SubiriJibu
JF-Expert Member
- Jun 26, 2009
- 1,803
- 1,863
Hatimaye tumetangaziwa kwamba kesho ni siku ya mapumziko na tangazo lenyewe limetolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu.
Lakini Ofisi ya Waziri Mkuu na hata cheo chenyewe cha Uwaziri Mkuu, hakijawahi kuwa mambo ya muungano.
Kulikuwa na Waziri mkuu wa Tanganyika yaani Julius Nyerere mwaka 1961 hadi Feb. 1962 kisha Rashid Kawawa toka Feb. 1962 hadi 1964.
Kule Zanzibar kulikuwa Waziri Mkuu, Mohamed Shamte toka siku ya uhuru December 1963 hadi Jan. 12, 1964.
Baadaye Kawawa akawa Waziri mkuu 1974 na kule Zanzibar mwaka 1984 kukawa na Waziri Kiongozi, Saif Sharrif Hamed.
Hivyo Uwaziri mkuu haujawahi kuwa mambo ya muungano.
Hata Sokoine hakukamata mhujumu uchumi hata mmoja kule Zanzibar.
Hivyo, hili tangazo nina mashaka asilimia nyingi kwamba halina mamlaka Zanzibar. Linaishia kisiwa cha Chumbe.
Zanzibar wanaweza kwenda kivyao. Hata wasipofanya sherehe ni kwa ajili ya utashi wao si kwa nguvu ya tangazo la Ofisi ya Waziri Mkuu.
Jadili, Sahihisha, Elewesha. Usitukane.