Mapovu toka CCM; waandishi wamenangwa na Tundu, tusubiri tamko | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mapovu toka CCM; waandishi wamenangwa na Tundu, tusubiri tamko

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kiganyi, Sep 9, 2012.

 1. Kiganyi

  Kiganyi JF-Expert Member

  #1
  Sep 9, 2012
  Joined: Apr 30, 2012
  Messages: 1,244
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Culled from Daily Nkoromo Blog

  TAALUMA ya uandishi wa habari nchini kila kukicha imeendelea kudharauliwa na wanasiasa na baadhi ya viongozi ambao wanajiona taaluma zao ndio bora na zenye uwezo wa kuhoji na kuakisi mambo.

  Mfumo huo umeendelea kuota mizizi huku hata zile klabu, majukwaa na mabaraza ya uandishi wa habari yakiwa kimya na badala yake kuzungumzia mambo mengine ambayo hayana faida kwa mwandishi wa habari.

  Uandishi wa habari Tanzania unakumbukana na changamoto lukuki ambazo zilipaswa kuwa sehemu ya mjadala kwa vyama vilivyopewa dhamana ya kuwaongoza waandishi wa habari ambao maisha na mfumo wa kazi zao umekuwa kama mchezo wa bahati nasibu.

  Kitendo ambacho kinafanya thamani na hadhi ya mwandishi kila kukicha kupotea huku majina ya dharau nayo yakizidi mara 'watu wamshiko', 'makanjanja' au 'vihiyo'. Yote haya yanasababishwa na ubinafsi na ukasuku wa kukariri matamko.

  Kauli ya kashfa na Mbunge Tundu Lissu (Singida Mashariki - CHADEMA) kuhusiana na wajumbe wa tume walioteuliwa na serikali kuhusiana na kifo cha Mwandishi wa habari Daud Mwangosi kuwa baadhi yao hawana uwezo ni fedheha kubwa kwa wajumbe hao na tasnia nzima.

  Mbunge huyo aliitisha mkutano na waandishi wa habari kuelezea msimamo wa chama chake kutokuwa na imani na tume hiyo hasa kutokana na kuwa na wajumbe baadhi aliodai wasiokuwa na ueledi wa mambo wanaochunguza.

  Katika mkutano huo, Lissu alizungumza mambo mengi juu ya tume hiyo, lengo likiwa kuaminisha umma kuwa tume hiyo haifai na ndiyo maana chama chao wanaikataa huku akitaja majina ya wajumbe wa tume hiyo ambayo kimtazamo wake yeye anasema hawana uwezo.

  Hata hivyo, muktadha wa hoja hii hautakuwa kuzungumzia uwezo wa kila mjumbe ndani ya tume hiyo, bali ni udhaifu wa vyama vyetu ambavyo navyo vinapotezwa katika mlengo wa kusimamia maslahi ya waandishi na kuanza kuwa watoa sauti ya wanasiasa kushindana kuikataa tume.

  Kuchaguliwa kwa Mwenyekiti wa tume hiyo Jaji mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Stephen Ihema na wajumbe wengine wakiwemo mahiri katika tasnia ya habari kama Theopil Makunga (Jukwaa la Wahariri) na Pili Mtambalike (Baraza la Habari Tanzania) ilikuwa ni sehemu ya waandishi na klabu za habari kufurahia na kuipongeza serikali.

  Kufurahia huko kunatokana na kifo cha Mwangosi ambaye ni mwenzetu kuwa kinachunguzwa na waandishi wenyewe, hivyo kutolewa kwa kauli za dharau kuwa waandishi wa habari hawawezi kuchunguza kifo ni tusi kubwa ambalo lilipaswa kukemewa na si kuachwa kama inavyotaka kufanywa.

  Nakumbuka katika jali ya MV Bukoba, mmoja wa wana habari mahiri nchini Jenerali Ulimwengu alikuwa mjumbe wa tume iliyochunguza chanzo cha ajali hiyo. Mbona mambo yalikwenda sawa au kwa kuwa Lissu alikuwa hajapata umaarufu?

  Japokuwa katika suala zima kuhusiana na tukio hilo waandishi walitofautiana kimtazamo na kifikra, lakini linapokuja suala la kudharauliwa, tunapaswa kuwa pamoja na kukemea. Kinyume chake baada ya kunang'wa na Lissu tunatakuja kupewa tusi kubwa zaidi.

  Mwenye uwezo na ueledi wa kuchunguza kifo si mwanasheria pekee? Lisu anapaswa kutambua hilo na kuachana na mawazo ya Mfalme Jua, juu ya kile anachokiamini kuwa ni sahihi na hapaswi kupingwa au kukatazwa na mtu.

  Jamii inaelimishwa na kufundishwa kupitia mifumo tofauti ya maisha na ndiyo maana wanasaikolojia wanaamini tabia ya mtu ni rahisi kuifahamu kupitia matamshi na matendo yake kuwa ni makuzi gani aliyapata utotoni.

  Sitaki niamini kuwa klabu, jukwaa na hata baraza lenyewe halijasikia maneno ya kejeli ya Lissu, bali naamini yapo makundi ndani ya waandishi wa habari likiwemo la wale walio tayari kwa lolote ili mradi wawanufaishe wengine na hasa wanasiasa au watwana wao.

  Hilo litapongezwa kwa matamko au hata kwa kujitokeza na kusukuma magari yao kuwa hawa kwa mtazamo wao kuwa hao ni mashujaa na wazalendo wa nchi hii .

  Hivyo, ningetamani nguvu iliyotumika kutoa tamko la kuwataka polisi wakae meza moja na CHADEMA kumaliza tatizo, ingetumika kutoa tamko juu ya dharau ya Lissu na chama chake kwa waandishi wa habari nchini.
   
 2. m

  majebere JF-Expert Member

  #2
  Sep 9, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 4,520
  Likes Received: 567
  Trophy Points: 280
  Mimi mpaka sasa sijaelewa kitu kimoja, kwanini ni CDM ndio wameshupalia hiyo tume na sio familia ya mfiwa. Afadhali hata waandishi wa habari wangeshupalia tungeelewa.
   
 3. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #3
  Sep 9, 2012
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Ukimsoma Mwandishi, unakubaliana naye kuwa hawa jamaa baadhi yao ni ma KANJANJA.

  Mwenyewe unasema kuwa Kauli ya Lisu (kwenye blue) na kwenye RED unasema ulikuwa msimamo wa chama. Sasa hapa nini kilisemwa? Maneno ya Lisu au ya Chadema?

  Mwisho ingelikuwa HAKI kutuwekea kwa nini yeye ameona baadhi hawafai. Kuna wengine walimkalia kooni juu ya Majaji Vihiyo na alipokuja kuweka report, wakazima vyombo vyao vya KULIA....
   
 4. F

  FJM JF-Expert Member

  #4
  Sep 9, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Tatizo sio tume, ila nani mwenye mamlaka ya kuunda tume ya kuchunguza kifo cha raia kama katiba inavyoeleza.

  Mwandishi wa hii article anaoenakana kutoelewa kabisa nini alichokuwa anazungumza Lissu. Na mbaya zaidi hata mwenyekiti wa tume (or kamati) ya Nchimbi ni jaji lakini badala ya kumshauri waziri kuhusu taratibu za uchunguzi wa vifo vyenye utata, yeye (jaji) kaenda kichwa kichwa!

  Yote tisa, kama CCM wanathamini waandishi wa habari kwa nini wanawauwa? Mwandishi wa makala hii asome ushuhuda wa mwandishi wa habari mwenzake kwenye gazeti la Tanzania Daima 9/9/2012, halafu aseme ni kwanini RPC wa Iringa bado yuko kazini hadi sasa?

  Mwisho, mwandishi wa hii makala anaweza kusema mwana-blog na mwandishi mwenziwe Godwin yuko wapi? Na kwa nii yuko huko aliko kama kweli CCM inathamini waandishi wa habari?
   
 5. morenja

  morenja JF-Expert Member

  #5
  Sep 9, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 3,525
  Likes Received: 1,051
  Trophy Points: 280
  duu umeshafika huku ??.napita tuu
   
 6. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #6
  Sep 9, 2012
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo wewe ni Mwandishi wa habari au ndugu? Mbona una washwa washwa pia?

  Kama CDM wanashupalia, ni kwa sababu alifia kwenye vikao vyao,infact kwenye SHINA la Chadema. Sasa wewe mtu akafia kwako, unabaki kusema "mie siyo mwandishi wa habari" na wala siyo NDUGU na kwa hiyo hili halinihusu.

  Kichwa kitumike zaidi ya kuotesha nywele jamani.
   
 7. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #7
  Sep 9, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Na kamwe hutaelewa!
   
 8. a

  andrews JF-Expert Member

  #8
  Sep 9, 2012
  Joined: Mar 28, 2012
  Messages: 1,680
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  mbwa koko kaa kimya unatapika go back to school umesoma na hujaelimika
   
 9. Foum Jnr

  Foum Jnr JF-Expert Member

  #9
  Sep 9, 2012
  Joined: Jul 27, 2012
  Messages: 272
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Ikiwa Tume itaundwa na Waziri (Kamati as it was suggested) au itaundwa na Rais basi credibility ya Tume ni wajumbe wenyewe na hitimisho lake. Sioni logioc ya Tume kuwa na ulazima wa kuundwa na Rais ambaye (kama alivyo waziri) wote ndio walalamikiwa kwa upande mmoja u mwengine, ikiwa findings za Tume zitatakiwa kufichwa kutokana na upendeleo basi nafasi ya Rais au Waziri zote ni sawa ie same party, same gov etc Kama kuna malalamiko katika uundwaji wa tume basi reforms zifanyike ili kuweka transparency ya Tume iweze kuwa na ufanisi na credibility ya utendaji, ila kwa sasa katika kutafakari reforms tuangalie ni nani atakaebeba jukumu la kuunda tume ilio na uhuru mkuu? Suggestion ni kuwe na kamati itakayoundwa na bunge, ikijumuishe wajumbe kutoka taasisi zinazokubalika za mchanganyiko pamoja na vyama tafauti.
   
 10. Laurence

  Laurence JF-Expert Member

  #10
  Sep 9, 2012
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 3,106
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Kaa kimya wewe bata hapa sio sehemu yako nenda kwa watoto wenzio huko facebook
   
 11. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #11
  Sep 9, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,700
  Likes Received: 12,750
  Trophy Points: 280
  Bado mnataka mcheze music ya lissu mtauweza!
   
 12. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #12
  Sep 9, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  CDM wana haki kushupaliwa kwani majibu yake yanwahusu tena sana.Tena zaidi ya waandishi wengi sana wa habari.General Ulimwengu ni wa calibre ingine.Sio hawa makanjanja ambo tayari kuna fununu kuwa wanataka tolea njaa hapa kwa kudownplay tukio zima.
   
 13. S

  SHEMGUNGA JF-Expert Member

  #13
  Sep 9, 2012
  Joined: Jan 13, 2012
  Messages: 653
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  mwandish umelopoka nenda kajifunze unaonekana uko kisccm!
   
 14. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #14
  Sep 9, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,223
  Trophy Points: 280
  mwandishi/mwenye blogu nae analwta majungu tu.....

  Angetuwekea sababu alizozitoa lissu, sio kuzizungusha na kuzielezea kwa mtazamo wake..... Halafu angeelezea wasifu wa hao 'wanatume ' na kutetea hoja yake(pale ambapo lissu amewadharau)
   
 15. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #15
  Sep 9, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  CDM wana haki kushupaliwa kwani majibu yake yanwahusu tena sana.Tena zaidi ya waandishi wengi sana wa habari.General Ulimwengu ni wa calibre ingine.Sio hawa makanjanja ambo tayari kuna fununu kuwa wanataka tolea njaa hapa kwa kudownplay tukio zima.
   
 16. tanga kwetu

  tanga kwetu JF-Expert Member

  #16
  Sep 9, 2012
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 2,165
  Likes Received: 1,124
  Trophy Points: 280
  ukiamua kujifyatua akili hakuna wa kukusaidia, Kiganyi. Lissu hakatai au hapingi waandishi wa habari kuwemo kwenye tume ila hao waliomo hawa-fit kutokana na kile kinachochunguzwa.
   
 17. 50thebe

  50thebe JF-Expert Member

  #17
  Sep 9, 2012
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 1,885
  Likes Received: 266
  Trophy Points: 180
  mtoa hoja hajui alichoandika wala hajui anachosimamia. Mashuhuda wa tukio la kuuwawa kwa Mwangosi wanatosha hivyo hii tume/kamati ni danganya toto tu.
   
 18. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #18
  Sep 9, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  Japo KIGANYI umerefer but huwa wewe hoja zako ni uchochezi afu unajiita mwana cdm...shame on u
   
 19. kibogo

  kibogo JF-Expert Member

  #19
  Sep 9, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 9,477
  Likes Received: 784
  Trophy Points: 280
  Huyu jamaa anakurupuka waziri amesema ameunda kamati yeye anakuja na hoja ya tume, hakuna tume iliyoundwa mpaka sasa ndugu,tunaisubiri iundwe na mkuu wa nchi.
   
 20. Kiganyi

  Kiganyi JF-Expert Member

  #20
  Sep 9, 2012
  Joined: Apr 30, 2012
  Messages: 1,244
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mkuu huwa unakosea sana kuni label hivo lakini sikulaumu!

  Mimi nimeshangaa mwandishi ambaye haelewi Lissu alikuwa anasimamia Sheria ya kuunda tume na he just came out loud kwamba jamaa kawadhalilisha wanahabari!

  Nadhani nakusaidia kuwatambua waandishi wanaopaswa kupuuzwa lakini kumbe inakukera! Na ndio maana nimeonesha kuwa hiyo habari nimeichagua toka wapi!

  N vizuri kuelewa na kuziona pumba na Mchele wakati huu kuliko kungoja hadi pale watu watapoanza kupotoshwa moja kwa moja!

  Sorry Mkuu! Ila mimi ni Mwanachadema na najivunia katika hilo!
   
Loading...