MARA: Mbunge wa Serengeti(CHADEMA), Mwl Marwa Ryoba Chacha ajivua uanachama na kujiunga CCM

Mbunge wa jimbo la Serengeti kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mhe. Marwa Ryoba Chacha amejivua uanachama wa chama hicho na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) muda mfupi uliopita kwa kile alichodai kuunga mkono juhudi za Mhe. John Pombe Magufuli katika kuwaletea wananchi wa Tanzania maendeleo.

Amesema hajashurutishwa na yeyote kuchukua maamuzi haya.

Marwa amewasihi wana Serengeti kumchagua wanayeona anafaa, anayeunga mkono juhudi za Mhe. Rais Magufuli katika kuleta maendeleo.

Akitangaza kujivua uanachama amesema,

Mimi Marwa Ryoba Chacha, mbunge wa jimbo la Serengeti na mwanachama wa CHADEMA, leo tarehe 27/08/2018 nimeamua kwa hiari yangu mwenyewe bila kushinikizwa na mtu yeyote kujivua uanachama wa CHADEMA na kujiunga na Chama cha Mapinduzi. Nawaomba wananchi wa Serengeti, mlinipa imani kubwa ya kuwatumikia lakini imefikia sehemu kupitia CHADEMA naona kama siwatendei haki.

Nimeamua nijivue uanachama na kujinga na chama cha mapinduzi ili kuunga mkono juhudi za maendeleo ambazo anazifanya Rais Magufuli. Niwaombe wananchi wa Serengeti, nafasi ipo kwenu chagueni mtu mnayemuona anawafaa kuwawakilisha ambaye ataungana na Rais Magufuli kuwaletea maendeleo.
Asanteni sana.

VIDEO:

Hongera sana mla
 
Jamaa kagundua kua hata uchaguzi ukiitishwa Chadema watasusia atapita bila kupingwa.

Tubadili katiba, kama mtu anataka kuhama chama ahame bila kutuingiza kwenye hasara za uchaguzi.

Nchi hii bado masikini, vipaumbele ni vingi sana, pesa iende kwenye mambo ya msingi na sio kila siku ni uchaguzi.

By t way kuna majimbo zaidi ya 150 ya yanayoongozwa na ccm toka 2015, wabunge wake wanaunga mkono CCM since then, sioni tofauti yake ya maisha na majimbo yasiyo ya CCM. Kuunga mkono au kutounga sijaona tofauti.

Tufanye wabunge wote wa upinzani waunge mkono jitihada za rais, je itabadili hali yetu ya maisha na kua mazuri zaidi, Tanzania itaanza kutiririka maziwa na asali? Kwamba kutokuunga mkono ndio kunazuia hayo?

Mwalimu alipambana na matatizo kama ujinga, maradhi, nk lakini hili la ujinga bado ni tatizo. Mtu anasema akiunga mkono analeta maendeleo, mbona maendeleo hayapo kwenye wabunge ambao ni wa ccm toka 2015?

Asante kwa wazo la pekee kwa huu mwezi!! Umeongea point ya maana sana mkuu. Mungu atusamehe watz kwa ujinga wa wabunge wetu!
 
Hizi zama zitapita na huu ujinga utapita tu.

Hoja ya Zitto kuhusu kile kifungu inazidi kupata nguvu kadri siku zinavyokwenda.

Kamwe hamtakuja kuniona namuunga mkono huyu mtu maana ni sawa na mhujumu uchumi.
Kwani we una umuhimu gani hata kwa tarafa yako??sana sana unaongeza idadi ya watu wasio na umuhimu wowote nchini
 
H
Jamaa kagundua kua hata uchaguzi ukiitishwa Chadema watasusia atapita bila kupingwa.

Tubadili katiba, kama mtu anataka kuhama chama ahame bila kutuingiza kwenye hasara za uchaguzi.

Nchi hii bado masikini, vipaumbele ni vingi sana, pesa iende kwenye mambo ya msingi na sio kila siku ni uchaguzi.

By t way kuna majimbo zaidi ya 150 ya yanayoongozwa na ccm toka 2015, wabunge wake wanaunga mkono CCM since then, sioni tofauti yake ya maisha na majimbo yasiyo ya CCM. Kuunga mkono au kutounga sijaona tofauti.

Tufanye wabunge wote wa upinzani waunge mkono jitihada za rais, je itabadili hali yetu ya maisha na kua mazuri zaidi, Tanzania itaanza kutiririka maziwa na asali? Kwamba kutokuunga mkono ndio kunazuia hayo?

Mwalimu alipambana na matatizo kama ujinga, maradhi, nk lakini hili la ujinga bado ni tatizo. Mtu anasema akiunga mkono analeta maendeleo, mbona maendeleo hayapo kwenye wabunge ambao ni wa ccm toka 2015?
Aya yote unaongea kujifariji..ukweli unaujua..hivi watoti wa mwenye nyumba na watoto wa mpangaji nani ana uhuru kwa baba mwenye nyumba..?? Je watoto wa mpangaji wana haki sawa sawa na watoto wa mwenye nyumba..?? Baki na ukweli kwa moyo wako.
 
Hizi zama zitapita na huu ujinga utapita tu.

Hoja ya Zitto kuhusu kile kifungu inazidi kupata nguvu kadri siku zinavyokwenda.

Kamwe hamtakuja kuniona namuunga mkono huyu mtu maana ni sawa na mhujumu uchumi.
Wewe ni mmoja na mtu mdogo sana usijilinganisha na mbunge,kazania cdm majibu unayo,humuamlii mbunge kukaa cdm kwa ujinga uliomo,taswira ya chama ni ubora wa chama siyo malalamiko na kulialia
 
Sio kihivyo kama unavyodhani! ila naona huu kama ujinga flan, anyway kupanga ni kuchagua, hata angekuwa wa chama gani ni maslahi kwa familia yake!
Ni ujinga kwako ila ni kutua mzigo kwa mhamaji.
Huwezi kubaki Chadema ukishinikizwa kupinga kila zuri la serikali hata kama zuri hilo linahusu jimbo lako ..hiyo ni sawa na kujibebesha zigo la misumari.
 
H

Aya yote unaongea kujifariji..ukweli unaujua..hivi watoti wa mwenye nyumba na watoto wa mpangaji nani ana uhuru kwa baba mwenye nyumba..?? Je watoto wa mpangaji wana haki sawa sawa na watoto wa mwenye nyumba..?? Baki na ukweli kwa moyo wako.
una maanisha nini? Kwamba Tanzania kuna wapangaji na wenye Nyumba? Du?hizi siasa uchwara zinazofanya either na watu waliofeli shule au walioenda shule kukariri tu maandishi vitabuni ili wafaulu mitihani inatuharibia nchi sana
 
Jamaa kagundua kua hata uchaguzi ukiitishwa Chadema watasusia atapita bila kupingwa.

Tubadili katiba, kama mtu anataka kuhama chama ahame bila kutuingiza kwenye hasara za uchaguzi.

Nchi hii bado masikini, vipaumbele ni vingi sana, pesa iende kwenye mambo ya msingi na sio kila siku ni uchaguzi.

By t way kuna majimbo zaidi ya 150 ya yanayoongozwa na ccm toka 2015, wabunge wake wanaunga mkono CCM since then, sioni tofauti yake ya maisha na majimbo yasiyo ya CCM. Kuunga mkono au kutounga sijaona tofauti.

Tufanye wabunge wote wa upinzani waunge mkono jitihada za rais, je itabadili hali yetu ya maisha na kua mazuri zaidi, Tanzania itaanza kutiririka maziwa na asali? Kwamba kutokuunga mkono ndio kunazuia hayo?

Mwalimu alipambana na matatizo kama ujinga, maradhi, nk lakini hili la ujinga bado ni tatizo. Mtu anasema akiunga mkono analeta maendeleo, mbona maendeleo hayapo kwenye wabunge ambao ni wa ccm toka 2015?
bajeti yake hipo; unataka ipigwe kama ESCROW.
Ndo maana ya DEMOCRASIA
 
Hizi zama zitapita na huu ujinga utapita tu.

Hoja ya Zitto kuhusu kile kifungu inazidi kupata nguvu kadri siku zinavyokwenda.

Kamwe hamtakuja kuniona namuunga mkono huyu mtu maana ni sawa na mhujumu uchumi.
Hayo ndio matunda ya Demokrasia...

Lowassa na genge lake walitoka CCM wakajiunga na CHADEMA..

Lazaro Nyalandu alijiuzuru Ubunge akajiunga na CHADEMA...

Hivi wewe umuunge au usimuunge mkono JPM kuna kitu kitabadilika kweli?...Zaidi ya humu JF kuna sehemu yoyote unajulikana?....Unajikuta mtu maarufu na una faida kwa nchi hii..😅😅😂😂
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom