Mara: Adaiwa kumuua aliyemuondoa harusini kwa kukosa zawadi

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
2,940
2,000
Polisi Wilaya ya Serengeti wanamshikilia Changwa Sebeki (19) mkazi wa Kijiji cha Merenga kwa tuhuma za mauaji ya Kegoka Mwikwabe (22) anayedaiwa alimuondoa kwenye harusi kwa kukosa zawadi.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Mara, Danilel Shillah leo Jumapili Novemba mosi ameliambia Mwananchi kwa njia ya simu kuwa tukio hilo limetokea jana Oktoba 31 majira ya saa 1.30 jioni kijijini hapo.

"Mtuhumiwa alimkatakata kwa panga na kusababisha kifo chake. Sababu ni kuwa katika harusi moja, marehemu alikuwa anasimamia vijana (wanaocheza na binti) kutoa zawadi lakini mtuhumiwa alicheza (na binti) na alipoambiwa atoe zawadi (kama ilivyo kwa taratibu za Kikurya), hakuweza kutoa hivyo akatolewa nje.

“Kutokanana kitendo hicho (kilichofanyika mwaka jana), mtuhumiwa huyo aliweka kisasi moyoni na alipokutana jana na aliyemtoa harusini akaamua kumkata.

Kamanda Shillah amesema wanatarajia kumfikisha mtuhumiwa mahakamani kwa kosa alilotenda na amewataka wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi.
 
kuku sharo

Senior Member
Aug 13, 2020
111
250
Bangi tu hizo, yaan tukio la kijinga hilo tena la mwaka jana ndo unalipa kisasi leo!

Au kuna sababu nyingine nyuma ya pazia!
 
Abigail Nabal

JF-Expert Member
Sep 2, 2020
463
1,000
Mi ndo mana sipendi wakurya
Naona kama akili zao sio nzuri
Hashindwi kukufanya lolote,Wana spirit ya ukatili hivi.
Juzi hapa nasoma habari jamaa kammwagia mkewe maji yalokuwa yanachemka kiss kachelewa kumpikia ugali..
 
Abigail Nabal

JF-Expert Member
Sep 2, 2020
463
1,000
Aah na wamepinda kwelikweli, nawaona hapa job
Kuna mmoja alimkatalia binti mimba.binti akafanya intelijensia hadI akapajua kwa jamaa,kafika ghafla kazama ndani jamaa haamini.zogo likaanza.
Halafu jamaa ni wale askari wa mambosasa,alivua ile mkanda wa sare zao alimpiga vibaya binti wa watu.watu mtaani tunasikia mayowe ya nguvu,mbio tukamsaidie tunakuta binti anapigwa.jamaa kwa aibu ya Watu akaacha,binti akafunguka yote jamaa ikabidi ahame kwa aibu hata kodi haijaisha...
 
witnessj

JF-Expert Member
Mar 22, 2015
19,904

Mmmh kweli makatili duuh!

Na hawako romantic kabisa, ni ubabe kwa kwenda mbele

Huyu wa job yeye kila siku anamzibua mke wake mingumi na miteke, kisa mke kuhoji jamaa kurudi saa 9 usiku every day

Halafu linajisifu hapa job ukatili wake ptuu
 
Abigail Nabal

JF-Expert Member
Sep 2, 2020
463
1,000
Mmmh kweli makatili duuh!

Na hawako romantic kabisa, ni ubabe kwa kwenda mbele

Huyu wa job yeye kila siku anamzibua mke wake mingumi na miteke, kisa mke kuhoji jamaa kurudi saa 9 usiku every day

Halafu linajisifu hapa job ukatili wake ptuu
Hii
Anasimulia hayo matendo yake kwenu na kujisifia?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom