Mara ya mwisho umepigana lin?na ulipigwa au ulipiga.

Baraka Roman

JF-Expert Member
Feb 16, 2013
692
262
Embu tujikumbushe kidogo kila mtu aseme mara ya mwisho alipigana lini na chanzo cha ugomvi kilikuwa nin?

Mie mara ya mwisho nimepigana 1997 nilivyokuwa std 2.Chanzo cha ugomvi jamaa (alinikata,alinipiga mtama wakat tunacheza mpira) tulitoka ngoma dro coz watu waliamulia.Wewe je?

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Mara ya mwisho nilipigana mwaka 90,na sijui alishinda nani kwani wote tulianguka kwenye miba na kuumia wote,finaly mwalimu alikuja akatunyuka bakora wote!
 
Nakumbuka it was 1994 nlikua form three. Nilipigana na cousin wangu mana tulikua hatuishi kugombana kama paka na chui. Siku hio kila mtu alikomaa mana yeye alinikaba hadi siku ya pili nliamka mwili wote unauma. Na yeye nlimparura na makucha hadi leo ana makovu ya kucha. Ila imekua kama dawa, kutoka siku hio hakukua na ngumi tena.
 
mie ilikuwa miaka ya 2000, tumeenda kijijin kusherekea xmas. tukiwa kwa babu kuna bomba la maji majirani huteka maji, basi vikaja vidada age yangu kuteka maji, kuonyesha mimi ni kidume tena nimetoka town nliwaletea jeuri na fuyo, mmoja wao akaniambia nitulize mzuka kama vipi atanipa kibano, kidume nikadharau gafla bint akanivamia akanipa za uso nikajidai kurusha mateke bint akadaka mguu nkaanza kuchezea za mbavu, ikabidi nitoke nduki huku ndugu zangu wakifa kwa kicheko
 
Leo, ila nimeshindwa kwa Knock out.. Yule Bazazi aliniminya **mbu nikashindwa kuvumilia nikabwaga manyanga..
 
mara ya mwisho nimefululiza kupewa kichapo.....
nimepigana na kaka angu kanipiga, kesho yake nikapigana na mdogo angu akanipiga the same week kadogo flani kakamuonea mdogo angu, kudadadeki nkajifanya kijike nkavua shati la shule kupigana nilipewa kibao kimoja tu cha mgongo nkarudi home nalia kamasi zinanitoka aaaggghhh sijapigana tena tangu siku hiyo.......
 
Ni miaka ya 90 nilipigana... Mwenzangu alikuwa na tatizo la kutoka damu puani, 2kilianzsha nagusa pua tu. Mshindi
 
Nilipigana na kondoo wetu tupo katikati ya maji mto rufiji,sitasahau niliokolewa masaa mawili baadae ufukweni.
 
mara ya mwisho nimefululiza kupewa kichapo.....
nimepigana na kaka angu kanipiga, kesho yake nikapigana na mdogo angu akanipiga the same week kadogo flani kakamuonea mdogo angu, kudadadeki nkajifanya kijike nkavua shati la shule kupigana nilipewa kibao kimoja tu cha mgongo nkarudi home nalia kamasi zinanitoka aaaggghhh sijapigana tena tangu siku hiyo.......

Ahahaha inaonekana enzi hizo ulikuwa afya mgogolo ee

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
dah niliwazingua madogo na gari lao la kamba steling mfuniko wa ndoo ndipo dereva wao akaniambia oya unganisha kamba vinginevyo ntakutoa midamu, nikabisha dah alinipa kibano hadi midamu ikanitoka it was 96
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom