- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Tangu nikiwa mdogo nilisikia na kuamini kwamba ute/ mapovu yanayokuwa kwenye mimea ni mate ya nyoka. Mpaka kufika wakati huu bado sijajua kama suala hili lina ukweli ama la.
Naomba wataalamu mnisaidie kujua uhalisia wa jambo hili
Kielelezo 1: Picha ikionesha mmea umeachiwa mapovu
Kielelezo 2: Picha ikionesha mdudu aina ya Spittlebugs anayetengeneza Povu kwenye mimea
Video ikionesha namna wadudu aina ya Spittlebugs wanavyotengeneza povu
Naomba wataalamu mnisaidie kujua uhalisia wa jambo hili
Kielelezo 1: Picha ikionesha mmea umeachiwa mapovu
Kielelezo 2: Picha ikionesha mdudu aina ya Spittlebugs anayetengeneza Povu kwenye mimea
Video ikionesha namna wadudu aina ya Spittlebugs wanavyotengeneza povu
- Tunachokijua
- Imekuwa ni imani ya wengi katika jamii mbalimbali wakihusisha mapovu yanayopatikana kwenye mashina na matawi mengi ya miti iliyo porini au vichakani na mate ya nyoka. Watu wengi wenye imani hii wamekuwa wakichukua tahadhari kubwa wakiamini kwamba ukiona mmea una mapovu hayo ni ishara kwamba nyoka wapo maeneo ya karibu.
Je, mapovu yanayokuwa kwenye mimea mbalimbali porni au vichakani ni mate ya nyoka?
Jamiiforums imefuatilia katika makala na tafiti za kisayansi kubaini ukweli wa jambo hili ambapo tumebaini yafuatayo
Texas Naturalist wataalamu wa Mazingira na Chuo Kikuu cha Florida nchini Marekani wamefanya utafiti na kubaini kuwa mapovu hayo yanayokuwa kwenye mimea hayahusiani na nyoka isipokuwa ni mapovu yanayozalishwa na wadudu waitwao spittlebugs ambao wanatoka kwenye familia ya Aphrophoridae na superfamily Cercopoidea.
Wataalamu wanaeleza kuwa Wadudu hawa hutembea kwenye mimea na huzalisha mapovu kama mbinu yao ya kujilinda wasishambuliwe na wanyama wengine wakati wananyonya utomvu wa mmea husika.
The New York Times wanaeleza kuwa Povu la spittlebugs hutokana na kuchanganya hewa na maji iliyopo tumboni mwao hivyo kulitoa povu hilo kama mkojo. Inaelezwa kuwa Wadudu aina ya spittlebugs wapo zaidi ya makundi (species) takriban 930 katika nususpishi 160 duniani.
Je povu hili ni sumu au hatari?
Wataalamu wa masuala ya mimea RHS wanaeleza kuwa Povu lenyewe halina hatari kwa asili yake na haliwezi kumuathiri binadamu, lakini wadudu aina ya spittlebugs wanaweza kubeba na kusambaza bakteria ya aina ya Xylella fastidiosa, ambayo husababisha magonjwa hatari ya mimea.
RHS wanaeleza kuwa bakteria hawa hula Mirija/njia inayotumiwa kusafirisha maji kutoka kwenye mizizi ya mmea kwenda kwenye sehemu za shina, matawi na majani ambayo hupelekea majani kuwa kama yamechomwa moto, kuoza, kupukutika au mmea mzima kufa.
Naye, Mkufunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori Mweka, Tito Lanoy anaeleza
Kwanza hayo siyo mate ya nyoka, mate ya nyoka ni yellowish au colorless kwa wale nyoka aina ya swira wanao tema mate. Mate ya nyoka hukauka punde tu yanapoa tua mahauli yalipo lenga unless kuwe na majimaji.
Hayo mapovu kwenye miti mara nyingi huwa ni ya wadudu wanao julikana kama Cicadas, wapo wa jamii nyingi. Pia kuna baadhi ya vyura nao hutengeneza povu kwa ajili ya kuhifadhi mayai yao yasiharibiwe na jua
Kwa hilo povu la cicadas hudondoka kama matone madogo madogo tofauti na yale ya chura, pia cicadas hutoa mlio au sauti kali sana tofauti na vyura.
Hayo matone yakikudondokea au yakimdondokea mnyama yeyote hayana madhara yeyote, ni imani tu za makabila mbalimbali kuwa yana madhara ila hakuna ukweli wowote
Hivyo, kutokana na ufafanuzi huo JamiiForums inaona hoja inayoeleza kuwa mapovu hayo ya kwenye mimea ni mate ya nyoka si ya kweli.