Lawkeys
JF-Expert Member
- Nov 16, 2009
- 1,118
- 287
MAPROFESA WAJA NA MAONI TOFAUTI KATIKA KESI YA MGOMBEA BINAFSI
Kesi ya mgombea binafsi imeendelea leo, marafiki wa Mahakama Prof. Palamagamba Kabudi na Prof. Juan Mwaikusa watofautiana katika maoni.
Prof. Kabudi alikuwa na hotuba ndefu iliojaa reference mpaka Chief Justice amesema Professor alikua analecture panel. Professor kabudi amesema Mahakama haina uwezo wa kutengua kifungu cha katiba ikiwa kina kinzana na ibara nyingine kwani Katiba ndio sheria mama ambayo ipo juu ya mahakama na mihimili mingine yote ya serikali. Amesema Katiba inawakilisha makubaliano ya wananchi. Amesisitiza kwamba Mahakama inauwezo tu wa kushauri bunge kufanya marekebisho ya katiba na sio vinginevyo kwani Katiba ni tofauti na sheria zingine zote.
Kwa upande mwingine Prof. Mwaikusa amesema kwamba, katiba haitoi haki za binadamu ila tu inaziguarentee, haki za binadamu ni inborn rights mtu anazaliwa nazo. Hivyo mahakama ndio chombo pekee kinachoweza kuhakisha kwamba haki hazivunjwi. Akaendelea kusema kwamba Mahakama kwahiyo inauwezo na inajukumu la kutangaza kifungu chochote cha Katiba ambacho kinaenda kinyume na haki za binadamu.
Prof. Mwaikusa ametoa angalizo kwamba kama mahakama haitakuwa na mamlaka hiyo basi haki za binadamu zitakuwa hatarini kwani sheria yoyote ambayo itatangazwa na Mahakama kwamba inakinzana na Katiba basi serikali itaiweka sheria hiyo kuwa sehemu ya Katiba mahali ambapo Mahakama haitaweza kuifikia kama ilivyo kwa habari ya mgombea binafsi na hivyo kuhatarisha haki za binadamu.
Prof. Mwaikusa kuhusiana na uamuzi uliotolewa na Mahakama kuu, amesema. Mahakama kuu haikukosea kutangaza kifungu cha katiba kinacho hitaji mgombea kuwa mwanachama wa chama fulani iliaweze kumbea kuwa ni kinyume na katiba ila amesema uamuzi huo haukuwa sahihi pale ulipo toa agizo kwa Bunge kutunga sheria itakayowezesha mgombea binafsi.
Mahakama imesema itatoa hukumu on notice yaani baada ya kuwapatia parties taarifa.
"Shoka kali isitumike kukatia mgomba"