Mapungufu: Maono sahihi ya wateuliwa ,wapigiwa kura vs dhamira ya maendeleo ya kweli

mwanamichakato

JF-Expert Member
Mar 20, 2015
886
703
Katika nchi yetu pendwa Tanzania wimbi la wengi wanaogombea kuteuliwa ama kupigiwa kura ili kupata uongozi katika ngazi mbalimbali kuanzia Serikari za mitaa, udiwani,ubunge na yamkini Urais,mashirika ya umma, kwa miongo mingi wamekuwa hawana sifa za dhati kuwa viongozi ama kuwa na uwezo sahihi ,maono sahihi ,dira sahihi na maudhui sahihi ya kiuongozi hivyo kupelekea utendaji kazi usio na maono yakinifu,usimamiaji legelege,usimamizi usio thabiti,ufuatiliaji wa kimdebwedo,uwajibishaji wa woga,ukali usio na makucha,uteuzi usiojitosheleza,kutofikia malengo endelevu,misingi mibovu,kupotoka kimaadili,kutokutenda wayanenayo,kutokuwa na huruma dhidi ya wananchi,kuwa mizigo,kuwa kiini cha ufisadi,wizi,ubadhirifu na kiburi cha uongozi usiotukuka.

Lakini pia sifa ya ghiriba,ulaghai,rushwa mchakato kupitia kununua wakereketwa,wapenzi,wanachama, wapiga kura ama viongozi wafanya maamuzi ya upitishaji wagombea vimekuwa vikifanywa waziwazi fedha ikiwa manukato makuu ya kuwavuta wanaopenda na wasiopenda ktk kufanikisha malengo.Mifano ya wengi waliopata ukwasi kwa njia halali na sizizo halali wakifaamika kabla na baada wamediriki kutumia ukwasi husika kununua uongozi na kuupata kisha kuutumia kujineemesha wao,familia zao,marafiki zao,mahawala zao,wana dini wenzao,waliowahi kusoma nao,waliowahi kufadhiliwa nao,waliowapigia debe,waliowaombea kura,waliowasaidia kuchakachua kura n.k.

Mengi yamefanywa lakini kuu limekuwa wingi wa fedha na ukwasi kuwa kigezo kikuu cha sifa za uongozi wa kisiasa kwa ngazi ya vyama na hatimae nje ya vyama.Fulsa za kuteuliwa na kupigiwa kura zimekuwa zikihusisha matumizi makubwa ya fedha,propaganda,vyombo vya habari ktk kuwaaminisha wateuzi na wapiga kura kufanya maamuzi kupitia msingi wa ushawishi,upiga debe,ukereketwa [kindakindaki,bandia,halisi].kuna upotofu mkubwa ktk hili likiendelezwa kuwa mchakato halali wa kupata viongozi wa kuitoa nchi ilipo kwenda inakopaswa.
 
Back
Top Bottom