Mapunda Apindukia Simba -Picha

Amavubi

JF-Expert Member
Dec 9, 2010
30,140
13,215
KIPA namba moja wa Tanzania, Ivo Philip Mapunda, usiku huu amesaini Mkataba wa mwaka mmoja na nusu kujiunga na klabu ya Simba SC ya Dar es Salaam, akitokea Gor Mahia ya Kenya.
Ivo anasaini Simba SC, baada ya kung’ara akiwa na kikosi cha Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars’ katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge mwaka huu.
Kipa Ivo Mapunda akitia dole gumba kwenye fomu za usajili za Simba SC baada ya kusaini usiku huu pembeni ya Katibu wa Simba SC, Wakili Evodius Mtawala kulia
 
3.jpg
 
Ivo anamaliza Mkataba wake Gor Mahia Desemba 16, mwaka huu na ataidakia kwa mara ya mwisho klabu hiyo katika mechi ya Kombe la DSTV Desemba 14 dhidi ya Tusker FC na baada ya hapo atapakia kila kilicho chake na kuja kuanza maisha mapya Msimbazi.
 
Ivo tayari amemwaga wino kuichezea Simba akitokea Gor Mahia ambayo alichangia kuipa ubingwa msimu uliopita ingawa zaidi alikuwa kipa namna mbili.
 
Msimu uliopita: Dharia. Dirisha dogo:Berko. Kadirisha kadogo: Mapunda. Msimu ujao: Buffon?

Halafu ndio walikuwa wanasema eti Yanga wanasajili kuwakomoa Simba,kamati ya Fundi/Usajili Simba ni magarasa tupu angalia walivyochemsha kwenye usajili kwa karibu misimu 4
 
katika vitu ambavyo mapunda amekosea maishani mwake ni kurudi tena kwenye hivi virabu vilivyomtema kuwa kaisha ,na sasa safari yake ya maisha ya soka inaelekea mwisho
 
Halafu ndio walikuwa wanasema eti Yanga wanasajili kuwakomoa Simba,kamati ya Fundi/Usajili Simba ni magarasa tupu angalia walivyochemsha kwenye usajili kwa karibu misimu 4
Wanaweza kuwa sahihi, kwamba wamelazimika kuchemka hivi baada ya kukomolewa na Yanga. Lakini hata ingekuwa hivyo, kupotea ni wakati wa kwenda tu, iweje wapotee hata wakati wa kurudi?
 
katika vitu ambavyo mapunda amekosea maishani mwake ni kurudi tena kwenye hivi virabu vilivyomtema kuwa kaisha ,na sasa safari yake ya maisha ya soka inaelekea mwisho
Hata hivyo umri umeshaenda sana, ni bora aje "kustaafia" nyumbani tu!
 
Nahisi 5-0 zitarudi kipindi hiki cha Berko na Mapunda. Simba watasingizia kuwa hawa makipa ni Yanga damu, kwa kuanzia tunawashona 4-0 kwenye mechi ya 'Nani Mtani Jembe'.
 
Halafu ndio walikuwa wanasema eti Yanga wanasajili kuwakomoa Simba,kamati ya Fundi/Usajili Simba ni magarasa tupu angalia walivyochemsha kwenye usajili kwa karibu misimu 4
Yanga imesajili vizuri miaka minne iliyopita, imepata mafanikio gani Afrika?
 
Nahisi 5-0 zitarudi kipindi hiki cha Berko na Mapunda. Simba watasingizia kuwa hawa makipa ni Yanga damu, kwa kuanzia tunawashona 4-0 kwenye mechi ya 'Nani Mtani Jembe'.

Ndoto za mchana!
 
Yanga imesajili vizuri miaka minne iliyopita, imepata mafanikio gani Afrika?

Ni ukweli usiopingika, Yanga haikufanya vizuri lakini Simba ilikung'utwa vibaya na lile li timu lenye jina baya linaloanza na kumalizia na herufi L....O mtawalia.
 
Back
Top Bottom