Mara: Askari watano JKT washikiliwa kwa tuhuma za mauaji

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
3,615
2,000

polisi%20site.jpg

Jeshi la Polisi mkoani Mara linawashikilia askari watano wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) waliokuwa wamemaliza muda wao wa kujitolea, wakisubiri ajira za muda wa Kikosi cha Jeshi la Wananchi 27 KJ MAKOKO kwa tuhuma za mauaji ya mkazi wa Rwamlimi manispaa ya Musoma, Paulo Joseph, maarufu kama ‘Baga’ kwa madai ya kumshambulia kwa kipigo askari mwenzao.

Kamanda wa polisi mkoa wa Mara Kamishina Msaidizi wa Jeshi la Polisi Longinus Tibashibwamu amethibitisha kushikiliwa kwa askari hao wa JKT, ambao pia wanadaiwa kuwakamata na kuwapiga raia wengine 5, akiwemo dereva wa gari ya abiria inayofanya safari zake kati ya Bweri na Mjini kati yenye namba za usajili T 108 CXK Michael Mrema.

Mkuu wa Kikosi cha Jeshi la Wananchi 27 KJ MAKOKO Kanali Mushashi amekutana na familia ya marehemu Paulo Joseph kwa ajili ya kutoa pole juu ya kifo hicho huku akiahidi kushirikiana na wafiwa katika shughuli zote za msiba huo kwani waliohusika na mauaji ya kijana huyo mwenye umri wa miaka 35, wapo chini yake.
 

Magabo

Member
May 20, 2021
85
125
Kitu cha kwanza kwa askari aliyeiva vizuri ni nidhamu. Bila hivyo askari bado hajaiva. Maneno ni mawili tu Jeshini, "Ndiyo afande" na "Hapana afande" full stop. Na unapokea amri kutoka kwa dogo uliyemzidi umri hata kwa miaka 10
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom