Mara: Adaiwa kumuua aliyemuondoa harusini kwa kukosa zawadi

Polisi Wilaya ya Serengeti wanamshikilia Changwa Sebeki (19) mkazi wa Kijiji cha Merenga kwa tuhuma za mauaji ya Kegoka Mwikwabe (22) anayedaiwa alimuondoa kwenye harusi kwa kukosa zawadi.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Mara, Danilel Shillah leo Jumapili Novemba mosi ameliambia Mwananchi kwa njia ya simu kuwa tukio hilo limetokea jana Oktoba 31 majira ya saa 1.30 jioni kijijini hapo.

"Mtuhumiwa alimkatakata kwa panga na kusababisha kifo chake. Sababu ni kuwa katika harusi moja, marehemu alikuwa anasimamia vijana (wanaocheza na binti) kutoa zawadi lakini mtuhumiwa alicheza (na binti) na alipoambiwa atoe zawadi (kama ilivyo kwa taratibu za Kikurya), hakuweza kutoa hivyo akatolewa nje.

“Kutokanana kitendo hicho (kilichofanyika mwaka jana), mtuhumiwa huyo aliweka kisasi moyoni na alipokutana jana na aliyemtoa harusini akaamua kumkata.

Kamanda Shillah amesema wanatarajia kumfikisha mtuhumiwa mahakamani kwa kosa alilotenda na amewataka wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi.
Hivi maana ya kujichukulia sheria mkononi ni nini kwa mustakabali wa tukio hili. Naona polisi wanaropoka ki mazoea sasa.
 
Haya mambo mengine yanafurahisha na kuhuzunisha at the same time.

Let's meet at the top, cheers 🍻
Hawa jamaa kuna ulazima wa kuwapeleka maabara kujua nini chanzo. kuna yule ticha walimpiga mkuki kwa issue ndogo tu
 
Tumeumbwa ku-generalize ila tunakosea sana maana kila mwanadamu kaumbwa na tabia yake kuna watu kutoka Mara ni waastarabu na wapple hasa hata ikitokea mmeonana huko kwenye vikao akajitambulisha ni mzaliwa wa mara utakataa....

Hivyo tusipende kuhukumu Ms. Witness...
 
Tumeumbwa ku-generalize ila tunakosea sana maana kila mwanadamu kaumbwa na tabia yake kuna watu kutoka Mara ni waastarabu na wapple hasa hata ikitokea mmeonana huko kwenye vikao akajitambulisha ni mzaliwa wa mara utakataa....

Hivyo tusipende kuhukumu Ms. Witness...
Vry true mkuu, nimekupata
 
Hii mijitu ina mambo ya ajabu sana, sijui tuwapelekee alshabab wawanyooshe kidogo!😂😂 leo tena limetokea tukio la mtu kuuwa mkewe na shemeji zake huko bukoba.
 
Mi ndo mana sipendi wakurya
Naona kama akili zao sio nzuri
Hashindwi kukufanya lolote,Wana spirit ya ukatili hivi.
Juzi hapa nasoma habari jamaa kammwagia mkewe maji yalokuwa yanachemka kiss kachelewa kumpikia ugali..
Kwan we nani anakupenda?Kione hiki nacho
 
Back
Top Bottom