Mapya yaibuka: BASATA waingilia kati sakata la Miss Tanzania aliyevuliwa taji

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,805
4,487
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limewaita Kamati ya Miss Tanzania pamoja na na Miss Tanzania 2020/21 ambaye amevuliwa taji hilo, Rose Manfere.

Kwa mujibu wa taarifa ya Kaimu Katiba Mtendaji wa Basata, Matiko Mniko, iliyotolewa leo Jumatano Julai 14, 2021 Kamati pamoja na mrembo huyo wanatakiwa kufika kwenye Mamlaka hiyo kesho saa 4:00 asubuhi.

"Tumewaita Kamati ya Miss Tanzania na Miss aliyevuliwa Taji kesho saa 4:00 kisha baada ya hapo tutatoa tamko Rasmi juu ya suala hili," amesema Mniko.

Mtanzania Digital imemtafuta Rose juu ya kuzungumzia suala hilo bila mafanikio baada ya simu yake kuita muda mrefu bila kupokelewa.

PIA SOMA:
- Miss Tanzania avuliwa kuiwakilisha Tanzania kwenye Miss World kutokana na utovu wa Nidhamu
 
Back
Top Bottom