Mara: Mzazi ampiga mwalimu na kumjeruhi baada ya kumuadhibu mwanae

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,007
9,873
Mwananchi mmoja aliyejulikana kwa jina la Nyimano Ghati mkazi wa kata ya Nkende Halmashauri ya mji wa Tarime Mkoani Mara amedaiwa kumpiga na kumjeruhi mwalimu wa shule ya msingi Nkende Mwl. Edina John kwa madai ya kuwa mtoto wake anayesoma shule hiyo alipewa adhabu na mwalimu.

Kufuatia tukio la mwalimu wa shule ya msingi Nkende kupigwa na mzazi, viongozi wa kamati ya shule hiyo wameitisha kikao cha dharula ili kuzungumzia tukio hilo ambapo diwani wa kata Nkende, Daniel Komote amelaani kitendo hicho na kuwaomba walimu waendelee kufanya kazi kwa ufanisi.
 
Adhabu ya vibiko ifutwe, kuna watoto wengine ata ukipiga ndio kwanza hata shule hatakanyaga tena, suala la adhabu ziangaliwe adhabu nyingine ambazo watoto wataweza kuzihimili.
 
We umefika hapo ulipo kwa viboko leo unaomba vifutwe...
 
Mwananchi mmoja aliyejulikana kwa jina la Nyimano Ghati mkazi wa kata ya Nkende Halmashauri ya mji wa Tarime Mkoani Mara amedaiwa kumpiga na kumjeruhi mwalimu wa shule ya msingi Nkende Mwl. Edina John kwa madai ya kuwa mtoto wake anayesoma shule hiyo alipewa adhabu na mwalimu.

Kufuatia tukio la mwalimu wa shule ya msingi Nkende kupigwa na mzazi, viongozi wa kamati ya shule hiyo wameitisha kikao cha dharula ili kuzungumzia tukio hilo ambapo diwani wa kata Nkende, Daniel Komote amelaani kitendo hicho na kuwaomba walimu waendelee kufanya kazi kwa ufanisi.
Huo ni ubabe wa kijinga, mwanafunzi huyo afukuzwe hapo shuleni na mzazi wake akatafute shule ya kulipia, hapo atakuwa anapigwa yeye ada na mtoto hataguswa
 
Madogo wa skuizi bila stiki hawaendi na wana dharau sana tena baadhi wanataka hadi kupigana na waalimu wao!

Huyo mwanafunzi afukuzwe shule, mzazi nae sheria zimuadabishe. Sheria zipo zifatwe tu na zitumike ipasavyo kwa wote waliozikiuka.
 
Back
Top Bottom