Mara: Siasa zimeanza Kupamba Moto CCM na CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mara: Siasa zimeanza Kupamba Moto CCM na CHADEMA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mgeni wenu, Jan 11, 2012.

 1. m

  mgeni wenu JF-Expert Member

  #1
  Jan 11, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 3,669
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Hii ni wiki ya Mapambano ya Kisiasa kati ya vyama viwili Mkoani Hapa,CHADEMA na CCM ambapo Wabunge na viongozi Waandamizi wa vyama hivyo wakipita Kueleza mambo mbalimbali ya Mkoa na Jimbo kwa Ujumla ikiwemo Katiba Mpya
  Kundi La CCM likiongozwa na Mawaziri(Wasira na Gaudentia Kabaka)linapata wakati Mgumu sana kwa wananchi hasa walipokuwa Tarime na Jana Serengeti ambapo ilibidi Hotuba zikatizwe Mara kwa Mara kutokana zomea zomea ya Wananchi hasa walipoulizwa"Mlikuwa wapi kutufunza Katiba ya Zamani kwanza ili tujue jinsi ya kuitofautisha na Mpya na walipokosa majibu viwanja vilivyofurika vilianza zomeazomea.
  Kwa upande wa Chadema ambao Leo wataanzia Viwanja vya Shule Ya msingi Mkendo watakutana na Maswali ya kwa nini wamekuwa na Tabia ya kutoka Bungeni na kwa nini walizuia Michango mashuleni wakati Wazazi wapo tayari kuchanga,ikiwemo ni kipi kiliwapelekea kufarakana Tarime na kuliachia Jimbo lirudi CCM,kwa upande wa CHADEMA wataongozwa na Mbunge pekee wa CHADEMA(Mara) Vincent Nyerere baada ya Ester Matiko kuomba udhuru kuwa Hatokuwepo kutokana na sababu za kifamilia.Leo pia MH Nyerere atakabidhi Madawati na kuitaja Miradi inayotekelezwa aliyoiahidi pamoja na Utekelezaji wa Ilani ya Jimbo lake na Ile ya Chama chake......Nawasilisha
   
 2. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #2
  Jan 11, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Wassira ameshachoka, hana ushawishi wowote kwa wanaMara na kwa ccm yeye ndo anaonekana afadhali.

  Mama Kabaka bado ni mchanga katika siasa pamoja na kukaa bungeni zaidi ya miaka sita sasa. Hana mvuto na ushawishi kwa wananchi pamoja na kujitahidi sana lakini wanaTarime hawajamkubali.

  Ni muhimu uongozi wa chadema mkoa na Taifa wamuongezee nguvu mh. Vicent Nyerere katika kukabiliana na ccm hasa kipindi hiki cha vuguvugu la katiba mpya.
   
 3. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #3
  Jan 11, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu hapo kwenye wekundu:

  1. Kwa hiyo maswali watakayoulizwa tayari unayo? wewe ndiyo utayauliza? Mimi nilidhani ni maswali ya papo kwa papo kumbe siyo
  2. Nyerere anatekelezaje ilani ya Chama chake wakati Chama hakiko madarakani?
   
 4. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #4
  Jan 11, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu hapo pekundu si hang over ya mfumo dume uliokomaa huko Tarime kwa Wanyamongo, Watimbaru, Wakira, Walenchoka, Wairege, nk.?
   
 5. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #5
  Jan 11, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Nawaambieni ya kwmb hiyo chichiem kukutana na wakati mgumu ni mfano tu.
  Tusubiri na mwone hapa Arusha,nawaambia ya kwamba wasijaribu hata kuipandisha kale kabenderea yao kakijani maana raia hawataki hata kuiona wala.

  Viva CDM!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 6. m

  mgeni wenu JF-Expert Member

  #6
  Jan 11, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 3,669
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  @kimbunga
  Hayo nitamuuliza mimi kama una maswali yako yaweke hapa ili nimuulize Vincent Nyerere
   
 7. nashy

  nashy JF-Expert Member

  #7
  Jan 11, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 679
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  waambie hao magamba wajiandae hata mimi nakuja Serengeti 2015 ni yetu chadema, wamwambie huyo mbunge anayejiita Dr kebwe kwamba nashy ninakuja kuyavua magamba huko
   
 8. o

  oldonyo JF-Expert Member

  #8
  Jan 11, 2012
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 554
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  we uko wapi?hivi unajua halmashauri ya mji wa musoma inaongozwa na nani?ccm musoma mjini ni chama cha upinzani kati ya kata zote waliambulia kama kata tatu hivi kama sijakosea nadhani utakuwa umenielewa.
   
 9. m

  mgeni wenu JF-Expert Member

  #9
  Jan 11, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 3,669
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Katika kata 13 kata mbili ni za CUF,kata3 ni za CCM na kata 8 ni za CHADEMA, kwa hiyo ILANI ya Chadema ndo iliyokubaliwa na wana Musoma na ndo maana inabidi itekelezwe
   
 10. m

  mgeni wenu JF-Expert Member

  #10
  Jan 11, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 3,669
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Mkutano umeanza na Watu ni wengi saaana
   
 11. m

  mgeni wenu JF-Expert Member

  #11
  Jan 11, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 3,669
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Mlioko Bunda mtujuze Wassira na kundi lake linaendeleaje?
   
 12. M

  Mrdash1 JF-Expert Member

  #12
  Jan 11, 2012
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,379
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Siyo kujiita, Dr. Kebwe ni daktari mhitimu wa chuo kikuu cha udaktari muhimbili miaka 19 hivi iliyopita, wa nyumbani kusanya nguvu kama kweli unataka kukabiliana na daktari
   
 13. M

  Mwl Ryoba Member

  #13
  Jan 11, 2012
  Joined: Oct 28, 2011
  Messages: 55
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  huyu bwana amemsahau kamanda Marwa (Chadema) aliye mtikisa kebwe
   
 14. m

  mgeni wenu JF-Expert Member

  #14
  Jan 12, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 3,669
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Kwa sasa msimtikise mumtoe Kabisa
   
 15. m

  mgeni wenu JF-Expert Member

  #15
  Jan 12, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 3,669
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Leo CCM watakuwa makutano ya Nyankanga wakiongozwa na Wasira,Mkono na Dr Steven Kebwe...,,Chadema japo jana walifunika viwanja vya Mkendo ila leo hatuna taarifa zao wako wapi Mwenye Taarifa atujulishe,Jana CCM bunda walipata wakati Mgumu sana katika Mkutano
   
 16. j

  jigoku JF-Expert Member

  #16
  Jan 12, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,347
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Siku nyingine mkuu uweke basi na picha za mahudhurion maana wengine tuko mbali huku.lakini pia angalizo tu ulete taarifa kama uhalisia ulivyo ili tuendelee kupima na kujifunza,maana hawa magamba mimi sitaki hata kuwaona wakiendelea kufanya ufisadi.Nakerwa sana na hiki kitu wanachokiita katiba mpya,maana walishachafua hali ya hewa tayari.walaaniwe kabisa
   
 17. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #17
  Jan 12, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Vipi pale Mkendo kati, mpaka kule maeneo ya beach bado ni vijiwe vya vijana wa Chadema wanashinda wanakunywa gongo na kuvuta bange!
   
 18. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #18
  Jan 12, 2012
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Akili ya mwenye suruwali fupi fupi hii
   
 19. m

  mgeni wenu JF-Expert Member

  #19
  Jan 12, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 3,669
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  @ritz ndo vijana ambao waliahidiwa ajira na ugumu wa maisha ndo unafanya tunywe Gongo japo bia twazitamani,Mbunge wetu nae Hanunui bia ye amekazana na Madawati na Madarasa sisi tule Madawati?
   
 20. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #20
  Jan 12, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Poleni sana, kuna sehemu inaitwa majita kuikona, maskani ya Chadema kuna vijana wanakunywa gongo na viroba kama maji
   
Loading...