pantheraleo
JF-Expert Member
- Jan 5, 2013
- 691
- 878
Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ambaye pia Mkuu wa mkoa wa Mara bw Adam Malima,amegiza kukamatwa mara moja kwa Mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Kitenga pamoja na Mwenyekiti wake wa kitongoji cha Kisangura kushindwa kutoa msaada wao baada ya moto kuteketeza bweni la wasichana katika shule ya sekondari ya Imacullata wilayani Tarime tukio ambalo limetokea usiku wa kuamkia Agosti kumi na sita mwaka huu.
Katika tukio hilo wanafunzi zaidi ya sabini wakiwemo walezi wao watano katika shule hiyo wamenusurika kifo baada ya moto kuteketeza kabisa bweni lao wakiwa wamelala huku vitu vyote vya wanafunzi hao vikiteketea.
Chanzo: ITV