Mara: TAKUKURU yanusa ufisadi kwenye nyumba za ibada

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,188
4,100

1610205147183.png

TAKUKURU YANUSA UFISADI KATIKA NYUMBA ZA IBADA

Ndugu wana habari,

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoa wa Mara katika kipindi cha miezi mitatu yaani Oktoba hadi Desemba mwaka 2020, ilitekeleza majukumu yake ya kisheria ya kiuchunguzi, uelimishaji umma, udhibiti na uokoaji na urejeshwaji wa mali za umma na zile za watanzina wayonge.

Katika kipengele cha uchunguzi wa uendeshaji mashtaka, jumla ya malalamiko 233 yalipokelewa na kufanyiwa kazi. Kati ya malalamiko haya jumla ya malalamiko 76 yalihusu tuhuma za rushwa katika uchaguzi Mkuu ambapo zote zilipokelewa na kufayiwa kazi.

Hakuna tuhuma zilizoweza kuthibitika kuwa na sifa za kufikishwa Mahakamani. Kwa ujumla hakuna mgombea kwa nafasi za udiwani na ubunge ambaye hakutuhumiwa. Ofisi yangu haikuwahi kupokea malalamiko juu ya wagombea nafasi za Urais kushiriki kutoa rushwa.

Ndugu wana habari,
Katika chunguzi zingine tulizofanya tuliweza kunusa harufu ya rushwa katika Kanisa la Mennonite Tanzania Wilayani Serengeti ambapo baadhi ya watumishi na waumini wanatuhumiwa kutumia nafasi zao kuuza gari aina ya Toyota Land Cruiser mali ya Kanisa hilo kwa Tsh 10M kitu ambacho kimeleta sintofahamu miongoni mwa waumini. Gari hilo litaendelea kuwa mikononi mwa TAKUKURU hadi uchuguzi utakapokuwa umekamilika na uamuzi kufikiwa.

Ndugu wana habari,
Moja kati ya maelekezo Mheshimiwa Rais Dr John Pombe Joseph Magufuli aliyoyatoa kwa watendaji wa Serikali alipokuwa Mkoani Mara wakati wa Kampeni za udiwani, ubunge na Urais 2020 ni kuwasaidia wajane na yatima katika kuwarejeshea faraja na mali zao zilizoporwa na kuangukia mikono ya wasimamizi umiza wa mirathi.

TAKUKURU Mkoa wa Mara katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita imeweza kuchunguza na kubaini uwepo wa wasimamizi umiza wa mirathi ambapo jumla ya kiasi cha Tsh 11 bilioni, nyumba tano (05) na magari mawili (02) mali za marehemu kutoka familia tofauti zilianguikia mikononi mwa wasimamizi wa mirathi umiza na kuwaacha wajane na yatima wakihagaika. Uchunguzi upo hatua ya mwisho.

Ndugu wana habari,
Katika hatua nyingine TAKUKURU Mkoa wa Mara imenusa ufisadi wa kutisha wenye kuhatarisha maisha ya watanzania unaofanywa na Duka la Madawa ya Serikalini (MSD) Kanda ya Ziwa, kwa kusambaza madawa ya binadamu yanayokaribia au yaliyokwisha muda wake na hivyo kupoteza sifa ya kuendelea kutumiwa na binadamu.

Mchezo huu si kwamba unaathiri watumiaji wa madawa hayo bali pia kuhujumu uchumi kwani yananunuliwa kwa gharama kubwa kwa kutumia fedha za walipa kodi.

Katika uchunguzi huu tulifanikiwa kupita katika baadhi ya Hospital, vituo vya Afya na zahanati, na tulibaini uwepo wa madawa ya binadamu yaliyokwisha muda wake box 40 zenye thamani ya Tsh 155.1 M. Kibaya zaidi madawa hayo yalikuwa yakiendelea kugawiwa huku wagawaji wakijua kuwa madawa hayo yalikuwa yameisha muda.

Uchunguzi wa nani alihusika kuingiza nchini madawa yaliyokaribia kuisha muda wake au nani aliyazuia madawa hayo kugawiwa kwa wahitaji yakiwa bado hayajaisha muda wake bado unaendelea..

Ndugu wana habari,
Katika kuwarejeshea wananchi wayonge fedha walizoporwa na wakopeshaji umiza, TAKUKURU Mkoa wa Mara katika kipindi cha miezi mitatu imefanikiwa kuokoa fedha kiasi cha Tsh 63.6 M. Katika hizi kiasi cha Tsh 17.4M ni fedha zilizorejeshwa Serikalini baada ya baadhi waliobainika kukwepa kodi kubanwa na TAKUKURU na hatimaye kulipa kodi walizokuwa wakidaiwa.

Aidha kiasi cha Tsh 1.5M kilipokelewa na Wakala wa Misitu Tanzania Mkoa wa Mara kufuatia lori la mkaa tulilolikamata likikwepa kulipa ushuru. fedha zilizobaki kiasi cha Tsh 44.7m ni fedha zilizookolewa kutoka mikononi mwa wakopeshaji umiza na tulizirejesha kwa waliokuwa wameporwa ambao wengi ni walimu wastaafu. Pia trekta lenye thamani ya Tsh 39 M Mali ya Serikali tulikabidhi Serikalini Desemba 2020.

Ndugu Wanahabari,
Kwa robo ya kipindi chote cha kuanzia Januari 2021 hadi mwisho wa mwaka wa fedha Juni 2021, pamoja na mambo mengine, TAKUKURU Mkoa wa Mara inajipanga kukamilisha chunguzi zote ziazohusiana na mirathi (kiasi cha Tsh 200 bil tuhuma ambazo tumeshazipokea).

Pia tutakuwa na chunguzi juu ya matumizi ya zaidi ya Tsh 15 bil ya fedha zilizotolewa kwa wakala wa maji vijijini Mkoani Mara (RUWASA) ambazo zimetumika huku lengo la upatikanaji wa maji likiwa bado halijafikiwa.

Mheshimiwa Rais katika kampeni zake kila alikopita pia aliahidi kutatua pamoja na mambo mengie tatizo la maji hasa kwa wananchi waishio vijijini. Ni jukumu letu kama TAKUKURU kuhakikisha kuwa ahadi hii inasimamiwa.

Chunguzi zote zinazohusu maji zinatakiwa kuwa zimekamilika ifikiapo Februari 2021 ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa.

Aidha, tumepanga kuwa tutakuwa na KLINIC INAYOTEMBEA kuwafuata wananchi hasa wasio na uwezo wa kufika katika ofisi zetu kwa lengo la kuwasikiliza na kutatua kero zao huko huko. Hii itafanywa kila siku ya Ijumaa kwa ratiba itakayokuwa imepangwa. Kliniki hii inaanza mwezi huu na pia itashirikisha idara zote zinazohudumia jamii katika mkoa wa Mara.
 

Attachments

  • OKTOBA DESEMBA 2020.docx
    74.9 KB · Views: 6
Hawa siku wakiingia IKULU Wataeleweka,
Sijisumbui hata kusoma ujinga,
Kuna mambo ya 1.5trn wamekaa kimya,uchaguzi 2020 kimya,
Ni mbwa koko tu,wanabwekwa hovyo...
 
Wakati huo huo ufisadi wa kutisha pale Ikulu wanaufumbia macho! Kazi kweli kweli kuwa na hizi taasisi UCHWARA zinazofanya kazi kwa matakwa ya mtu mmoja.
 
Back
Top Bottom