Mapya yaibuka: Maafisa wa TMAA walipewa hela ili Smelter isijengewe Tanzania

shige2

JF-Expert Member
Oct 11, 2016
8,106
3,967
Wana JF kuna mambo mapya yanayozidi kujitokeza tangu rais Magufuli awasimamishe maafisa wakuu wa Taasisi ya TMAA inayosimamia MADINI ambayo pia ilimfanya rais Magufuli kumvua Uwaziri Mh.Muhongo kama Waziri wa Madini kwa sababu zilizo wazi.

Inavyosemekana ni kuwa mwaka wa 2009 TUME maalumu iliyojulikana kama PRESIDENTIAL MINING REVIEW COMMISSION,iliyoongozwa na JAJI Mark Bomani. Tume hii ilitoa MAPENDEKEZO kuwa SMELTER ijengwe hapa nchini.

Lakini cha kushangaza ni kuwa maafisa hao wa TMAA wakawa tayari wamekuwa COMPROMISED na Makampuni husika yaani WAKAHONGWA ili WAYANYAMAZISHE matakwa ya Tanzania Kuwa na UWEZO wake na TEKNLOJIA HIYO.

Katika mbinu zao za kuzima ripoti na mapendekezo ya tume TMAA, miaka sita iliyopita hivi wakaanza mipango ya KUYAMWAGIA MAJI mapendekezo YOTE ya Tume ya Jaji Mark Bomani ili KUIDHOOFISHA kabisa
Na mwishowe KUZIZIMA kabisa NDOTO za Watanzania kuwa na mitambo yao ya SMELTER.
Na hivyo KUTUSALITI sawasawa ili tuendelee KUIBIWA VIZURI na hayo Makampuni.

Mwaka wa 2011 MAAFISA wa TMAA walitembelea miji ya TOKYO na SAGANOSEKI Copper concentrate Smelter nchini JAPAN ili WAJIONEE wenyewe TEKNOLOJIA hiyo na jinsi nchi yetu inavyoweza KUJIJENGEA Smelter yake yenyewe.

Katika safari yao ilikuwa pia wajue GHARAMA za UWEKEZAJI/UJENZI na uwezo na gharama za uendeshaji nchini.

Ikikikumbuka kuwa tume ya Jaji Mark Bomani ilikuwa pia imeenda huko kabla wakati ikiandika na kuchukuwa DATA, ili kutayarisha ripoti mpya ya sheria ya MINIMG LAW/Sheria mpya za MADINI.

Mwaka 2011 TMAA nao wakatoa ripoti yao iliyojulikana kama:
"A STUDY on VIABILITY to CONSTRUCTING a COPPER Concentrate SMELTER in Tanzania"

Ripoti yao ILIPINGA VIKALI mapendekezo ya Tume ya Jaji Bomani.
Na hivyo Kuwaachia wezi field day ya kuiba mchanga wetu WATAKAVYO na WAPENDAVYO. Maana tayari TMAA walikuwa wamekuwa compromised/WAMEHONGWA.

Kwa wale wanaolaumu uamuzi wa Rais Magufuli na kupendelea Makampuni wanaposikia haya si WAONE HUZUNI kuwa hakika TULIIBIWA Vya KUTOSHA na IMETOSHA?
Na Tanzania INAWEZA kabisa KUJIJENGEA yenyewe hiyo MITAMBO.

Maana NIA TUNAYO na UWEZO TUNAO tukishikana pamoja na kushirikiana kama Watanzania
HAKUNA lolote ambalo Tanzania HAITALIWEZA KULIFANYA.

Kwa Maafisa kama hawa wa TMAA WALIOTUSALITI wanastahili kuwa JELA bila HURUMA.

Hatuwezi kuwa taifa la OMBAOMBA wakati kila RASLIMALI tunayo.
Na hali watu wachache wenye tamaa wanataka tubaki Maskini huku wao wakijenga magorofa
TUNAKATAA kama Watanzania.
Mungu IBARIKI Tanzania na Rais Magufuli.
Chanzo: The EastAfrican.
 
Maneno mengi utekelezaji sifuri!!!

Kama hao TMAA na ACACIA ni waongo si serikali ijenge basi hizo smelters!!! Serikali ikijenga, tunawatoza gharama ndogo hao ACACIA wanaosema not economical kwa wao kujenga smelters.

Nadhani gharama zetu zitakuwa very affordable kwa sababu tunaamini ujenzi wa hizo smelters not expensive kama akina TMAA wanavyosema!!

Ile ripoti ya TMAA mie nimeisoma mara nyingi sana!! Wengi wenu humu mnaangalia wanasiasa wamesema nini!!!

Mosi, TMAA hawakusema smelters zisijengwe bali bali walisema not commercially viable. Hata hivyo, wakapendekeza nini cha kufanyika to make the whole thing viable.

Moja ya mambo waliyokuwa wameyataja ni kiasi cha mchanga kinachozalishwa na nishati ya ku-run hiyo mitambo!!!!

Kwa upande wa Barrick, wao walisema "not economical TO US" kujenga smelters!!

From economic point of view, mtu anaposema not economical haimaanishi kwamba kujenga ni hasara!

However, kwavile wamesema "not economical to us (acacia)" manake kuna better option kwao kuliko kujenga smelters. Hiyo ndiyo tafsiri ya not economical!

Lakini ambacho "not economical" kwa Barick/Acacia/investor kinaweza kuwa very economical kwa serikali. This so because, wakati ACACIA wanaangalia economic benefits serikali inatakiwa kuangalia socio-economic benefit!!

Mbona simple tu!!!!

Ah! Nimekumbuka! TUSIKODISHE!

Hawa Acacia si wanasema tani 20 zina 3kg za dhahabu wakati Ripoti ya Wazalendo inasema tani 20 zina wastani wa 28kg za dhahabu?! It's OPPORTUNITY for us!

Tunajenga smelters kisha tunanunua hayo makinikia kwa thamani ya mineral composition inayoripotiwa na Acacia!! Kwamba, tani 20 za makinikia zina 3kg ONLY!

Tunanunua na tunafanya processing wenyewe... hapo tutakuwa tumepata 28kg from the very single container!

Tena turahisishe mambo! Hitimisho la Kamati ya Wazalendo kama ambavyo iliripotiwa hapa JF inasema:
Kwa ujumla thamani ya metali/madini yote katika makinikia kwenye makontena 277 yaliyozuiliwa bandarini, ni TZS bilioni 829.4 kwa kutumia viwango vya wastani na TZS bilioni 1,438.8 kwa kutumia viwango vya juu. Kwa kuwa viwango hivi vya thamani havitumiki kukadiria mapato ya Serikali, ni wazi kuwa kuna upotevu mkubwa sana wa mapato kwa nchi yetu.
Viwango hivyo hapo juu ni wastani wa Sh. 1.134 Trillion just for a single trip!!!

Aidha, Mheshimiwa Rais nae akaripotiwa akisema:
Kuna kamati inayotaka kujua makontena yanasafirishwa mangapi, haraka haraka ni makontena 250 na 300 kwa mwezi, kwa mwaka zaidi ya makontena 3600.
Kama kontena 277 zina thamani ya Sh. 1.134 trillion, this means kontena 3600 zinazosafirishwa kwa mwaka zitakuwa na thamani ya Sh. 14.74 Trillion!!!

TUtakuwa stupid tusivyo-grab hiyo opportunity!! Halafu si tunasema smelters zinauzwa bei rahisi tu.... hivi wapi tunaweza kupata biashara kubwa kama hiyo!!!!!

Haya sasa... badala ya maneno meeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeengi; hususani wale wazalendo (sio akina sie) basi tufanye hima tumshawishi Rais Magufuli aachane na mpango wa ndege na badala yake tuwekeze kwenye smelters na hayo makinikia tunanunua wenyewe, tunayo-process wenyewe na kwa hesabu hizo hapo juu, hatukosi Trillion 10 as net profit kwa mwaka!!!
 
Hawa wazungu wa ajabu sana hata nyama ya kitimoto inayoliwa mgodini inatoka sauzi na kenya eti hatuna teknolojia ya kufuga mbuzi wetu

Hata nyanya na mbogamboga zinatoka sauzi eti kila kitu hatuna teknolojia

Sasa kama kila kitu hatuna basi na madini hatuna teknolojia ya kuwa nayo wakatafute nchi nyingine sisi acha tuendelee kuchimba kwa moko siku kitu kikihira nchi nzima inafaidi kuliko sasa mara mrahaba sijui marahaba
 
Foolish TMAA, wanyongwe mahayawani wakubwa. Kwani hiyo smelter inatoka kwa Mungu? Hakuna kinachoshindikana kuwepo hapa kwetu kama tayari kipo duniani. Ingeweza kuwa ni condition kubwa ya mwekezaji yeyote kabla ya kusaini mkataba awe na smelter hake na serikali sasa ifunge smelter yake twende saawa. Kama hawataki waondoke wakajipange upya. Lets review all mining contracts na hizo ziwe ni moja ya hard conditions
 
Report Ile vitu vingi na source zao nyingi ni kutoka kwa huyohuyo muwekezaji.
Kwa nini tumwamini mwekezaji kwa Kila kitu anachosema?
Sioni kama walifanya kazi waliyotumwa kikamilifu
 
Back
Top Bottom