Mara: Askari watano JKT washikiliwa kwa tuhuma za mauaji

Lumoge

JF-Expert Member
Apr 1, 2020
610
1,000
Mafunzo ya kijeshi hayo yamepitwa na wakati. Mbona nchi nyingine wanajeshi ni watu wapole sana? Kuna sehemu nilifanya kazi yenye wanajeshi wa USA. Ni wapole na waungwana kweli kweli japo muda wote walikuwa wanatembea na silaha kiunoni. Mkipishana mlangoni ni lazima asuburi upite kwanza.
Upo sahihi kimsingi moja ya majeshi ambayo askari wake wamestaarabika ni jeshi la USA. Yani Wana utu mno kwa raia.
 

mlima wa mizeituni

JF-Expert Member
Sep 7, 2019
628
1,000
Kwanza nina hamu mie?
Kuna afande km wa 3, wawil wa kiume na m1 wa kike, walikua wananichukia hataree, hata sijui niliwakosea nn, walinitesa mie had nilijuta kuwafahamu.

Siku ya mwisho ya maagano na kukabidhi combat, wanajifanya kuomba msamaha na kuniambia nisiwe na moyo wala roho ya kisasi, huenda tutaktan sehem nyingne nikashindwa hata kuwapa msaada, jaman yan wale watu siwasamehe kamweeh.
Tatizo lako ulitaka kuleta ka'umaarufu'.. watu wenye ka'umaarufu' hawajawahi kuachwa salama!
 

Patra31

JF-Expert Member
Apr 24, 2020
3,012
2,000
Hiyo a.k.a ya marehemu imenifikirisha sana bila kupata jibu.
Kwa kawaida tulio wai ishi musoma mtu akiitwa/akijiita baga(mabaga) inamaana ni mlemavu.
 

Marathon day

Senior Member
Jan 31, 2020
163
250

polisi%20site.jpg

Jeshi la Polisi mkoani Mara linawashikilia askari watano wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) waliokuwa wamemaliza muda wao wa kujitolea, wakisubiri ajira za muda wa Kikosi cha Jeshi la Wananchi 27 KJ MAKOKO kwa tuhuma za mauaji ya mkazi wa Rwamlimi manispaa ya Musoma, Paulo Joseph, maarufu kama ‘Baga’ kwa madai ya kumshambulia kwa kipigo askari mwenzao.

Kamanda wa polisi mkoa wa Mara Kamishina Msaidizi wa Jeshi la Polisi Longinus Tibashibwamu amethibitisha kushikiliwa kwa askari hao wa JKT, ambao pia wanadaiwa kuwakamata na kuwapiga raia wengine 5, akiwemo dereva wa gari ya abiria inayofanya safari zake kati ya Bweri na Mjini kati yenye namba za usajili T 108 CXK Michael Mrema.

Mkuu wa Kikosi cha Jeshi la Wananchi 27 KJ MAKOKO Kanali Mushashi amekutana na familia ya marehemu Paulo Joseph kwa ajili ya kutoa zpole juu ya kifo hicho huku akiahidi kushirikiana na wafiwa katika shughuli zote za msiba huo kwani waliohusika na mauaji ya kijana huyo mwenye umri wa miaka 35, wapo chini yake.
Ila hai hawajaajiriwa kwahiyo ni kosa kwaita askari, nijuavyo JKT ni chuo cha mafunzo, ukihitimu na kuajiriwa unaofanya mafunzo ya uaskari JWTZ, ( TPDF) so hao tuwaite bado ni MA SERVICE, sio askari. Nadhani tuweke sawa hili kwanza.
 

Isanga family

JF-Expert Member
Feb 25, 2015
8,947
2,000
Ulikosa ajira jwtz sio bure au itakua walikugongea mke maana sio kwa povu hilo
Unazungumzia ajira unakuta yeye kaajiri Watanzania kibao JF ina watu ww endelea kudharau ukibahatika kukutana nao live hautaamini na utaacha kuwadharau usiowajua na kejeli zisio na maana...
 

JUAN MANUEL

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
3,611
2,000
Hawa vijana hamnazo kabisa,
Ubabe wao wakiwa wengi,Kule Dar Kawe,wanadungwa visu na mateja mpaka unashangaa.
 

uttoh2002

JF-Expert Member
Feb 3, 2012
6,077
2,000
Kitu cha kwanza kwa askari aliyeiva vizuri ni nidhamu. Bila hivyo askari bado hajaiva. Maneno ni mawili tu Jeshini, "Ndiyo afande" na "Hapana afande" full stop. Na unapokea amri kutoka kwa dogo uliyemzidi umri hata kwa miaka 10

Okay, nidhamu ya ndiyo na Hapana kwa AFANDE tu, huko uraini ni ndiyo kipigo!
 

Godo

JF-Expert Member
Apr 11, 2017
336
500
Ili liwe funzo kwa vijana wapuuzi wanaovimba mtaani kisa wamepata mafunzo na hawatambuliki popote zaidi ya kuambiwa wao ni akiba,kesi iendeshwe inavyotakiwa wale vifungo vya maisha wote wate kama mi huwa sina huruma nao haiwezekani ukatishe maisha ya binadamu mwenzako kijinga jinga tu, hao jamaa huku mtaani hawana ishu wengi ni darasa la saba na wenye four za 32 wamefundishwa uzalendo na kujiajiri kwenye nyanja mbalimbali hasa kilimo lakini raia akivaa kikofia kina vinembo vya jeshi la nchi nyingine watampiga hadi basi na ndio maana kuna mtu analalamika kuwaajiri hamfai sababu wengi wao ni wavuta bangi na walioshindikana wakaamua kwenda huko bora kuchukua watu mtaani wenye nidhamu hau mashuleni na vyuoni moja kwa moja.
 

Magabo

Member
May 20, 2021
85
125
Okay, nidhamu ya ndiyo na Hapana kwa AFANDE tu, huko uraini ni ndiyo kipigo!
Ahaa!! Uraiani kwa Askari aliyeiva vizuri: Unakatwa klofi la uso na raia, jibu lako: "Asante sana Bro! Hayo ni moja ya mazoezi tunayopewa kambini. Tafadhali hebu ongeza Kofi la pili!"
 

uttoh2002

JF-Expert Member
Feb 3, 2012
6,077
2,000
Ahaa!! Uraiani kwa Askari aliyeiva vizuri: Unakatwa klofi la uso na raia, jibu lako: "Asante sana Bro! Hayo ni moja ya mazoezi tunayopewa kambini. Tafadhali hebu ongeza Kofi la pili!"
Labda kanisani madhabahuni
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom