Benson Mramba
JF-Expert Member
- Oct 29, 2013
- 644
- 1,482
Nimekuwa nikikwazika sana kumsikia Mama akiongea as if hakuwa makamu wa Rais wa Dkt. Magufuli. Wakati mwingine nimekuwa naona kama anasaliti uongozi mzuri wa Hayati Magufuli.
Jana wakati akipokea ndege ya mizigo ya ATCL Mama aliongea kama kiongozi aliyeshiriki katika harakati za Awamu ya tano. Pamoja na ripoti mbaya ya CAG Kichere (mtazamo wangu) ambayo niliona ina malengo ya kupotosha harakati za Dr Magufuli kwa ATCL lakini Mama jana alijibebesha uhusika wa mambo yote ya ATCL nilipenda sana.
Maoni yangu: Ili Mama afanikiwe katika Awamu yake hii ya sita hapaswi kujitenga na Dr Magufuli hata kidogo KIMSIMAMO WALA KIMTAZAMO.