Mama Obama
JF-Expert Member
- Mar 5, 2016
- 1,621
- 1,087
Wana JF kuna mambo mapya yanayozidi kujitokeza tangu rais Magufuli awasimamishe maafisa wakuu wa Taasisi ya TMAA inayosimamia MADINI ambayo pia ilimfanya rais Magufuli kumvua Uwaziri Mh.Muhongo kama Waziri wa Madini kwa sababu zilizo wazi.
Inavyosemekana ni kuwa mwaka wa 2009 TUME maalumu iliyojulikana kama PRESIDENTIAL MINING REVIEW COMMISSION,iliyoongozwa na JAJI Mark Bomani. Tume hii ilitoa MAPENDEKEZO kuwa SMELTER ijengwe hapa nchini.
Lakini cha kushangaza ni kuwa maafisa hao wa TMAA wakawa tayari wamekuwa COMPROMISED na Makampuni husika yaani WAKAHONGWA ili WAYANYAMAZISHE matakwa ya Tanzania Kuwa na UWEZO wake na TEKNLOJIA HIYO.
Katika mbinu zao za kuzima ripoti na mapendekezo ya tume TMAA, miaka sita iliyopita hivi wakaanza mipango ya KUYAMWAGIA MAJI mapendekezo YOTE ya Tume ya Jaji Mark Bomani ili KUIDHOOFISHA kabisa
Na mwishowe KUZIZIMA kabisa NDOTO za Watanzania kuwa na mitambo yao ya SMELTER.
Na hivyo KUTUSALITI sawasawa ili tuendelee KUIBIWA VIZURI na hayo Makampuni.
Mwaka wa 2011 MAAFISA wa TMAA walitembelea miji ya TOKYO na SAGANOSEKI Copper concentrate Smelter nchini JAPAN ili WAJIONEE wenyewe TEKNOLOJIA hiyo na jinsi nchi yetu inavyoweza KUJIJENGEA Smelter yake yenyewe.
Katika safari yao ilikuwa pia wajue GHARAMA za UWEKEZAJI/UJENZI na uwezo na gharama za uendeshaji nchini.
Ikikikumbuka kuwa tume ya Jaji Mark Bomani ilikuwa pia imeenda huko kabla wakati ikiandika na kuchukuwa DATA, ili kutayarisha ripoti mpya ya sheria ya MINIMG LAW/Sheria mpya za MADINI.
Mwaka 2011 TMAA nao wakatoa ripoti yao iliyojulikana kama:
"A STUDY on VIABILITY to CONSTRUCTING a COPPER Concentrate SMELTER in Tanzania"
Ripoti yao ILIPINGA VIKALI mapendekezo ya Tume ya Jaji Bomani.
Na hivyo Kuwaachia wezi field day ya kuiba mchanga wetu WATAKAVYO na WAPENDAVYO. Maana tayari TMAA walikuwa wamekuwa compromised/WAMEHONGWA.
Kwa wale wanaolaumu uamuzi wa Rais Magufuli na kupendelea Makampuni wanaposikia haya si WAONE HUZUNI kuwa hakika TULIIBIWA Vya KUTOSHA na IMETOSHA?
Na Tanzania INAWEZA kabisa KUJIJENGEA yenyewe hiyo MITAMBO.
Maana NIA TUNAYO na UWEZO TUNAO tukishikana pamoja na kushirikiana kama Watanzania
HAKUNA lolote ambalo Tanzania HAITALIWEZA KULIFANYA.
Kwa Maafisa kama hawa wa TMAA WALIOTUSALITI wanastahili kuwa JELA bila HURUMA.
Hatuwezi kuwa taifa la OMBAOMBA wakati kila RASLIMALI tunayo.
Na hali watu wachache wenye tamaa wanataka tubaki Maskini huku wao wakijenga magorofa
TUNAKATAA kama Watanzania.
Mungu IBARIKI Tanzania na Rais Magufuli.
Chanzo: The EastAfrican.
Rais Magufuki ameunda uadui mkubwa na Viongozi kutoka pande zote, chama chake na Upinzani. Wale wote waliokuwa wakivuna bila ya kuwa na mashamba wamemukalia kooni na kuimba demokrasia. Wanasema tulisema, lakini Sasa wamegeuka wanasema anafukuza wawekezaji, makampuni yanafungwa, anachukuwa pesa za watu kwenye mabenki. Nchi yeyote ukiwa na mali ambazo hazijuikani umezipata wapi, na hauna record ya kodi yamapato serikaini utachunguzwa na mali zako kutaifishwa.
Tumekuwa na wawekezaji waliofanya biashara miaka NENDA miaka rudi wanasema wanapata hasara lakini hawaondoki wala hawafungi biashara hawa ni wezi wa kodi za Watanzania. Tanzania imeibiwa sana na wawekezaji kama hawa wakisaidiwa na baadhi ya Viongozi wetu waliojitajirisha na ndiyo hao Sasa wanaotumia pesa zao kuichafua serikali ya Tanzania chini ya Dr Magufuli kwa jina la demokrasia.
Demokrasia gani inayopatikana kwa kuifirisi nchi na kuwafanya watu kuwa masikini wa kutupa, na wachache kuwa matajiri wa kupindukia kwa kuwaibia wengi. Kenya ina katiba nzuri na uhuru wakumuita hata Rais nyani, lakini haiwasaidii wananchi, Wananchi wanasema,, wanandamana na kupigwa mabomu lakini viongozi wanaiba bila ya kujali demokrasia. Wezi hawafungwi na na Kila uchaguzi wakenya wanakufa kwa mamia. Leo tunamusikia Tundu Lissu akisema demokrasia ya ukweli iko Kenya bila ya aibu. . Tumepata bahati kumpaka Rais amejitosa kupambana na hawa wezi, Sasa anaitwa dictator na muuwaji wa watu kwa mapanga. Hii yote ni kazi ya wezi wachache waliojitajirisha kwa mali ya wizi. Sasa wanatumia pesa zao kumufanya Rais ashindwe kuiongoza Tanzania.
Wapinzani walimusifu Rais Magufuli kuwa anafanya kazi waliokuwa wakitaka, na anapigna na ufisadi kama waivyokuwa wakitaka. Sasa wanasema na kumuita dictator. Sasa wanayatetea makampuni makubwa kuwa ameyabana na anafukuza wawekezaji. Tundu Lissu ALISEMA majaji wanahongwa. Rais Magufuli akawapanguwa, na kuhioji Safari zao za gharama pesa wanapata wapi, za kusafiri nchi za nje na familia zao Kila mala, Tunamusikia Tundu Lissu Sasa anawatetea na kusema wanaruhusiwa kusafiri na kulipiwa na serikali. Amefanya mazungumuzo na Acacia, kabula ya mazungumuzo kukamilika, tayari mtu kama Tundu Lissu anamuzomea kwenye television ya dunia kuwa hajalipwa hata senti moja, utafikiri pesa hizo Rais Magufuli akili-was ataziweka mifukoni mwake. Hata Kama hatuelewani kwenye siasa, ugonvi wa mali yetu wote lazima tuwe pamoja, lakini kuna wale watu wachache wanaollipwa na mafisadi na makampuni makubwa wanafanya Kila njia Rais Magufuli ashindwe kuiongoza nchi ili waendelee kujitajirisha wenyewe na kuwaacha mamilioni ya Watanzania masikini.