Mapya yaibuka sakata la mtuhumiwa wa mauwaji ya Mwangosi

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
[h=3][/h]


Karandika lililobeba mahabusu wengine likiwasili mahakamani hapo bila ya mtuhumiwa wa mauwaji ya Daudi Mwangosi
Askari polisi wakiweka ulinzi kumziba mwenzao asipigwe picha leo
[h=5]Mtuhumiwa wa mauwaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa Chanel Ten mkoa wa Iringa Daudi Mwangosi , askari mwenzao mwenye namba G2573 Pasificus Cleophace Simoni (23) akiingia katika gari la polisi lenye namba za usajili PT 1404 huku ulinzi ukiwa umeimarishwa kuzuia wanahabari wasipige pich[/h]

[h=5]Wanahabari wakiwa wamejipanga kwa picha wakisubiri mtuhumiwa kuletwa mahakamani hapo [/h][h=5] SAKATA ya mauwaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha Chanel Ten mkoani Iringa marehemu Daudi Mwangosi limeendelea kuchukua sura mpya mkoani Iringa baada ya askari polisi anayetuhumiwa kuhusika na mauwaji hayo kufichwa katika gari maalum na askari wenzao .[/h]
Tukio hilo lilitokea leo wakati mtuhumiwa huyo akifikishwa mahakamani huku askari polisi hao muda wote walionekana kuzunguka huku na kule katika mahakama hiyo kama njia ya kuwathibiti wanahabari waliokuwepo mahakamani hapo wasipate nafasi ya kumpiga picha mtuhumiwa huyo ambaye ni askari mwenzao mwenye namba G2573 Pasificus Cleophace Simoni (23)


Hata hivyo kabla ya kuingia karandika la mahabusu wengine gari ya polisi aina ya Toyota yenye namba za usajili PT 1404 ikiwa na askari zaidi ya 10 ilifika katika viwanja hivyo vya mahakama na kuegeshwa pembeni bila ya mtuhumiwa huyo aliyekuwa amefunikwa sura yake kwa kofia na kufichwa kabisa sura yake kuonekana huku akiwa amekaa mbele kwa dereva huku akifichwa na askari mwenzake pasipo kushuka.



Zikiwa zimebaki kama dakika 10 mahakama kuanza gari hilo lilisogea hadi mlango wa Mahakama na askari waliokuwepo mahakamani hapo zaidi ya 20 kulizunguka gari hilo huku wengine wakiwathibiti wanahabari akiwemo mwandishi wa habari hizi kama njia ya kuzuia kupigwa picha kwa mtuhumiwa huyo na baada ya kuingia ndani ya mahakama kabla ya hakimu kufika uthibiti ndani ya chumba cha mahakama ulikuwa mkali zaidi dhidi ya wanahabari hasa wale wenye kamera.



Wakati huo huo Mahakama ya hakimu mkazi wa wilaya ya Iringa imeahirisha kesi hiyo ya mauwaji ya mwanahabari Daudi Mwangosi ambae pia alikuwa ni mwenyekiti klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IPC) ,mtuhumiwa huyo askari mwenye namba G2573 Simoni (23) atafikishwa tena mahakamani hapo Desemba 5 mwaka huu kesi hiyo itakapo tajwa tena.
[h=5]
Mwendesha mashitaka wa jamhuri Adolf Maganda aliieleza mnahakamani hiyo mbele ya hakimu Dyness Lyimo kuwa mtuhumiwa huyo mnamo 02 Septemba mwaka huu katika kijiji cha Nyololo Wilaya ya Mufindi Mkoa wa Iringa alimuua Daudi Mwangosi kwa makusudi kinyume na kifungu cha sheria namba 148 kifungu kidogo 5A.i cha makosa ya jinai.
[/h][h=5][/h][h=5]
Kwa mujibu wa kesi za jinai, sheria kifungu 196 kanuni ya adhabu Cap. 16 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002, kinakataza mtuhumiwa wa mauaji ya kukusudia kupewa dhamana.​
[/h][h=5][/h][h=5]

Habari na Picha kwa Hisani ya Francis Godwin
[/h]
 
wengine wamehukiwa juzi kunyongwa hawa bado wanamkinga muuaji asionekane? Hayo si sehemu ya majukumu ya Askari shupavu , wazalendo na wanaojua kazi zao. Askari makini na shujaa anatambua wajibu wake yuko tayari kumkamata hata bosi wake pindi akiwa na ushahidi wa ukiukwaji anaoufanya je si zaidi kwa huyu muuaji?
 
hata walio hukumiwa kunyongwa iko siku mtasikia wako mitaani kwani walitimia kazi waliotumwa na ccm sasa kwanini askali huyu ashitakiwe kama siyo tunazugwa tu..
 
IMG_4781.JPG

Mtuhumiwa wa mauwaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa Chanel Ten mkoa wa Iringa Daudi Mwangosi , askari mwenzao mwenye namba G2573 Pasificus Cleophace Simoni (23) akiingia katika gari la polisi lenye namba za usajili PT 1404 huku ulinzi ukiwa umeimarishwa kuzuia wanahabari wasipige picha.

Mbona anayeingia kwenye gari ni mwanamke?
 
Huyu jamaa hata akaunti ya fB hana. Uki google kupata info zake, hakuna! Kaazi kweli kweli
 
Nijuavyo mimi auaye kwa upanga atakufa kwa upanga!
Watamzuiazuia sasa hivi, lakini siku ikifika atashindwa hata kutumia mikono yake kujiziba!
Time speaks!....loudly!
 
Inawezekena kila siku ya kesi anapelekwa mtu mwingine, ndio maana hawataki aonekana.
 
one day one time kitafahamika tuu. kila jambo lina mwisho wake na hata haya ya usanii katika kesi hii yatafika mwisho
 
kwani kuna siri gani wanayoificha hapa si inafahamika ya kuwa jamaaa ndo alihusiaka na mauaji ya mwangosi kulikoni leo hii wanamficha lengo lao nini hasa hawa askari wenzake
Hata kama wanamficha watu wasimuone mbona kwenye picha anaonekana vizuri kwenye vieo ya youtube
Wasiwasi wangu ni kuwa hawa jamaa wanampango wa kuchakachua suala hili ili huyu jamaa hapo baadae aaciwe huru bila raia kujua kwa kudanganya umma kuwa jamaa amefungwa jela kumbe changa la macho na watu mpango huu wamekwishasitukia
 
Watamkinga mpaka watachoka tu, manake itatajwa sana kabla ya kuanza kusikilizwa.
 
hata walio hukumiwa kunyongwa iko siku mtasikia wako mitaani kwani walitimia kazi waliotumwa na ccm sasa kwanini askali huyu ashitakiwe kama siyo tunazugwa tu..

Mkuu wale wametolewa kafara maana wamemuua mtoto wa mkubwa na wadau wengi wa Tabora waliifuatilia ile kes, familia ya marehemu ina jina kubwa kuliko hao maaskari, sidhani kama wangemuua muuza mitumba wa Manzese hukumu ingekuwa hivyo. Usishangae ukiambiwa huyo askari aliugua na amefariki gerezani na akazikwa 'kimtindo' kama Balali na kesi ikaishia hapo maana anachukuliwa kama shujaa na si mtuhumiwa.
 
Hivi ni sawa kwa mhalifu kufichwa sura yake, na alipokua kizimbani pia walifanya hivyo?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom