Waitara: CHADEMA inapokea ruzuku ya sh 329 milioni kila mwezi, Dr Mashinji analipwa mshahara sh 7mil kwa mwezi!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,832
141,749
Aliyekuwa mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara yupo mubashara Clouds 360 anaelezea jinsi ruzuku ya chama inavyofisadiwa.

Mwita anadai mbunge wa Tarime John Heche alipokuwa mwenyekiti wa Bavicha alikuwa analipwa mshahara sh 1.5 mil kila mwezi kinyume cha utaratibu.

Anadai wabunge wa viti maalumu ndio mtaji wa Mbowe pale CHADEMA.

Anadai yeye ndio mbunge bora wa jiji la Dsm, amejenga madaraja na hospitali pale Chanika na kwamba wakati wa mafuriko wapiga kura wake huja nyumbani kwake kupata hifadhi.

Kadhalika anadai ameondoka Chadema baada ya Mbowe na Dr Mahanga kumhakikishia kuwa hataitishwa kugombea tena 2020.

Mwita anadai mwaka 2008 alihama CCM na kwenda Chadema baada ya kugombana na aliyekuwa Katibu mkuu mzee Makamba na yule mwenyekiti wa UVCCM Dr Nchimbi.

Amesisitiza kuwa amejiuzulu ubunge muda huu baada ya kuona kuna fursa ya yeye kurudi tena bungeni katika uchaguzi mdogo kwa tiketi ya CCM hivyo hakuna atakachopoteza. Pia amedai yeye hakuutaka uenyekiti bali alitamani sana Mwenyekiti wa chama taifa awe Tundu Antipas Lissu.

Amemaliza kwa kusema ameshachukua fomu ya kugombea tena ubunge wa Ukonga na kwamba katika mazingira ya kisiasa akitokewa na baya lolote atamhisi Mbowe!

Source: Clouds tv!
 
Mashinji akikamilisha miradi yake yote nae atahamia CCM very Smart ngenya!
qRI8Gs7.gif
 
Back
Top Bottom