Maradhi yote Ugua ila kuchacha usiombee!!

kaka acha jazba, ukiwa mgonjwa haliyakuwa unapesa unafarijika sana maana chochote utakacho unapata kinachobaki kupambania ni uzima wako tu, ila ukikosa pesa kila kitu kinakuwa tatizo kwako si kula si kuvaa, si tiba si faraja vyote unavikosa unaweza kujikuta unaugua magonjwa yasiyo na tiba kwasababu kila ukipimwa hautambuliki ugonjwa gani hasa unaugua, hata wale wanaoamua kujidhuru wenyewe, kujinyonga au kujiua kwa njia nyingine mbalimbali wengi wao ni wale waliokumbana na shida ya pesa.
Kabla ya kuruhusu huu mjadala kwenda mbali,hebu utuambie kwanza mpaka hapo ulipofikia, umeumwa maradhi mangapi/ ya aina gani hapo kabla?

Siku ukitembelea zile Hospitali kubwa kubwa za wagonjwa wa afya ya akili, wagonjwa kisukari, kansa, nk. Utakuja kuomba radhi. Yaani umeishiwa kidogo tu ndiyo ulinganishe hiyo hali yako na maradhi!!

Huwezi hata kupiga mizinga na kuishi kwa mission town kama wajanja wengine wa mjini!! 😇
 
Pesa zinatafutwa Bwashee! Ila kuna hayo maradhi niliyo kutajia, hata uwe na hizo pesa kiasi gani bado utaishi maisha ya mateso tu.

Hivyo nitakupinga mpaka mwisho kusema eti bora maradhi kuliko kuchacha!!!
 
Hao ndio wale wanaokufa huku wanatabasam, sasa kamchungulie mgonjwa anaetarajia kufa kwasababu ya kukosa pesa yakununulia dawa uone alivyo na sura ngumu.
Vijana wasiojua maisha bana wanaona pesa ndio kila kitu...Hujatembea mahospitalini MTU anakufa na pesa zimemzunguka zimejaaaa...yule MD wa safaricom Kenya alikuwa analipwa 100+ mill kwa mwezi lakini alijua havuki tarehe fulani atakayokufa kwa cancer....
 
Alieimba huu wimbo alifikiria sana kifalsafa. Kama sina senti mfukoni kichwa kinauma, ila nikiwa nazo hata malaria inakaa mbali na mimi. Ulimwenguni unaishi kwa raha ukiwa na pesa. Wenye dini zao mtanishambulia ila ni ukweli.
 
Back
Top Bottom