Mara: TAKUKURU yaokoa Bil. 1.096 Tarime

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,806
11,968
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA

TAARIFA KWA UMMA

TAKUKURU MKOA WA MARA YAOKOA TSH 1.0 96 BILIONI


Ndugu wana Habari, Kwa takriban mwezi mmoja TAKUKURU Mkoa wa MARA imekuwa ikifanya uchunguzi kuhusiana na ufisadi katika malipo ya fidia katika kijiji cha MATONGO Wilayani TARIME.

Katika uchunguzi huu TAKUKURU imeweza kubaini mambo makubwa yafuatayo:-
Kwanza, suala la tegesha katika Wilaya ya Tarime limekuwa ni donda ndugu lililokosa wa kulikemea kwa ujasiri. Suala la tegesha linao utetezi wa kisiasa na ndiyo maana hakuna mwana siasa hata mmoja kutoka chama chochote aliyewahi kusimama na kukemea uchafu na aibu ya kutegesha.

Pili, watumishi wa Serikali ambao kimsingi tulitegemea wawe mstari wa mbele kukemea tabia hiyo ndiyo walikuwa mstari wa mbele kuukingia kifua ufisadi huo na hata wengine kuwa miongoni mwa wadai katika madai hayo.

Tatu, zoezi zima lilibebwa na watu wenye nguvu za kifedha na kiwadhifa kiasi cha kutofanywa chochote kwa muda wote ambao zoezi la tegesha limekuwa likiendelea.

Kifupi tegesha ni zoezi chafu linalolitia Taifa aibu kwani linawaumiza pia wawekezaji kutoka nje, ni zoezi linalothibitisha kukosa uzalendo kwa wathamini wake na aibu kwa taaluma ya wathamini kitu kilichokwisha kuhalalishwa na hakuna aliyewahi kuingilia kati.

Uchunguzi huu ulikumbana na nguvu kali za kisiasa, kijamii kwa madai kuwa tegesha ndiyo uchumi kwa wananyamongo na kwa hiyo kujaribu kuingilia kati zoezi hili maana yake ni kuangusha uchumi wa wananyamongo. Kifupi uchunguzi ulikuwa mgumu sana.

Katika uchunguzi huu sehemu ya pili TAKUKURU ilishughulika na jumla ya chunguzi 28 zilizobainika kuwa na thamani ya Tsh 2,056,451,700/= zilifanyiwa kazi. Katika thamini hizi 28 uchunguzi chunguzi 15 zenye thamini 15 zenye thamani ya Tsh 1,119,550,915 zimekamilika. Katika uchuguzi huu TAKUKURU tulibaini kuwa kiasi cha fedha kilichotakiwa kulipwa kwa thamini hizo 15 ni Tsh 64,000,000/= tu lakini fedha zilizolipwa ni 1,119,550,915/ na hivyo kumaanisha kuwa kiasi cha 1,055,550,915/- sawa na 1,649.3% kuwa ni zao la ufisadi.

Kazi tuliyoifanya kubwa katika hatua za awali ni kuhakikisha fedha hizi zinarejeshwa kutoka mikono michafu na tumefanikiwa kwa kipindi cha mwezi mmoja kurejesha kiasi hicho cha Tsh 1,055,550,915/- ( bilioni moja na milioni hamsini na tano, laki tano na hamsini elfu mia tisa kumi na tano)

Mbali na wananchi hao 15, wapo wananchi wengine 13 ambao thamini zao zinaonekana kuwa walistahili kulipwa kiasi cha Tsh 31,444,346 badala yake kulipwa kiasi cha Tsh 936,900,785/= wamekimbia mji na hawajulikani waliko. Wananchi hao ambao akaunti zao tumezizuia kwa muda walilipwa malipo hewa ya kiasi cha Tsh 905,456,348/ kiasi ambacho ni sawa na 2,879.6% ya malipo waliyostahili kulipwa na tunaendelea kuwatafuta ili warejeshe fedha hizo.na fedha zao zipo benki. Uchunguzi wa TAKUKURU hata hivyo umebaini kuwa kiasi ambacho kilitakiwa kulipwa kupitia thamni hizi 13 ni kiasi cha 31,444,346/= na hivyo kufanya malipo ya kiasi cha 905,456,438/= kuwa ni hewa. Ufisadi huu ni sawa na 2,879.6%

Kwa hawa waliokimbia naomba kutumia nafasi hii kuwataka wajisalimishe katika ofisi za TAKUKURU Mkoa wa MARA kwa mazungumzo ya kurejesha fedha walizopokea kwa makosa vinginevyo hawatabaki salama.

Zaidi ya kuokoa fedha hizi, TAKUKURU imeendelea pia na zoezi ililolianzisha kuwasaidia wastaafu ambpo kwa mara nyingine tumeweza kuokoa kiasi cha Tsh 41,300,000/= na hivyo kufanya jumla ya fedha ambazo tumeokoa mpaka sasa (taslimu) kuwa Tsh 1,096,850,915/ kwa kipindi hiki kifupi.


Tunashukuru kwa kupewa heshima ya kusimamia uchunguzi huu ambao ni wa kwanza na wa aina yake.

Kutokana na madudu tuliyoyaibua Nyamongo, tayari TAKUKURU tumepewa kazi nyingine ya kupitia uthamini wa upanuzi wa uwanja wa ndege Musoma ambapo tayari tumeshaanza kunusa harufu ya rushwa. Chunguzi zote mbili tutaziendesha kwa pamoja.

Mwisho, TAKUKURU imepokea taarifa kwamba wapo viongozi wa juu kabisa Mkoani ambao katika kipindi hiki cha uchaguzi wamekuwa wakipita kwa wanachama wa CCM na wafanyabiashara kukusanya fedha kwa madai ya kutumwa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Tanzania DR JOHN POMBE MAGUFULI

Hadi sasa TAKUKURU imeshakusanya ushahidi wa Tsh 600,000,000/= ambazo hatuamini kama Mheshimiwa RAIS anaweza kuomba fedha kupitia njia hii. Uchunguzi unaendelea na punde tutakapoukamilisha tutawasilisha taarifa.

Tunavishukuru vyombo vyote vya usalama pamoja na Taasisi zote zilizotupa ushirikiano wakati wa zoezi hili. Kuusiana na zoezi la kupitisha wagombea, ofisi yangu inaendelea kufuatilia vitendo vichafu vya baadhi ya wagombea kushiriki moja kwa moja katika kutoa rushwa.

Asanteni kwa kunisikiliza
 
Back
Top Bottom