Mapya kuhusu ESCROW, Shule ya Prof Tibaijuka yathibitisha kupokea pesa' in good faith'

Kwa kweli kama pesa hii ilirudi kwa wananchi kwa kusaidi hizi shule mbili za sekondari za wasichana...basi tulegeze moyo kwa mama Tibaijuka, angalau mgao wake ulirudi kwa jamii.
 
Hiyo shule haisomeshi watoto wa kipato cha chini...hiyo ni hadaa tu kwanza ukifika unaambiwa wazi ada ni 4-5mil. Na eanafunzi walio pale ni watoto wa wanene. Unless hiyo ahule ina biashara nyingine chafu. Wenye vipato vya chini huenda pale na wakapigwa chini.
 
Kwa kweli kama pesa hii ilirudi kwa wananchi kwa kusaidi hizi shule mbili za sekondari za wasichana...basi tulegeze moyo kwa mama Tibaijuka, angalau mgao wake ulirudi kwa jamii.

No way, sio kwa kiongozi wa umma. . . . . . .Akakomae na shule sasa ili asaidie kwa karibu zaidi
 
Kusafishana taratibuu. Mfanyakazi wa umma anapokea kiasi kikubwa cha fedha na wengine wengi tu. Halafu unataka kusema hii ni okay?

Only in Tanzania nchi nyingine hawa watu washashtakiwa siku nyingi na wamefungwa.
Jk anasafisha mmoja baada ya mwingine subirini muone.
 
Uzuri wengi hapa JF hawasomi Content ili wachangie kwa hoja.
Mimi nimesoma andiko lao nimegundua kumbe ni kutaka kumsafisha Prof Tibaijuka kwa kutumia tope.

Mambo mawili nilyoona yanawafunga ni haya.

1-Hawakuweka kumb no ya mwaka 2012 iliotumika kuomba msaada.Ni muhimu sana
2-Inawezekanaje fedha zikaingia kwenye account 12/2/2014 na kesho yake 13/2/2014 Bodi ikaitwa ikakaa na siku hiyo fedha zikahamishwa kupelekwa benki M kulipa deni. Kawadangaye watoto.

Hivi mnaangaika na nini? kwani Prof Tibaijuka ndiye waziri pekee aliywahi kujiuzulu hata kama hausiki? shame
 
Kubalini kufa kama mlivyoukubali uhai, kwanini maisha yenu yawatese wenyewe hadi kufikia hatua hii, hiyo essay ni muhimu ingepelekwa kwa vyombo vinavyohusika Mf;CAG, PCCB au kwa PAC but its too late, kwetu sisi mnatuonea tu.
 
Shule haikuwa na akaunti mpaka pesa ilipwe kwenye akaunti binafsi? Akaunti hiyo binafsi ndipo zinapowekwa ada za wanafunzi?
Mnajitekenya na kucheka nyie wenyewe. Shame. Soon mtakaa kimya kama maiti.

ililipwa account binafsi , then ikawekwa account ya shule ikakaa kwa siku mmoja tu kisha yooote ikatolewa kesho yake. tibaijukka asituone watoto
 
Utetezi wa kitoto huu kabisa.
Hela ziingie leo , bodi ikae kesho yake hlf kesho yake hiyo hiyo fedha ziingie kwenye akaunti nyingine na zipotee kabisa tusijue mwisho wake.
Halafu hofu ya nini , wasubiri uchunguzi kama utafanyika.
 
Uzuri wengi hapa JF hawasomi Content ili wachangie kwa hoja.
Mimi nimesoma andiko lao nimegundua kumbe ni kutaka kumsafisha Prof Tibaijuka kwa kutumia tope.

Mambo mawili nilyoona yanawafunga ni haya.

1-Hawakuweka kumb no ya mwaka 2012 iliotumika kuomba msaada.Ni muhimu sana
2-Inawezekanaje fedha zikaingia kwenye account 12/2/2014 na kesho yake 13/2/2014 Bodi ikaitwa ikakaa na siku hiyo fedha zikahamishwa kupelekwa benki M kulipa deni. Kawadangaye watoto.

Hivi mnaangaika na nini? kwani Prof Tibaijuka ndiye waziri pekee aliywahi kujiuzulu hata kama hausiki? shame

Na hii je?

Hawana tabia ya kuwauliza wafadhili vyanzo vya hela zao.Lakini tulihakikishiwa Mkombozi Benki kuwa hela za Bw Rugemalira zimelipiwa kodi tukapokea.... Hii imetoka wapi tena
 
6. Maombi ya Ufadhili: Kwa kuzingatia ushauri huo wa SIDA, mwaka 2012 Bodi ilimtaka Mwanzilishi (ProfesaTibaijuka) ambaye pia ni Mtafuta Fedha (Fund Raiser) wa JOHA TRUST kuwaomba baadhi ya wafanyabiashara mashuhuri nchini kuunga mkono shughuli za asasi yetu kwa michango. Bwana na Bibi James Rugemalira ni miongoni mwa wafanyabiashara walioombwa mchango huo kwa barua ya tarehe 4 Aprili 2012 kupitia kampuni yao ya Mabibo Beer Wines and Spirits Limited. Hatimaye mapema Februari 2014, bila kutaja ni kiasi gani, Bw. Rugemalira alimjulisha Mwanzilishi kwamba yuko tayari kufanya mchango ulioombwa na kumwagiza kwamba sharti ni yeye Mwanzilishi kufungua account hapo Mkombozi Benki kuupokea mchango huo na kuchukua jukumu la kuufikisha shuleni na kuhakikisha unatumika kama ilivyokusudiwa. Bw Rugemalira alieleza hakutaka kuhangaika kuhamisha fedha kwenda benki nyingine ambapo tayari kulikuwa na akaunti za shule.

7. Mchango wa VIP ulivyopokelewa: Kama alivyotakiwa, Mwanzilishi alifungua account hiyo hapo Benki ya Mkombozi tarehe 3 Februari, 2014 na kuupokea mchango huo wa jumla ya bilioni moja, milioni mia sita kumi na saba na lhaki moja (Shs 1,617,100,000/=) kwa niaba ya shule tarehe 12 Februari, 2014 kutoka kwa kampuni ya VIP Engineering and Marketing.

Maswali zaidi, kuliko majibu. Shule iliomba kiasi gani?

Kuhangaika? Mijizi bwana, Mambo siku hizi ni Elektronik yanachukua sekunde tu halafu mnasema kuhangaika, si ana nia njema ya kuisadia shule na shule ina akaunti yake, au?
 
U p u u z i mtupu huo walio uleta!Bosi wao ni Mama Tibaijuka na lzm waseme alicho waambia waseme
 
Uzuri wengi hapa JF hawasomi Content ili wachangie kwa hoja.
Mimi nimesoma andiko lao nimegundua kumbe ni kutaka kumsafisha Prof Tibaijuka kwa kutumia tope.

Mambo mawili nilyoona yanawafunga ni haya.

1-Hawakuweka kumb no ya mwaka 2012 iliotumika kuomba msaada.Ni muhimu sana
2-Inawezekanaje fedha zikaingia kwenye account 12/2/2014 na kesho yake 13/2/2014 Bodi ikaitwa ikakaa na siku hiyo fedha zikahamishwa kupelekwa benki M kulipa deni. Kawadangaye watoto.

Hivi mnaangaika na nini? kwani Prof Tibaijuka ndiye waziri pekee aliywahi kujiuzulu hata kama hausiki? shame

Hata mimi nimeyaona hayo, pia hilo deni la Bank M wangetuwekea slip zake hapa tulione
 
In one of Nyerere/s speech aliwahi kutoa mfano wa mke wa Mfalme aliyetuhumiwa kwa uzinzi,mfalme alifanya uchunguzi na hatimaye akathibitisha kuwa mkewe hakuzini nje ya ndoa,lakini still alimpa talaka na kumueleza kuwa wewe ni mke wa mfalme hupaswi hata kutuhumiwa.
Proffesor pamoja na kutetewa na jopo,bado utetezi wake sio convincing,je hakujua kuwa hela anayopewa imetoka escrow account?je hakujua escrow account ni ya nini?je hakujua kuwa sambamba na yeye kuna viongozi wenzake wenye nyazifa nao walikuwa wanapewa misahada in in good faith kama yeye?je alisahau kwa makusudi au kwa bahati mbaya suala la zawadi vs maadili ya uongozi na utumishi wa umma?je hakujua mtoa zawadi ni muhusika wa escrow yeneye utata?.Bado nina maswali mengi ya kujiuliza na nitaendelea kujiuliza as we go on.
MaSwali ya mwisho,je angekuwa sio waziri hiyo pesa angepewa?Je bodi ina nguvu gani kwenye shule ya Binafsi?je hiyo shule sio ya kwake binafsi au ana ubia na bodi katika umiliki wa shule hiyo?
 
Back
Top Bottom