Daniel?
5.Yuko wapi Eric?
6.Yuko wapi Akwilina?
7.Yuko wapi Kanguye?
8.Kosa la Tundu Lissu ni lipi?
9.Kosa la Mbowe na Esther ni lipi?

Unaleta topic ya kumsikitikia muuaji mkubwa huyo, acha nchi izame na ipotee kabisa,we have nothing to loss,tumechoka sasa.
Kwingine kote nimekuelewa ila hapo "we have got nothing to loose" Fikiria vizuri mzee baba .
 
Atoke kidogo aende nje ya nchi kama Rais..atapata exposure, atakutana na maraisi wenzake watamshauri, atajifunza mambo mengi, atapata uzoefu zaidi kwenye uongozi na namna ya kutatua changamoto mbalimbali...za kijamii na kiuchumi..

Nimegundua wakuu wa nchi zilizoendelea wanatembea sana kwa masuala ya kiuchumi, wanasign memorandum...etc...Mfano anfalua Trump na utajiri wao lkn anasafiri sana nje na kusign mikataba mbalimbali, Rais wa Ufaransa,Angela Markel ,Rais Putin,Xi wa china...wanasafiri sana hawa watu kila leo.......
Kagame nae tunamuona anavyojitahidi...kila mikutano mikubwa unashangaa kumuona....bila shaka kuna kitu anapata...
Wasaidizi wa Rais nafikiri wamshauri..na wamtengenezee na kumuandalia mambo kama hayo...sababu sisi ni maskini lazima atoke aende asisubiri watu wamfuate ikulu....na ukiona mtu ndo kaja ujue yeye ndo kaona fursa....aache utemi..ajishushe aende akatafutie taifa ugali....kuna watu wengi wakumsaidia kazi za nyumbani mfano waziri mkuu, makamu wa rais etc....
 
Back
Top Bottom