Mara nyingine moyo huzungumza yaliyo moyoni wakati wa hasira

Kosae1

JF-Expert Member
May 16, 2016
211
151
Nimesoma mahali. Mnadhani ni kweli wadau?

Ukiona boyfriend au girlfriend wako mnaopendana kabisa, wakati mmepishana au mna hasira akakutamkia huwezi kuwa mume wangu au huwezi kuwa mke wangu, jiulize sana. Kuna kitu kimefichika kwenye moyo wake usichokijua.

Yamkini mpo tu kwa sababu ya kutimiza mambo fulani fulani. Kimsingi kwako haoni thamani ya mke au mume ambaye moyo wake unamdhihirishia. Ni bora kuwa mpole na kuanza kufikiri upya.
 
Sio kweli, sio mara zote lazima iwe hivyo...

Mara nyingi usimuamini mtu anayeongea akiwa katika mihemko,
Kuna wakati mtu anapoongea kwa hasira lengo ni kukuudhi tu!
Pia usimuamini mtu anayezungumza na wewe akiwa na furaha kupitiliza, kwa sababu anaweza kukuahidi jambo ambalo hawezi kulitimiza baada ya furaha kuisha.

Haya mambo hayana formula mkuu...
 
Mkasirishe kabla hujamuoa. Moyo hushinda vyote na kupasuka ka jipu lililoiva, halichagui mahali ulipo au saa ya kupasuka kwani linataka kutoka
 
Eeh, wee ukitaka kuujua jambo lililojificha moyoni mwa mtu msubiri akikasirika.
 
Nimesoma mahali. Mnadhani ni kweli wadau?

Ukiona boyfriend au girlfriend wako mnaopendana kabisa, wakati mmepishana au mna hasira akakutamkia huwezi kuwa mume wangu au huwezi kuwa mke wangu, jiulize sana. Kuna kitu kimefichika kwenye moyo wake usichokijua. Yamkini mpo tu kwa sababu ya kutimiza mambo fulani fulani. Kimsingi kwako haoni thamani ya mke au mume ambaye moyo wake unamdhihirishia. Ni bora kuwa mpole na kuanza kufikiri upya.
Freudian's slip of tongue
 
Hiyo ni kweli kwa 100%. Mara nyingi watu wakiwa na hasira hushindwa kuji-control na kujikuta wanatoa matamko ambayo angekuwa calm angeweza kijizuia. Kwahiyo ni kweli usipuuze maneno aliyokutamkia mwanamke wakati akiwa na hasira maana kwa kiasi kikubwa huo ndio uhalisia wake.
 
Back
Top Bottom