Maradhi yanayomsibu binadamu na tiba yake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maradhi yanayomsibu binadamu na tiba yake

Discussion in 'JF Doctor' started by MziziMkavu, Oct 18, 2011.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Oct 18, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  MARADHI YANAYOMSIBU BINAADAMU NA TIBA YAKE

  A. MATATIZO YA MZIO (ALLERGY). MATATIZO mengi kuhusu maradhi katika mfumo wa kupumua hutokana na hisia kali sana dhidi ya baadhi ya vitu.Vitu hivi baadae humsababishia madhara maarufu kwa jina la Allergy. Mfano wa vitu

  hivi ni: pamoja na baadhi ya vyakula; Kufisidika au kuharibika kwa maji (water pollution); Kufisidika au kuchafuka kwa hewa, kwa mfano vumbi (air

  pollution);
  Mabadiliko ya hali ya anga au hewa na mabadiliko ya hali ya misimu; Kemikali, gesi, harufu mbaya au uvundo, moshi; Dawa za kumeza. Mafuta mazuri, hata harufu ya vipodozi au manukato; Na baadhi ya vitu vingine, ambavyo mtu havipendi na pengine humdhuru. Vumbi yaweza kusababisha mtu kupiga chafya,

  baridi au moshi vinaweza kumfanya mtu kukohoa, kula baadhi ya vitu vinaweza kumfanya mtu kupata maradhi ya ngozi, kunusa au kupata harufu ya baadhi ya mafuta mazuri yanaweza kumfanya mtu aumwe na kichwa n.k. Hali zote hizi ni mifano ya mzio. Tiba kubwa ya mzio ni kuepukana na yale yote yanayosababisha mzio.

  B. PUMU (ASTHMA): Haya ni maradhi ambayo husibu mapafu na kumsababisha mgonjwa apate shida ya kupumua. SABABU: Yawezekana kusababishwa na vumbi, aina ya unga au vumbi litokanalo na maua, baadhi ya vyakula, mabadiliko ya hali ya hewa, wanyama kama paka na mbwa, aina ya bacteria, kuvuta sigara, pumu ya kurithi. n.k.

  DALILI: (3) Mgonjwa hupata shida ya kupumua ndani
  hewa safi ya oksijeni na kupumua nje hewa chafu ya kabondayoksaidi. (4) Wakati mwingine utamsikia mgonjwa akipumua anatoa sauti isiyokua ya kawaida (wheezing sound) hii ni kwa sababu ya wingi wa makohozi (mafua) yaliyosongamana ndani ya mapafu na kuzuia nafasi ya hewa. Mgonjwa hupata shida anapokua ndani ya chumba ambacho ndani yake hakuna hewa ya kutosha kwa sababu ya udogo au upungufu wa madirisha. Mgonjwa hupata nafuu baada ya kutoa na kutema makohozi na kukaa sehemu yenye hewa safi.(5) Kukohoa au kikohozi cha muda mrefu.

  TIBA: Kanuni ya kwanza: Chukua bakuli yenye maji ya moto kisha udondoshee ndani yake matone kadhaa ya mafuta ya habatsoda. Kaa juu ya kiti halafu ujifunike shuka na usogeze bakuli lenye maji ya moto nahabat soda ili upate mvuke wake.

  Tiba hii inaitwa Aromatherapy. Baada ya kufanya hivyo jipake mafuta ya habat soda mgongoni na kifuani halafu unywe mafuta ya habat soda matone matatu. Tumia kanuni hii kutwa mara mbili asubuhi na jioni kwa muda wa wiki mbili.

  Kanuni ya pili: Chukua asali nusu lita, juisi ya kitunguu saumu mili lita 200, unga wa habat soda vijiko vinne vikubwa, unga wa tangawizi vijiko viwili vikubwa, unga wa mdalasini kijiko kimoja kikubwa. Vyote changanya pamoja. Kula vijiko viwili vikubwa kutwa mara tatu.

  C. MAFUA (FLU NA COMMON COLD)
  . HAYA ni maradhi maarufu, ambayo huambukiza kwa urahisi kutoka kwa mgonjwa hadi kwa mtu mwingine.

  TIBA: Chukua asali robo lita, unga wa tangawizi vijiko viwili vikubwa, unga wa mdalasini kijiko kimoja

  kikubwa na unga wa habasoda vijiko viwili vikubwa. Changanya zote pamoja kwa kukoroga kwa kijiko. Kula vijiko viwili vikubwa kutwa mara tatu.

  D. MATATIZO YA MASIKIO:
  Bila shaka viungo au mishipa ya masikio, pua na koo yameungana na yana uhusiano wa karibu. Kwa hivyo kiungo kimoja kikiathirika yawezekana viungo vingine kuathirika, ikiwa vishambulizi vya bacteria vitasambaa hadi sehemu nyingine. Sikio ni kiungo maalum katika viungo vya hisia ambayo kazi yake ni kusikia.

  Ukiwa na Shida yoyote ile
  Unaweza kunitafuta kwa Mawasiliano Doctor.MziziMkavu Email barua ya pepe. fewgoodman@hotmail.com What's App na Viber +905344508169
   
 2. facebook

  facebook Senior Member

  #2
  Oct 18, 2011
  Joined: Jun 25, 2011
  Messages: 198
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ngoma vp? Huna tiba yake mbadala?
   
 3. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #3
  Oct 18, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  MAUMIVU YA MASIKIO NA SABABU ZAKE: Maumivu yoyote ya meno, ufizi na koo yanaweza kusababisha maumivu ya sikio kwa sababu ya mahusiano ya karibu. Pia kukohoa sana kwa muda mrefu kunaweza kusababisha maumivu ya masikio. Sikio linaweza kuuma ikiwa mara kwa mara utaweza kutia vijiti sikioni kwa ajili ya kusafisha.

  Wakati mwingine sikio linaweza kushambuliwa na bacteria na kusababisha maumivu.

  KUTOKWA NA USAHA SIKIONI:
  Ikiwa utaweka kitu kama ujiti wa kiberiti au mfano wake sikioni, unaweza kusababisha jeraha kwenye sikio na damu kuanza kutoka. Baadae usaha unaweza kutungwa sehemu ya jeraha na kutoka kidogokidogo. Lakini pia mashambulizi ya bacteria sikioni yanaweza kusababisha kutokwa na usaha.

  TIBA ZA MAUMIVU YA MASIKIO NA KUTOKWA NA USAHA: Tiba: Chukua maji masafi ujazo wa kijiko kimoja cha chai halafu uchukue chumvi kidogo kiasi cha vidole viwili uchanganye ndani ya maji hayo kisha hayo maji uchanganye na asali kijiko kimoja kidogo cha chai. Weka tone moja ya dawa hii ndani ya sikio


  MATATIZO YA MACHO: KONJACTIVA (CONJUCTIVITS): Ni maradhi ya macho sehemu ya utando au ute sehemu ya conjuctiva, ambayo inaunganisha sehemu ya ndani ya jicho na kope. SABABU:


  Yanaweza kusababishwa na vumbi, moshi, upepo ulio na ubaridi, kuweza kutumia macho kwa muda mrefu kutizama kwa mfano kusoma, kukaa katika mwanga mkali wa jua, upepo wenye ukavu na ujoto wenye hali ya umoto, mvuke, gesi, moto, kemikali, n.k.

  DALILI:
  Kujikuna, kuvimba
  macho, macho kuwa mekundu, macho kutoa maji au machozi, kuhisi kuna mchanga ndani ya macho, kuogopa mwanga mkali, n.k. TIBA: Weka macho yawe safi na uyakoshe kwa maji ya baridi. Epusha macho kutokana na joto, baridi, moshi, vumbi, macho yasitumie nguvu sana kama vile kusoma sana. Tumia dawa za kulainisha choo ikiwa hupati choo vizuri kwa sababu pia huchangia katika maumivu ya kichwa na macho.

  MARADHI YA KUTOPATA CHOO (CONSTIPATION):
  Haya ni maradhi ambayo mgonjwa huwa hapati choo kwa wepesi. Haja kubwa inaweza kutoka baada ya siku moja au mbili au zaidi na ikitoka huwa ni kigumu na hutoka kwa shida na wakati mwingine huwa kama cha mbuzi. Wagonjwa wengine hupata maumivu wakati wa kwenda haja kubwa. Mtu mwenye afya nzuri hupata haja kubwa kwa kiwango cha chini mara moja kwa siku. Na choo huwa laini na hutoka bila matatizo.

  SABABU ZA MARADHI HUSIKA
  : (1) Upungufu wa vitamini mwilini hasa vitamin B. (2) Maradhi ndani ya utumbo mpana. (3) Kula vitu vigumu na vikavu kama vile vyakula vya ngano. (4) Upungufu wa ulaji matunda na mboga. (5) Kutokunywa maji ya kutosha. (6) Upungufu wa fibre kwenye chakula zinazopatikana kwenye maganda ya mahindi. (7) Ukosefu wa kufanya mazoezi ya viungo.

  TIBA:

  Chukua glasi moja ya maziwa freshi baridi uchanganye na vijiko viwili vikubwa vya asali na kijiko kimoja kidogo cha mafuta ya habati Soda. Kunywa glasi moja kutwa mara mbili asubuhi na jioni. Dawa hii hufanya choo kuwa laini na kupata haja kubwa kwa wepesi.


  MARADHI YA KUHARISHA:
  MARADHI ya kuharisha
  ni maradhi ambayo mgonjwa hupata haja kubwa mara kwa mara na haja kubwa huwa laini na wakati mwingine huambatana na gesi au maumivu. SABABU ZAKE: (1) Kula chakula kichafu. (2) Kula chakula kilichoingia viini vya maradhi.

  TIBA: : Chukua kijiko kimoja cha Maua ya babu naji (chamomile)
  ukoroge ndani ya kikombe cha chai na maji ya moto. Yakishapoa unywe bila ya kuongeza sukari.Fanya hivyo kutwa mara tatu. Ndani ya babunaji mna virutubisho vyenye uwezo wa kusitisha kuharisha.

  Maradhi ya KICHEFUCHEFU NA KUTAPIKA: Hali ya kujisikia kuwa unataka kutapika lakini hutapiki inaitwa kichefuchefu (Nausea). Hali hii ni kawaida sana hasa wakati unaposafiri kwa chombo kama meli au ndege, hali ya ujauzito,kupata harufu mbaya, kuona au kuhisi kinyaa baada ya kuona kitu au chakula Fulani kibaya chenye ladha na harufu mbaya, wengine hupata kichefuchefu akimuona mtu mwengine akitapika. Hali ya kichefuchefu humsababishia mtu kuweza kutapika wakati mwingine.

  TIBA: Chukua kijiko kimoja kidogo cha unga wa pilipili manga ukoroge ndani ya glasi moja ya maji halafu ukamulie ndani yake ndimu nusu. Kunywa glasi moja kutwa mara tatu kwa siku.

   
 4. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #4
  Oct 18, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  GESI TUMBONI (COLIC): Ikiwa mtu atakula kwa wingi vyakula vinavyoleta gesi halafu vyakula hivyo visisagike vizuri tumboni, hukusanya gesi tumboni na kufanya mingurumo humo na kumsababishia maumivu, humkosesha mtu utulivu na kumfanya kutoka jasho na machovu bila ya kufanya kazi. Mtu hujisikia mara kwa mara aende haja kubwa na akienda hapati choo. Pia humsababishia mtu kuumwa kwa mgongo au kiuno. Ikiwa gesi hii itakosa kutoka kwa njia ya haja kubwa, basi yaweza kupanda juu na kufanya presha sehemu au karibu ya moyo na kusababisha maumivu ya moyo.

  TIBA: Chukua asali robo lita , unga wa arki susi vijiko vitatu vikubwa na unga wa habat soda vijiko viwili vikubwa. Koroga zote pamoja kwa kijiko. Chukua vijiko viwili vya mchanganyiko huu ukoroge ndani ya kikombe cha maji ya moto halafu yakishapoa unywe kikombe kimoja kutwa mara mbili asubuhi na jioni.


  Kutibu Maradhi ya BAWASIRI (MGORO):
  Haya ni maradhi ambayo humsibu mgonjwa sehemu ya haja kubwa ambayo humsababisha kupata maumivu. DALILI ZAKE: (1) Kupata choo kigumu. (2) Kutokwa damu sehemu ya haja kubwa baada ya kujisaidia. (3) Muwasho au maumivu na joto kali sehemu ya bawasiri. (4) Kupata maumivu wakati unapokaa. (5) Vidonda au kutokwa nje na kijinyama sehemu ya kutokea haja kubwa. (6) Upungufu wa nguvu za kiume.

  TIBA: Jambo la kwanza kabla ya tiba mgonjwa aweze kutibiwa maradhi ya kutopata choo vizuri ikiwa anayo kwa sababu huzidisha maradhi haya. Pia epuka kula Nyama hasa ya ngombe, Pilipili na vitu vikali. Halkadhalika usinywe maziwa kwa wingi.

  Tiba: Kunywa juisi ya tikiti maji asubuhi kabla ya chakula na usiku kabla ya kulala kwa siku 14 au siku 21 .Dawa hii hutibu na kuondoa maumivu ya bawasiri.

  TIBA 2:
  Ikiwa ni bawasiri ya kutoka nje au yenye vidonda, paka mafuta ya nyonyo aka Mafuta ya Mbarika (Castor Oil) kila siku asaubuhi na usiku unapolala kwa muda wa siku14 au siku 21.
  .

  MATATIZO YA HEDHI: Matatizo ya Hedhi
  Matatizo ya Hedhi yanawagusa moja kwa moja wanawake, tena yako katika aina na namna tofauti; hata hivyo nayo yana tiba yake inayolingana na aina ya tatizo husika.

  TIBA YA HEDHI ILIYOFUNGA (AMENERRHOEA): Kanuni ya kwanza: Tafuna ufuta kiasi cha kijiko kimoja kila siku mara tatu. Fanya hivyo hadi upate hedhi. Ni bora zaidi kula ufuta kabla ya zile siku ambazo hedhi hutoka na uendelee wakati inapotoka hedhi. Dawa hii ni hatari kwa mwanamke mja mzito, hivyo atahadhari nayo,na tangu hapoyeye haimuhusu.

  TIBA YA HEDHI ISIYOTOKA VIZURI: Chukua Jirjir (rocket) kijiko kimoja ukoroge ndani ya kikombe cha maji ya moto. Yakishapoa uchuje.Kunywa kikombe kimoja cha kahawa kutwa mara tatu.


  TIBA YA HEDHI INAYOTOKA KWA WINGI ZAIDI YA ADA: Tiba: Chukua kijiko kimoja cha maua ya Babunaji (Chamomile) ukoroge ndani ya kikombe kimoja cha maji ya moto. Yakishapoa, unywe kikombe kimoja kutwa mara tatu kabla ya kula.


  TIBA YA MAUMIVU YA HEDHI YANAYOTOKA KIDOGOKIDOGO (DYSMENORRHOEA): : Tiba:Chukua nanaa na utayarishe mfano wa chai Kunywa kikombe kimoja cha chai kutwa mara tatu

  TIBA YA HEDHI INAYOCHELEWA KUTOKA KWA SIKU ZAKE AU KUTOKA KABLA YA SIKU ZAKE KUFIKA: Hapa maana yake ni kuwa baina ya hedhi mbili huenda yakakaribiana sana au kuachana sana kinyume na ada. Yaani siku za tarehe zake haziendi sawa Chukua bakdonise (parsley) gramu 50 kisha uweke ndani ya maji lita moja, ichemshe kwa muda wa dakika tano na ikishapoa uchuje. Kunywa glasi moja kutwa mara mbili.

  MATATIZO YA MKOJO:
  UCHAFU kutoka mwilini hutolewa nje ya mwili kwa mfumo wa mkojo, kinyesi, jasho kupitia kwenye ngozi. Ikiwa kutatokea kizuizi chochote cha kuzuia uchafu kutoka mwilini sumu ya uchafu huu baadae huchanganyikana na damu na kusababisha maradhi mbalimbali.Figo ni kiungo ambacho hutoa sumu mwilini kupitia njia ya mkojo.
  VIJIWE VYA KIBOFU CHA MKOJO (DYSURIA)
  : Maradhi haya hutokea kwa kupatikana vijiwe kwenye kibofu cha mkojo. Vijiwe hivi huzuia mkojo kutoka vizuri na kufa yatoke matone matone.


  SABABU: (1) Kula nafaka mbichi kwa mfano: mchele, mahindi, njugu karanga, n.k. (2) Vyakula vilivyoisha muda wake wa matumizi au vyakula vyenye viwango vya chini ambavyo havistahiki kuliwa na binadamu. (3) Vyakula vigumu ambavyo tumbo haliwezi kusaga vizuri na hata likisaga, litasaga kwa mashaka kwa mfano chakula ambacho hakijaiva vizuri au nyama ngumu. (4) Kutotafuna chakula vizuri kwa sababu ndani ya tumbo hamna meno, kwa hivyo utalipa tumbo kazi ya ziada.

  TIBA: : Chukua mbegu za matango vijiko vitano vikubwa na mbegu za tikiti maji vijiko vitano vikubwa uchemshe kwenye maji robo lita. Kunywa glasi moja kutwa mara mbili.


  MKOJO AMBAO HAUTOKI AU HUTOKA MATONE: Kanuni ya kwanza: Chukua kikombe kimoja cha uji wa ngano uchanganye na kijiko kimoja kidogo cha unga wa uwatu na kijiko kimoja kikubwa cha samli safi ya ngombe. Koroga kwa kijiko. Kunywa kikombe kimoja kutwa mara mbili. Dawa hii hutibu mkojo ambao hautoki au hutoka matone madogo.

  MARADHI YA KUTOKWA KWA MKOJO KWA WINGI BILA YA KHIARI (POLYURIA):
  Haya ni maradhi ya kutokwa na mkojo bila ya khiari . Kabla mkojo haujakusanyika vizuri kwenye kibofu cha mkojo na mgonjwa kujiandaa kwenda

  chooni, hutokwa na mkojo hata kabla ya kufika chooni. SABABU: (1) Kulegea kwa kibofu cha mkojo. (2) Maradhi ya kisukari. (3) Kuwa na minyoo tumboni. (4 Kutumia madawa ambayo huchochea kutokwa kwa mkojo. (5) Kuwa katika mazingira au hali ya hewa ya baridi. (6) Kunywa kwa wingi vinywaji, pombe,n.k.

  TIBA: : Chukua kijiko kimoja kidogo cha chai cha unga wa harmal, vijiko viwili vikubwa vya unga wa tangawizi,kijiko kimoja cha unga wa mdalasini na vijiko viwili vikubwa vya unga wa pilipili manga. Vichanganye vyote pamoja. Changanya kijiko kimoja cha chai ndani ya kikombe cha maji ya moto ukoroge na yakishapoa unywe kikombe kimoja

   
 5. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #5
  Oct 18, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  dawa ya ngoma uache zinaa tu hutopata ngoma.
   
 6. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #6
  Oct 18, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  KUTOKWA KWA MKOJO KWA WINGI BILA YA KHIARI (POLYURIA): dawa yake hiyo kutwa mara mbili asubuhi kabla ya chakula.

  Kanuni ya Kwanza
  : Pika majani ya matango kisha unywe robo kikombe cha chai kutwa mara tatu.

  Kanuni ya pili: Chukua Bizrulqutni vijiko vitatu vikubwa uchemshe ndani ya maji lita moja na nusu. Kunywa kikombe kimoja cha kahawa kutwa mara mbili.


  MARADHI YA MTU AU MTOTO KIKOJOZI: Kikojozi ni mtu ambae hukojoa kitandani usiku au mchana wakati anapokua amelala usingizi. Anaweza kuwa mtoto au mtu mzima SABABU: Sababu kubwa za mtu kuwa kikojozi ni pamoja na Kulegea kwa kibofu cha mkojo Kuota usingizini kuwa mtu anakojoa, na kuwa na usingizi mzito kuliko kiasi.

  KULEGEA KIBOFU: Ikiwa kibofu cha mkojo kimelegea mkojo utakua hauna kizuizi cha kuzuia unapokua umeshakusanyika kwenye kibofu.

  TIBA: Chukua asali nusu lita, unga wa kamun aswad vijiko sita vikubwa na unga wa habat soda vijiko vitatu vikubwa halafu ukoroge vyote pamoja. Chota vijiko viwili vikubwa vya mchanganyiko huu wa dawa ukoroge ndani ya kikombe cha maji ya moto halafu unywe kikombe kimoja kutwa mara mbili.

  KUKOJOA KWA SABABU YA NDOTO: Sifa ya mtu anayekojoa kitandani akiwa usingizini anaweza akaota kuwa amekwenda chooni kukojoa lakini akiamka asubuhi anajikuta kuwa amekojoa kitandani, na anapokuwa anakojoa kitandani huwa anahisi raha wakati ule wa kukojoa.


  SABABU: Hii huwa ni athari za ndoto za kishetani kwa sababu shetani humuotesha ndoto za kukojoa na akamkojoza kwa kihakika.
  Hali hii pia huwatokea watu wazima bila kujali jinsia wala umri, wazima au wagonjwa

  TIBA: kAMA NI MKRISTO ASOMEWE BIBLIA KABLA YA KULALA NA KAMA NI MUISLAM FANYA HIVI Hakikisha umeshika udhu kabla ya kulala halafu usome kabla ya kulala Ayatul Qursi, Suratul-Ikhlas, Suratul Falaq na Suratul Nas mara tatu tatu kama inavyosema hadithi. Pia kabla ya kulala uombe dua ya kulala. Ukifanya hivyo shetani atakaa mbali nawe na ndoto hizi hazitatokea tena.

  ANAEKOJOA KWA SABABU YA USINGIZI MZITO: Hali kama hii huwatokea watoto ambao hucheza sana mchana kisha wakachoka. Wanapoenda kulala huwa wamechoka sana na hata usiku wakati wamelala hawawezi kupata hisia ya kutaka kwenda kukojoa chooni kwa sababu wamezidiwa na usingizi.

  TIBA: Tiba yake ni mtoto aweze kupunguza mchezo na aweze kulala kidogo mchana kama ilivyo katika mafundisho ya sunnah. Tiba ya pekee ni mtoto adhibitiwe na kupangiwa ratiba za kucheza, na kupangiwa muda wa kutosha kuweza kupumzika, ikiwezekana alale mchana kidogo.

  Anayeweza kufuata haya Maagizo yangu ayafuate yatamsaidia asiweze asiyafuate mimi sijamlazisha Mtu nimefundishwa bure na mimi nimetoa hapa bure.

  MAKE IT OR BREAK IT source.MziziMkavu.
   
 7. GAZETI

  GAZETI JF-Expert Member

  #7
  Oct 18, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 3,532
  Likes Received: 1,020
  Trophy Points: 280
  Mkuu sijamaliza kusoma zote lakini nashukuru kwa jitihada kubwa na
  aina ya changamoto unazoleta hapa jukwaani!
   
 8. TUNTEMEKE

  TUNTEMEKE JF-Expert Member

  #8
  Oct 18, 2011
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 4,582
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  asante sana mkuu ubarikiwe na Allah!
   
 9. Mgariga

  Mgariga Senior Member

  #9
  Oct 18, 2011
  Joined: Apr 1, 2011
  Messages: 176
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  ubarikiwe mku ila ntarudi kukuuliza baadhi ya material uliyotaja, mengine cjawahi kuyasikia...unga/mafuta ya 'habat soda' let me go through b4 i come back......
   
 10. J

  Joyceline JF-Expert Member

  #10
  Oct 18, 2011
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 1,010
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Asante sana nimepata tiba ya tatizo langu mojawapo lilikuwa linanisumbua sana.
   
 11. Kijuche

  Kijuche JF-Expert Member

  #11
  Oct 18, 2011
  Joined: Aug 26, 2010
  Messages: 419
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kazi njema mkuu.
   
 12. bhageshi

  bhageshi JF-Expert Member

  #12
  Oct 18, 2011
  Joined: Jul 24, 2010
  Messages: 264
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Nilikuwa napita tu hapa kushuhudia, Pole na hongera kwa kupata tiba japo sifahamu maradhi yanayokusibu ambayo mzizimkavu amekuonesha tiba...
   
 13. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #13
  Oct 18, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,689
  Likes Received: 410
  Trophy Points: 180
  Ahsante sana kwa darsa hili murua la kutufungua macho sie wagema ulimbo.
   
 14. Kivumah

  Kivumah JF-Expert Member

  #14
  Oct 18, 2011
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 2,413
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Thank U for this useful post Mzizi
   
 15. terabojo

  terabojo JF-Expert Member

  #15
  Oct 19, 2011
  Joined: Aug 3, 2010
  Messages: 215
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Je, tiba ya moyo(low au high)?
   
 16. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #16
  Oct 20, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  Dawa ya Kutibu Maradhi ya blood pressure, kusafisha damu au mishipa ya damu kujaa mafuta kutoa gasi tumboni unachemsha maji na kutia katika glassunatia kijiko kimoja kikubwa cha asali kijiko kikubwa cha cha siki ya apple
  na kumeza haba moja au mbili ya kitunguu swaumu kama utatia habba soda pia unakuwa umekamilisha tiba

  Kila maradhi yana pozo.. na dawa ziko za aina tofauti tu kuna dawa za miti shamba kuna dawa za chemical yaani tunazopatiwa hospitali na kuna dawa zinatokana na matunda alitojaaliwa Allah S.W. Mimi binafsi napenda kujitibu kwa dawa za matunda kwani hamna atrificial ndani yake. Inshallah nitaandika juu ya matunda mawili matatu ambayo husaidia kuondoa maradhi ya moyo.


  Apples: Matunda haya yana wingi wa potassium na phosphurus na kiwango kidogo cha sodium, miaka ya nyuma walikuwa wakitumia tunda hili pamoja na asali kwa ajili ya matatizo ya moyo, kuwa na wingi wa potassium katika mwili husaidia kuepukana na maradhi ya moyo kwahivo mtu mwenye maradhi ya moyo ni vizuri kula matunda haya asubuhi na jioni na uzuri zaidi akila pamoja na asali.


  Grapes(zabibu): Zabibu au juice ya zabibu husaidia sana katika maumivu ya moyo yaani cardiac pain. Maradhi ya moyo yanaweza kuondoka kwa mgonjwa akitumia zabibu kwa muda.


  Orange(machungwa): Juice ya machungwa ukichanganya na asali husaidia kuondoa maumivu ya moyo kama coronary ischaemia.


  Garlic(kitunguu saum):Kitunguu saum kinalinda upatikanaji wa heart attack, husaidia kuondoa mafuta katika mishipa ya moyo pia husaidia artiries kupeleka damu upesi (artiries huwa nzito na hii hupelekea kupatikana kwa high blood perssure na heart attack) Mgonjwa wa moyo akitumia garlic kwa muda maradhi hayo humuondokea atumie kila siku asubuhi chembe 2 na usiku chembe 2.


  Onion(kitunguu maji): Onion kazi yake ni kama ya kitunguu saum .


  Wheat(ngano): Majani ya ngano husaidia moyo kufanya kazi yake pia husaidia na mapafu, pia capillary hufanya kazi uzuri zaidi na kuongeza damu.


  Honey (Asali):Asali ni dawa bora kulikoni zote nilizozitaja hapo juu. Mwenye maradhi ya moyo anywe kila siku glasi ya maji achanganye na asali pamoja na maji ya ndimu na pia anywe kama ataamka usiku na aendelee kufanya hivi kadri awezavyo na Inshallah maradhi hayo yatamuondoka.
   
 17. terabojo

  terabojo JF-Expert Member

  #17
  Oct 20, 2011
  Joined: Aug 3, 2010
  Messages: 215
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Shukurani Sana
   
 18. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #18
  Oct 20, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  Migraine Au kwa Kiswahili huu ugonjwa unaitwa kipanda uso au kichwa kuuma upande Mmoja Dawa yake ni hii, Grapes (zabibu): Juice ya zabibu zilizoiva ndio dawa ya migrane, utumie kiwango kidogo cha juice hiyo utumia hadi utakapoona kuwa umepata nafuu! Inshallah itakusaidia.

  Dawa Ya Fungus Za Miguu
  Fungus katika ya vidole ni fungus ya kawaida inawezekana wewe mtumiaji sana wa maji, kwani maji huchimbua mwili!! kwahivo vijidudu kama hivo huingia na kupambana na white blood cells lakini kwa kuzidiwa nguvu ndio fungus hujitokeza, kama fungus uliyoisema wewe ni ya kawaida ila ina kero

  kwakweli. Kwanza kabisa kama mtumiaji wa maji sana upunguze yaani sio kutumia maji kwa kunywa laa! kutumia maji yaani kuchezea maji inawezekana ukikoga unatumia maji zaidi au kila wakati unakosha miguu yako na mambo kama hayo. Hata hivo ipo dawa moja na nafikiri inajulikana sana nayo ni ndimu na jivu. Unachukua jivu unaweka katika sehemu hiyo katikati ya kidole na halafu unanyunyizia ndimu! Dawa nzuri lakini inachota sana.! Inshallah nafikiri umenifahamu.

  Au hii DawaKuna powder inaitwa 'DEODORANT POWDER' "FAA" inapatikana masupermarket, huenda ikawa iko kabila jengine kwani FAA ni sabuni, na hiyo ni powder ambayo pia ni nzuri na inawafaa kwa wale wanaotoka majasho kisha wakatokwa na harufu. Hii powder ukisha kukoga unakuchunja kidole kimoja kimoja na unatia ni uzuri wakati unapokwenda kulala inakausha na pia hutoki harufu ya miguu.

  Sababu yake ni kuvaa soksi na boot kwenye nchi za joto ndio hufanya jasho kwenye vidole na kusababisha fungus. kwa hivyo jaribu usikae muda mrefu na soksi na boot au badilisha viatu na usivae soksi.

  Dawa nyengine ya Fungus ni 'DAKESEN' Prickly Heat Powder - Cooling and Refreshing, inauzwa kwenye masupermarket madogo madogo tena ni rahisi bei yake baiza 250. unatia wakati unapokwenda kulala kwa kufungua kidole kimoja kimoja na kutia hiyo powder. InshaAllah kwa uwezo wake Subhana itaondoka.

  HII POWDER NI NZURI SANA PIA KWA WATOTO AU WATU WAZIMA WENYE KUPATA TETE KUANGA UNAKUWA UNAMTUMILIYA MTU KWA KUMPAKA MWILI MZIMA KWA KILA UNAPOKUMBUKA. INAVUNJA NGUVU YA TETE KUANGA NA HAZIENEI NA KUKAUKA KWA HARAKA.


  Dawa ya kusafisha uso Asali

  Sandal
  Rob
  Hilba (tia kidogo sana kwa ajili ya harufu)
  maji ya mawardi na maji


  changanya vyote pamoja na utie kwenye uso na huku unafanya massage kisha wacha kwa dakika kumi na kosha kwa maji ulochanganyisha na maji ya mawardi.

  Dawa Ya Mapele Kwenye Uso Chukua Siki Ya Apple Kidogo Changanya Na Maji Kidogo Pamoja Na Mafuta Ya Nazi Kidogo Sana, Paka Kwenye Mapele. Subiri Dakika Tano Au Kumi, Kosha Uso Kwa Maji Yalokuwa Si Baridi Sana. Paka Kwa Siku Mara Moja.

  Dawa Ya Kuzuia Kutapika Na Kuharisha Wakati Mmoja Wetu Anapotapika Na Kuharisha Ikiwa Ni Mtu Mzima Au Mtoto Dawa Kubwa Inayozuia Ni Kukamua Ndimu Na Kutia Maji Kisha Utie Chumvi (juice Ya Ndimu Yenye Chumvi). Na Usinywe Yote Kwa Pamoja Uwe Unakunywa Kidogo Kidogo Na Uwe Unasita Kama Dakika Tena Unakunywa Tena Na Hivyo Hivyo. Huenda Mtu Atatapika Mara 3 Au 4 Na Kuharisha Lakini Kwa Kuendelea Kunywa Hiyo Juice Kila Baada Ya Dakika Atazuia Ishaallah Kwa Idhni Yake Allah.


   
 19. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #19
  Oct 20, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  HEDHI KWA MWANAMKE

  Matabibu wanasema mwanzo na wakati wa mwanammke kuingia katika hedhi ni afikiapo umri wa miaka 10, mpaka kufikia umri wa miaka 14 na mwanzo wa kumaliza kipindi au wakati wa kuingia katika hedhi nimiaka 30 na tano na mwisho kufunga hedhi ni miaka 60.

  Ama wanazuoni wa fiqhi wanasema mwanammke kuingia katika hedhi kabla ya miaka tisa basi si hedhi. Na umri wa mwisho kufunga hedhi ni 60.

  Mwanachoni mwengine wa madhhebu ya Shafii anasema hedhi haina mwisho maalum wakumaliza. Kuna kauli mbali mbali zinatafautiana, kwasababu kila mmoja alietoa fatwa yake ametegemea utafiiti wake.

  DAWA ZA KUTEREMSHA HEDHI.

  Ikiwa hedhi imezuilika kwa kufikia umri wa kumaliza au ni kwasababu ya mimba, inafahamika lakini ikiwa si kwasababu mbili hizo basi hufanyiwa dawa na kuirudisha hedhi.

  1. Kunywa chai ya mdalasini.

  2. Mvuje ukinywewa pamoja na pilipilimanga huteremsha hedhi iliyo fungwa katika uzai au mapito yake.  DAWA YA WENYE KUUMWA NA MGONGO ?

  Gundi ( hili gundi limekaa kama ubani wa kufukiziya ) ukiwaambia wenye kuuza madawa wanafahamu. Unasaga unakuwa unga.
  Lozi ( unaroweka kwa maji ya mfukuto kisha unatoa maganda na unazikausha kidogo kwenye oven kisha unazisaga.)
  Sukari ya Mawe au sukari guru (sukari nyekundu)
  Hiliki
  Za'fani
  siagi kidogo
  Maziwa

  ** Unayayusha siagi yako kisha unatia sukari (mawe au guru) kisha unatia lozi unachanganya kisha unatia gundi, hiliki na za'faran. unaiyepua unaitia kwenye sinia.

  *** Ikisha kupoa unatia kwenye chupa au pahala kuihifadhi.

  NAMNA YA KUTUMIA:- Kijiko cha supu kimoja asubuhi utakula na usiku kimoja.
  MAZIWA UTAKUNYWA GILASI MOJA ASUBUHI BAADA YA KWISHA KULA HIYO DAWA NA USIKU GILASI MOJA BAADA YA KWISHA KULA DAWA.

  INSHAALLAH KWA UWEZO WAKE ALLAH, ATAPONA KWA KILA MWENYE MARADHI ALLAH ATAMUONDOSHEA. AMIN
   
 20. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #20
  Oct 20, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  Dawa ya Maradhi ya Hepatitis

  Juu ya kuwa kwamba bado hazijapatikana dawa za uhakika juu ya maradhi haya, lakini wachunguzi wamegundua kuwa vipo vitu viwili ambavyo vinaweza kusaidia kwa wale waliopata maradhi haya katika early stage na pia unaweza kujikinga na maradhi hayo.

  Zabibu (Grapes): Huifanyia kazi Ini pamoja na kuinua glycogenic,kwahio inaaminika ulaji wa zabibu huweza kuwa ni kinga dhidi ya maradhi hayo ( na ni vizuri zaidi kula fruits kabla ya kula chakula cha mchana isiwe kama wenzetu nchi za arabuni wao kwanza huanza chakula baadae ndipo hula matunda, kwa utaratibu wa lishe bora kwanza inatakiwa kula matunda ndipo ule chakula kizito)

  Mtindi (Curd,yogurt): Kutokana na upungufu wa damu, ambayo ni moja katika sababu kubwa zinayosababisha maradhi ya hepatitis, Lectic Acid inayopatikana katika mtindi husaidia mfumo mzima wa damu ndani ya mwili. Kula mtindi uchanganye na asali iwe unakula mara kwa mara.


  Dawa ya Maradhi ya homa

  Dawa za homa ziko nyingi tu lakini nitazitaja kwa uchache ambazo ni common.

  Kuoga maji ya baridi pale unapojisikia homa, huondosha machovu ya mwili.

  Chai kavu ukaipika pamoja na ndimu kisha uinywe moto moto hutoa joto la mwili na huondoa homa moja kwa moja.

  Maji ya balungi uchanganye na maji ya kawaida huondoa homa.

  Juice ya apricots uchanganye na glucose au asali uwe unakunywa asubuhi na usiku.

  Inshallah zitasaidia.

  Hepatitis B nini dawa yake?
  Maradhi mabaya mno na Inshallah Mola atatuepusha nayo na alowajaalia kuwapa mtihani huu atawashushia Afya.

  Hata hivo nimepata makala moja (kwa english) inayozungumzia juu ya utibabu wa maradhi haya nikaona bora niiweke tupate faida kwa sote ijapokuwa sijaweza kuitranslate kwa kiswahili pia nipo katika kuitafuta dawa za mitishamba ambayo zinatibu maradhi haya lakini hadi sasa sijaipata lakini Inshallah nikiipata nitaeweka ili iwe faida kwa sote sote.

  Alpha-interferons were the first drugs approved in the United States for the treatment of chronic hepatitis B. Interferon treatment is recommended for individuals who have "replicative disease" (HBeAg positive). About 40% of such individuals will lose serum HBeAg after 16 weeks of treatment with interferon-alpha. Loss of HBeAg is correlated with an improved prognosis. A few treated patients (less than 10%) may even be cured as assessed by the loss of HBsAg.
  Patients treated with interferon-alpha should have evidence of infection with hepatitis B virus, documented by the presence of hepatitis B surface antigen in the blood, for six months. The patients should also have evidence of virus replication, documented by the presence of hepatitis B e antigen in the blood. Ongoing inflammation of the liver should also be present as documented by an elevation in serum aminotransferase activities. A liver biopsy should also be performed prior to treatment. Patients with severe, decompensated liver disease (eg. encephalopathy, ascites, very high serum bilirubin, prolonged prothrombin time, etc.) should not generally be treated with interferon alfa except in the setting of an approved clinical study.

  The recommended dose of interferon alfa-2b for the treatment of chronic hepatitis B is 5,000,000 units daily, administered by subcutaneous or intramuscular injection, for a total of 16 weeks. The patient must be monitored carefully during the treatment period for side effects including flu-like symptoms, depression, rashes, other reactions and abnormal blood counts.

  A meta-analysis of several randomized trials of interferon alfa-2b in the treatment of patients with chronic hepatitis B showed such treatment to be cost-effective (Wong et al. Annals Intern. Med. 1995;122:664-675). This analysis showed that treatment with interferon alfa-2b decreased viral replication, documented by loss of serum hepatitis B e antigen, in about 45% of patients compared to less than 10 % of untreated patients. About 8% of patients also lost hepatitis B virus surface antigen (cured) within one year of treatment compared to a rate of about 1% a year for untreated patients.

  Other treatment options for chronic hepatitis B include nucleoside analogues. In December, 1998, the United States Food and Drug Administration approved lamivudine , also known as 3TC and is also effective against HIV, for the treatment of chronic hepatitis B (patients who are HBeAg positive). Lamivudine is taken orally at 100 mg/day for chronic hepatitis B. In studies where they were compared, lamivudine was equally effective to interferon-alpha in inducing a loss of serum HBeAg. It also has been shown to improve liver biopsy results in patients treated for one year. In September 2002, the United States Food and Drug Administration approved adevofir dipivoxil, another nucleoside analogue also effective against HIV, for the treatment of hepatitis B. The dose is 10 mg/day for chronic hepatitis B. At the present time, other nucleoside analogues are being studied in clinical trials. The combination of interferon-alpha and a nucleodide analogue, two nucleoside analogues together (such as lamivudine and adefovir) are also under investigation.  Hepatitis B nini dawa yake? maji ya miwa kuywa kwa wingi ni mazuri sana kwani yanamsaidia mwenye hayo maradhi Hepatitis B.Na Dawa ya kutibu Maradhi ya Hepatitis B Virus,ninayo nitafute kwa wakati wako nitaweza kukutibia na ukapona kabisa. Unaweza kunitafuta kwa Mawasiliano Herbalist Dr. MziziMkavu Email barua ya pepe.fewgoodman@hotmail.com What's App na Viber +905344508169 Au Ni add Kwa Facebook tumia jina hili mzizimkavu.
   
Loading...