Mara: Jafo asimamisha shughuli za uchenjuaji mtambo wa Double F

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,000
9,861
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Selemani Jafo amesitisha shughuli za uchenjuaji dhahabu katika mtambo wa Double F katika kijiji cha Nyakisya, wilayani Tarime kutokana na uchafuzi wa mazingira.

Alitoa agizo hilo jana mkoani Mara baada ya kupokea malalamiko ya wananchi kuhusu athari za kiafya na kimazingira zinazo sadikika kutokana na kemikali ya cyanide inayotumika katika shughuli za uchenjuaji wa dhahabu na kutiririka katika chanzo cha maji cha Senye.

Akitoa malalamiko kwa niaba ya wakazi wa maeneo hayo, Mwenyekiti wa Mtaa wa Nyakihenene, Mwita Ngusui alisema wakazi wengi na vitongoji vya jirani kwa kiasi kikubwa wameathirika na kemikali hiyo.
Baada ya kusikiliza malalamiko hayo, Jafo alisema kikosi kazi kinachoundwa na taasisi za serikali pamoja na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Mamlaka ya Mkemia Mkuu na Bodi ya Bonde la Ziwa Victoria watachunguza na kutoa taarifa za kitaalamu kuhusu maji hayo ili hatua stahiki kuchukuliwe.

Alisema ofisi yake haitamvumilia mwekezaji yeyote anaeharibu mazingira na kuathiri afya za watu.
Katika hatua nyingine, Jafo amebaini ukiukwaji wa Sheria ya Mazingira ya mwaka 2004 kwa mgodi huo wa Double F kwa kuanza shughuli ya uchenjuaji bila kufanya tathmini ya athari kwa mazingira.

Alimwelekeza Msimamizi wa Mtambo huo, Is-haka Juma kuwalisiliana na ofisi za NEMC mapema iwezekanavyo ukaguzi wa mazingira ufanyike.

Mbunge wa Rorya, Jafari Chege alishukuru serikali kwa kusikia kilio cha wananchi wa Rorya na kufanya ufuatiliaji wa haraka.

HabariLeo
 
Alisema ofisi yake haitamvumilia mwekezaji yeyote anaeharibu mazingira na kuathiri afya za watu.
Katika hatua nyingine, Jafo amebaini ukiukwaji wa Sheria ya Mazingira ya mwaka 2004 kwa mgodi huo wa Double F kwa kuanza shughuli ya uchenjuaji bila kufanya tathmini ya athari kwa mazingira.

Je watendaji wake atawavumilia kwakutotimiza wajibu wao?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom