sinajinasasa
JF-Expert Member
- Dec 10, 2013
- 2,989
- 4,129
Ila dogo unaonekana una mastory sana, hheerehKulikuwa mtoto mmoja wa kiume wa brother wangu mmoja. Alikuwa mtukutu sana. Kesi shuleni(primary) haziishi, kila wakati "uje na mzazi wako"
Akiitwa mzazi, alikuwa ananiomba niende. Baada ya majadiliano, nawaomba radhi sana Walimu wake.
Hitimisho inakuwa viboko sita vya makalioni kutoka kwa mzazi. Nakabidhiwa kiboko. Nilikuwa nacharaza bakora kisawasawa. Toto halitowi hata chozi.
Jioni tukikutana nyumbani, maneno yake:
"Daa! Baba mdogo anachapa fimbo kuliko hata Mwalimuu!!
Uzuri wa yule mtoto, kichwani alikuwa yuko vizuri.
Paaap! akafaulu darasa la saba, akapelekwa shule moja nzuri sana Mkoa wa Pwani. Ile karibia anamaliza form two, akamlamba mwenzie ngumi za uso, akafukuzwa shule.
Brother akawazaa, akaona ngoja amtafutie shule moja private ya watemi watupu, kwao makonzi ya kichwa ni kama kutafuna karanga.
Akaipata Tanga mjini. Dogo likapigana kitemitemi mpaka likamaliza form four.
Baba yake akawa ameishapoteza matumaini kabisa hata maendeleo yake hafatilii.
Siku ambayo sitakuja kuisahau ni siku ambayo Dogo anamkabidhi baba yake matokeo ya mitihani ya form four.
Brother alicheka, alicheka, mpaka akakaa chini!! Kulikoni?
Dogo limepaform, limepiga division one, point 16 yenye misonge miwili, Mathematics na Physics!!
Toka siku hiyo wakawa marafiki kama mtu na mdogo wake!