Uchaguzi 2020 Mara: Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Bupilipili amewataka Wenyeviti wa Mitaa na Vijiji Wilayani humo kusimamia Ulinzi na usalama kipindi hiki cha Uchaguzi

Nyanswe Nsame

Senior Member
Jul 9, 2019
158
175
DC Bunda atoa agizo kwa wenyeviti wa mitaa, vijiji - uchaguzi mkuu

Mkuu wa Wilaya ya Bunda mkoani Mara, Lydia Bupilipili amewataka wenyeviti wa mitaa na vijiji wilayani humo kusimamia masuala ya ulinzi na usalama katika maeneo yao hususani kipindi hiki cha uchaguzi mkuu.

Amesema pamoja kusimamia Ulinzi na Usalama, pia wanapswa kushiriki katika shughuli za maendeleo katika maeneo yao ili kuwa mfano kwa wananchi wanao waongoza.

Bupilipili amesema, katika kipindi cha uchaguzi kumekuwepa na matukio mbalimbali ya wizi wa mifugo katika maeneo mbalimbali hivyo wenyeviti hao wanapaswa kuchukua hatua.

Ametaja maeneo ambayo yanaongoza kwa wizi wa mifugo kuwa ni Kinyabwiga na manchemailo ambako wananchi wanaibiwa mifugo yao pamoja na mali zao nyingine.

Amesema ulinzi na usalama ndio nguzo muhimu ya maendeleo ya wananchi kwa kuwa endapo watu watafanya shughuli zao kwa amani watasaidia kuchangia katika pato la taifa.

Bupilipili ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na wenyeviti wa mitaa na wenyeviti wa vijiji wilayani humo ambapo amewataka kushughulika na matatizo ya wananchi kuanzia ngazi za vijiji na mitaa kabla ya kufika ngazi za juu

Amesema amekutana na Wenyeviti hao ili waweze kufahamu wajibu na majukumu yao ya msingi ikiwa ni pamoja na namna ya kusimamia masuala ya maendeleo.

"Alafu wizi wa mifugo unafanyika kwa wajane tu ambao wameachiwa mifugo na waume zao lakini watu wengine hawaibiwi na unakuta wizi unafanyika na mwenyekiti yupo na viongozi wengine wa kijiji wapo.

"Unaweza kukuta sasa hivi watu wanapiga soga (stori) lakini madarasa hayatoshi hawana zahanati na mwenyekiti wa kijiji yupo, ndio maana tunasisitiza mwenyekiti wa kijiji kusimamia hilo.

"Ili tuendelee kuwa katika uchumi wa kati lazima kila mtu awe na uhakika wa maisha yake, miradi yake na shughuli mbalimbali za kimaendeeo bila kuingiliwa na kubughuziwa na mtu mwingine," amesema Bupilipili.

Katika hatua nyingine, Bupilipili amewataka wananchi kuhakikisha wanajiunga katika bima za afya iliyoboreshwa inayotolewa kwa Shilingi 30,000 kwa familia nzima kipindi cha mwaka mmoja.

Amesema viongozi wa vijiji wanapaswa kuwahimiza wananchi kufahamu umuhimu wa bima ya afya kwa kuwa afya ndio msingi mkubwa wa binadamu kwa kuwa bila kuwa na afya shughuli za maendeleo haziwezi kufanyika.

Kwa upande wake, Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la kutetea Haki za Wanawake na wasichanaa Kivulini Yassin Ally, amesema pamoja na viongozi hao (wenyeviti) kusimamia shughuli za maendeleo na amani kwenye mitaa yao bado kumeibuka changamoto.

Ally alieleza kuwa, wenyeviti wengi wamekuwa chanzo cha ukatili kwa wanawake na watoto kutokana na kuendelea kuchukua tozo iliyopewa jina la tozo ya meza inayosababisha kuendelea kuwepo kwa migogoro.

Amesema tozo zinazotozwa na wenyeviti hao, hazina viwango na mwongozo maalumu pia hazina risiti halali ya serikali inayotoa uhalali wa wao kutoza.

Amesema tozo hizo zimekuwa kikwazo kwa wahanga wa ukatili, ubakaji, ndoa za utotoni na migogoro ya ndoa ambazo Serikali inaeleza wahanga wa ukatili wanapaswa kupata huduma ndani ya saa 72.

Ally ameiomba Serikali kutoa mwongozo kwa wenyeviti wa mitaa vijiji na vitongoji nchini kuondoa kero hiyo ya tozo kwa wahanga wa ukatili wa kijinsia na ndoa za utotoni kwa kuwa hakuna mwongozo uliyotolewa na Serikali ya wao kutoza fedha ambayo haina kiwango maalumu.

Mkuu huyo wa wilaya amekutana na wenyeviti wa vijiji 78 na wenyeviti wa mitaa 88 uliofanyika ukumbi wa halmashauri ya Bunda mji.

........... MWISHO...............
 
Back
Top Bottom