Mara: Watu wanne washikiliwa kwa tuhuma za QNET

Ila watanzania sijui vichwa vyetu vina shida gani?hivi na hali ilivyo ngumu namna hii..mtu unadiriki kutoa 5m kununua saa kweli?
 
Kuna ndugu yangu mmoja aliwahi nipigia cm kuna biashara tufanye katika familia nzima kanipendelea mimi tu.
Nkaona hii ndo bahati sasa tukapanga appointment nikaibuka kwenye nyumba flani iv wamekodi.

Nkapigwa semina masaa mawili ya Qnet (nlikua siifahamu kabla), nkawackiliza then lilipokuja suali la kujiunga nkawambia acha nikajifikirie kesho ntawaletea majibu

Basi ucku nlizama net nkafuatilia sana kuhusu huu mtandao nikaona kumbe ni magumashi.
Basi kila akiniita nkamalizie semina nkawa namzungusha mpaka kanikatia tamaa.

Sasa cku izi anaweka status mara "Next trip to Dubai, see u there Billionaires". Mara wanapost vdeo wako kwenye ukumbi mkubwa wamevaa uniform za Qnet wanacheza mziki.

Jana ndo kanimaliza kabisa kapost picha na wenziwe kila mmoja ana gari jipyaa afu akawa ameandika "Congrats billionaires, lets keep doing it".
Kinamna flan karoho kakawa kanansuta lkn najiuliza au nlifanya makosa kujiunga??? (Ni Zazibar by the way)
 
Mimi nilitegemea baada ya sakata la DECI miaka kadhaa iliyopita watu wangekuwa wamepata fundisho na kuachana na haya mambo.
Tangu nilivypoteza zaidi ya shilingi milioni moja na nusu DECI, siwezi kuja kuibiwa kipumbavu tena.
Watanzania tuamke, hakuna pesa inakuja kirahisi, bila kufuata misingi ya kiuchumi iliyothibitishwa.

Je, intelijensia ya vyombo vya usalama iko wapi? Kwanini wanakuja kuyashitukia haya makampuni ya wezi wakati watu wanakuwa wameshaibiwa tayari?
 
Kuna dada mmoja tunajuana muda mrefu akanambie ana jambo anataka kunishirikisha niende ofisini kwao,basi siku nikaenda pale kufika pale napewa maelezo ya Qnet na mtu mwingine pale kama muelimishaji akanambia blabla kibao za Qnet na salam zaó. Muelimishaji ananieleza mambo mazuri tu nikamuuliza elimu yake ana master,nambia mbona pesa rahisi namna hiyo kupata. Nani mhusika ambaye pesa yangu nikimpa nadai mimi sina haja ya saa m4.5 nikamwambia mimi sitoi pesa bila kujilithisha nikona kahamaki nikaondoka zangu mpaka sijarudi tena huko.
 
Kuna dada mmoja tunajuana muda mrefu akanambie ana jambo anataka kunishirikisha niende ofisini kwao,basi siku nikaenda pale kufika pale napewa maelezo ya Qnet na mtu mwingine pale kama muelimishaji akanambia blabla kibao za Qnet na salam zaó. Muelimishaji ananieleza mambo mazuri tu nikamuuliza elimu yake ana master,nambia mbona pesa rahisi namna hiyo kupata. Nani mhusika ambaye pesa yangu nikimpa nadai mimi sina haja ya saa m4.5 nikamwambia mimi sitoi pesa bila kujilithisha nikona kahamaki nikaondoka zangu mpaka sijarudi tena huko.
Hawa jamaa huwa ving'ang'anizi sana wanapotaka kukuingiza mkenge. Wanakupitisha kwenye pichapicha za viongozi wa serikali waliopiga picha kwenye matukio yao unaweza kuingia king usipotumia akili. Naishukuru sana JF maana ilinisaidia kuwaepuka..siku waliponiita tu ofisini kwao na kunipa fix zao breki ya kwanza ilikuwa ni kuja kuitafuta Qnet ndani ya JF...nilichokisoma kilinisaidia kuwakimbia...walinipigia simu mpaka wakakata tamaa. Big up Jf
 
Tanzania ni nchi moja ya ajabu sana sana,

Huu wizi umeanza kitambo sana na wala hakuna hatua yeyote, huwezi kuniaminisha kuwa Serikali na vyombo vyake ndo wameijua Qnet mwezi huu. Nakataa, haiwezekani.

Nadhani Serikali huwa inajua kinachoendelea ila inasubiri burungutu lijae tu ili waokote mabilioni kama ilivyokuwa kwa deci na Mr kuku. Sirikali inawachezesha upatu wananchi wake ili ipate vijisenti..................!
 
Fatilia ujue😂😂
Goodmorning billionaire!!!!!
Hawa walinikosakosa tena kwa kupitia mdogo wangu tena mhitimu mzuri wa UDSM,nilikosa pesa akanishauri niuze gari langu ili nipate milioni 6 ya kujiunga,nikamwambia mbona mnahubiri magari halafu unanishauri kuuza hili langu?Akasema nikiuza hili (old fashion)naweza pata lingine la kisasa!Duuu,nikasanuka.
Juzi ananijulisha kuwa kaagiza gari jipya lipo bandarini,nikamwambia kila lakheri.Sasa sijui hii sakuasakua km itamkosa !!!.Make nampigia hapokei simu zangu

Sent from my SM-G531H using JamiiForums mobile app
 
QNET sasa watakimbia nchini.

Wamewatapeli washkaji zangu kama 3, niliwaonya hawakunielewa ila sasa wamenielewa na wamekiri walichemka.

QNET wakitaka kukuibia wanakupiga semina halafu wanakukataza kusimwambie mtu kabisa hadi pale utakapowapa pesa, yaani ni kama vile wanakufundisha kuua mtu ama kuuza bangi. Ukishawapa pesa ndio wanakwambia kawaambie ndugu ama rafiki zako.

Kama huna hela wanakushauri uuze hata shamba ama nyumba ama uchukue mkopo bank uwape.

Bidhaa zao zinaanzia millioni 5, wanakwambia ni saa ya dhahabu ama almasi, hakuna independent valuer ambae anaweza kuthibitisha kiwango cha dhahabu ama almas kwenye saa zao.

Ila nashauri serikali iachane nao maana wanaojiunga ni watu wazima wenye akili zao, sasa mtu mzima mwenye akili timamu anachukua pesa zake anampelekea mwanaume mwingine kijinga hivyo huyo ni wa kuonea huruma?

Watu hata uwaonye vipi bado wataibiwa tu, tuliwaonya kuhusu D9, Forex, GNLD, Forever Living, One Coin, QNET bado hawakusikia juzi hapa Mr Kuku akawapiga tena mchana kweupe na bado mwingine atakuja atawapiga. Na mimi nasema wapigwe tu maana hakuna namna nyingine.
Kwa Mr.kuku nakataaa,hujawahi fatilia anachokifanya na mgawanyo wa fedha ndo Mana.
Jamaa kweli anaenndesha miradi mikubwa ya kuku na hajaanza Leo Wala Jana,Tatzo limekuja pale alipokaribisha uwekezaji na halua na elimu ya Hisa na uwekezaji ndo serikali imempigia Hapo.
Ila Talent Kama hizi zapswa kuendelezwa na kushikiliwa kwa vijana wengi wa Africa.
Mr.Kuku na QNET watu Wawili tofauti,QNET na Forex plus forever Hawa Ni matapeli kabisaaaa,Kuku Ni muwekezaji HASWAAA ktk kuku na mabanda makubwa sanaaaaaa kigamboni huko
 
Jeshi la Polisi wilayani hapa Mkoa wa Mara, linawashikilia watu wanne kwa tuhuma za kujihusisha na mtandao wa Kampuni ya QNET na kutapeli watu.

Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Dkt. Vicent Naano alisema hayo mjini hapa jana na kuongeza kuwa watu hao wanashikiliwa baada ya operesheni kufanywa na vyombo vya dola.

Alisema polisi walibaini watu wanaojihusisha na mtandao huo na jumla ya watu 25 walikamatwa baada ya uchunguzi.

Hata hivyo, Dk Naano hakuwa tayari kutaja majina ya watuhumiwa hao ingawa alisema faili kuhusu watu hao limepelekwa ofisi ya mwendesha mashtaka wa Serikali kwa ajili ya taratibu za kufikishwa mahakamani.

Alisema uchunguzi umebaini kuwa watu wengi mjini Musoma wametapeliwa na mtandao huo ikiwamo familia moja ya mstaafu wa Serikali ambayo ilitapeliwa Sh15 milioni ingawa hakuwa tayari kutaja jina la mstaafu huyo.

“Huyu mama alikuwa mtumishi pale manispaa, baada ya kustaafu alipeleka Sh5 milioni Qnet kisha binti yake akapeleka Sh5 milioni, kabla huyu mama hajampa kijana wake mwingine Sh5 milioni fedha ambazo hadi sasa hawajarudishiwa,” alisema Dk Naano.

Takukuru yamrejeshea Sh5.48 milioni mwalimu anayedai kutapeliwa na Qnet.

Alisema katika uchunguzi, wamebaini kuna watu wengi waliotapeliwa fedha zao lakini wameshindwa kufika katika vyombo vya dola kutoa taarifa huku akitoa wito kujitokeza.

Dk Naano alisema wamebaini mtandao huo hauna mwakilishi hapa nchini lakini wahusika walikuwa wakitumia taasisi nyeti ambazo ni vigumu kufahamu kama kuna shughuli za mtandao huo.

“Tumebaini walikuwa na ofisi nne hapa mjini na tayari uchunguzi unafanyika na tumefikia pazuri ingawa sitataja majina kwasasa,” alisema mkuu huyo.
Hii nchi ni ya kipumbavu. Kwahiyo hawajui zilipo ofisi za Qnet ???

Badala ya kukata mizizi, wamekomaliaa upumbavu tu.

Wanakomaa na Qnet, Qnet, halafu waneacha makampuni kibao yanafanya biashara hizo hizo.

Watawala wa nchi hii possibly ni wehu.
 
Kwa Mr.kuku nakataaa,hujawahi fatilia anachokifanya na mgawanyo wa fedha ndo Mana.
Jamaa kweli anaenndesha miradi mikubwa ya kuku na hajaanza Leo Wala Jana,Tatzo limekuja pale alipokaribisha uwekezaji na halua na elimu ya Hisa na uwekezaji ndo serikali imempigia Hapo.
Ila Talent Kama hizi zapswa kuendelezwa na kushikiliwa kwa vijana wengi wa Africa.
Mr.Kuku na QNET watu Wawili tofauti,QNET na Forex plus forever Hawa Ni matapeli kabisaaaa,Kuku Ni muwekezaji HASWAAA ktk kuku na mabanda makubwa sanaaaaaa kigamboni huko
Utakataa kwa sababu ni mmojawapo ya watu waliopigwa.

Hata QNET wana miradi mikubwa, wanasema wanafadhili Manchester City, a legitimate football Club lakini bado ni matapeli wa Ponzi scheme.

Unataka mimi nitenge muda kufuatilia pyramid scheme/Ponzi scheme ambazo zinaonekana kwa macho ya kawaida kabisa?

Huhitaji jicho la tofauti wala hata elimu ya chuo kikuu kuelewa hilo.
 
Back
Top Bottom