Yo Yo
JF-Expert Member
- May 31, 2008
- 11,210
- 1,710
Ughaibuni bana,nakumbuka siku yangu ya kwanza kuruka majuu the dramer started pale airport....huku akili yangu ikiwa inajenga hisia mapicha picha niliokuwa nayaona kwenye video eti sasa naenda kukaa kwenye magorofa yale nikiwa na usongo mkubwa wa kuwarukia totozi za kitasha.
Kwenye pipa nilikaa na jamaa na demu wake wanakula denda live kila wakati mimi nashangaa iweje hawaoni aibu walinipa wakati mgumu kweli kweli chakula kilikuwa kidoogo sana sikushiba kuongeza naona noma nikavumilia tu....sikulala mpaka nafika zaidi ya masaa 9 natungua macho....
kimbembe ni kwamba nikiwa nimepiga tisheti langu na jinzi na raba zangu zile benq(za plastiki) kumbe wakati huo ni winter majuu pale air port niliipata fresh mama mmoja akanionea huruma akanipa kaniki yake nijitande....
wenyeji wangu walichelewa kwa masaa 2 machozi yalinilenga lenga huku sijui mabegi yangu yako wapi kumbe......niliteseka kwa kipindi kifupi lakini niliona kama mwaka......mbaya zaidi ngeli ilikuwa ya ugoko haipandi vizuri kuuliza.....
Kufika town mawazo yangu ni lini nitapata mtoto wa kitasha nionje ladha zao.....unajua kilitokea nini baada ya wiki kadhaa? nilipata mmoja nikajua nimeshaua kumbe akaniambia tuwe marafiki tu hata miaka mi3 nikashindwana nae.....
nyie mnakumbuka lipi?