OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 49,189
- 103,710
Barbara Gonzalez, alizaliwa jijini Dar es Salaam miaka kadhaa iliyopita, baba yake akiwa ni raia wa Colombia na Mama Mtanzania. Mbali na kuwa msaidizi wa Mohamed Dewji, pia alikuwa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Mohamed Foundation aliyojiunga nayo Aprili, 2016 ambayo hutoa misaada ya huduma za kijamii kwa makundi mbalimbali nchini.
Pia alihudumu katika Bodi ya Ushauri ya Taasisi ya Young African Leaders Initiative (YALI) iliyo chini ya Rais wa zamani wa Marekani, Barrack Obama ambayo lengo lake kuu ni kuwekeza katika viongozi wa kizazi cha baadaye barani Afrika.
Barbara pia alikuwa mshauri wa taasisi ya Deloitte Consulting Limited Tanzania na pamoja na hilo, alifanya kazi katika miradi kadhaa iliyo chini ya mashirika makubwa duniani miongoni mwao yakiwa ni USAID, UNICEF, Benki ya Dunia na Plan International.
Huko Deloitte ndiko mimi nilipokutana naye kwa mara ya kwanza, alikuwa na chupa ya Mo Energy akikata kiu yake maridadi kabisa. Ghafla nikasikia amekuwa CEO wa Simba baada Simba kuachwa solemba na aliyekuwa Mtendaji Mkuu wake, Senzo Mazingisa aliyejiuzulu ghafla na kukimbilia Yanga.
Baada ya kusikia stori hiyo nilimtumia ujumbe kumpa hongera mrembo huyu aliyepata shahada yake ya kwanza Chuo Kikuu cha Manhattanville College kilichopo New York, Marekani ambako alihitimu kwa ufaulu wa juu katika Sayansi ya Siasa na Uchumi.
Ujumbe wangu ulimsihi kutumia akili zoote kuipatia wadhamini wazito Simba Sc. Nikamwambia aanze sasa kutafuta mrithi wa Sportspesa,muda wake ukiishi ni kumwaga wino tu. Lakini iwe pesa ndefu kuliko timu yeyote Afrika Mashariki na Kati. Alinijibu kwa kifupi......Noted with thanks.
Nachotaka kusema wana Simba tunafarijika sana tunaposikia habari za Simba Sc kusaini mikataba na makampuni mbalimbali. Tunakupongeza na tunategemea makubwa sana katika mchakato wa kumpata mdhamini mkuu baada ya muda wa Sportpesa kuisha.
Simba Nguvu Moja