Maprofesa wamwinua Rais Magufuli, wanapiga kazi kiukweli

eddy

JF-Expert Member
Dec 26, 2007
15,983
11,399
Kama Magufuli ana watu wa kujisifia basi ni maprofesa walioko katika utawala wake ukweli wanazitendea haki taaluma zao.

Kila nikitizama namwona Profesa Muhongo, Profesa Mbarawa, Profesa Maghembe haya ni majembe ya ukweli na yanapiga kazi sawa sawa.

Hongereni sana. Ila kuna jamaa yangu Kitwanga hana shahada mbili ila nae ana vimikwara fulani hivi.
 
Magembe hamna kitu

Maghembe ni jembe ila awamu iliyopita ilikuwa haina dira. Hiyo wizara ya mali asili na utalii nayo ni pasua kichwa. Ina maslahi binafsi, wizi na rushwa kubwa kwenye kila idara. Misitu kuna mbao, Magogo na Mkaa. Utalii kuna wizi wa tour operators kuficha fedha za kigeni kwenye akaunti zao nje ya nchi, wizi na Ubadhirifu Tanapa,mamlaka ya ngorongoro, uwindaji wa kitalii uliogeuka ujangili nk. Mbaya zaidi wahalifu ni vigogo wa ndani na nje ya nchi yetu. Wafanyakazi wa wizara na viongozi wengine wa serikali wakiwemo wabunge wana mkono katika kukwamisha juhudi zake.
 
Wanapigia wapi kazi,?? Maana huku kwetu Mwanjelwa sukari bado 2500,cement 16000,rushwa za elfu tano tano kibao,hapa rufaa dawa hakuna na zilizopo zinauzwa bei kama dhahabu,HIYO KAZI WANAPIGIA CHUMBANI???!
 
eti uu nao ni uzi...hata JK alikuwa Profesa lakin ndio katugharimu kiasi chote hiki
 
Wanapigia wapi kazi,?? Maana huku kwetu Mwanjelwa sukari bado 2500,cement 16000,rushwa za elfu tano tano kibao,hapa rufaa dawa hakuna na zilizopo zinauzwa bei kama dhahabu,HIYO KAZI WANAPIGIA CHUMBANI???!
hiyo ni kazi ya yule nshomile mkuu kazi ilishamshinda tunasubiri kupiga chini tu.
 
Back
Top Bottom