Mapokezi ya Maalim Seif Zanzibar, Mwili wangu umekufa ganzi

demigod

JF-Expert Member
Jan 2, 2015
8,250
15,116
Wakuu hongereni na majukumu ya kila siku.

Najua mlio wengi hamjapata nafasi ya kuwa pahala nilipo. Ninaiita nafasi kwa kuwa ninachokishuhudia hapa LIVE kimeniletea hisia za kimwili, kiakili na kisaikolojia ambazo huwezi kuzipata kwa namna yeyote ile hata kwa kutazama pichani huko kwenye mitandao kile kinachoendelea hapa nilipo.

Acha nieleze hisia ambazo nimekumbana nazo kimwili hapa nilipo ambapo mapokezi wa mgombea wa Urais kupitia chama "kikuu cha upinzani kwa hapa Zanzibar" yanafanyika.

Ingawa nimekuja kwa shughuli binafsi, ujio wa Maalim Seif umeweka doa moyoni mwangu. Idadi ya watu waliojitokeza kumlaki umechoma simanzi ya huruma niliyonayo kwa wazanzibar ambao wamekuwa wakinyonywa na serikali iliyopo madarakani.

Moyo wangu umepigwa na mshtuko baada ya kushuhudia baadhi ya wakina mama wakiwa wanatokwa machozi kwa namna ambayo ililowesha mazima nafsi yangu. Machozi ya matumaini ya ukombozi ambayo yanayotarajiwa kutoka kwa maalim seif yenye kuashiria kuwa vizazi vyao huenda vikaishi kama binadamu hapo baadaye.

Simanzi ilijaa usoni pangu baada ya kuwaona vijana wazanzibari wa kila rika wakisimama barabarani ili wapatepo nafasi ya kumlaki mtu aliye shika na kuhodhi matumaini ya maisha yao. Ukizitazama sura zao zinaashiria kukata tamaa kabisa na umasikini, shida, manyanyaso, uonevu na ukatili uliokuwa ukihudumiwa kwa wazanzibar na serikali iliyopo madarakani.

Huruma ilinijaa mapajani mwangu baada ya kuona wananchi wa zanzibar wakifunga maduka yao, hata wakiwa tayari kukosa kipato chao kamili cha siku ili waweze kuosha macho yao kwa kumtazama mwanakondoo aliyeshushwa kwa ajili yao.

Kinywa changu kilijaa Jazba isiyo na maandishi baada ya kushuhudia baadhi ya wahuni wa uvccm wakishusha bendera za chama cha mwanakondoo huyo pasi na kukemewa na askari waliokuwa wakitazama tu bila kuchukua hatua yeyote ile.

Sononeko la moyoni mwangi likisindikizwa na hali duni ya wazanzibar ilinifanya nibadilishe ratiba yangu mapema ya kurudi Bara kwa maana kila kijiwe cha hapa nilipo yanajadiriwa maovu yaliyofanywa kwa wazanzibar.

Siko tayari kuendelea kufa ganzi kwa namna hii, nilipanga kukaa zenji mpaka Alhamisi lakini ninaogopa kufanya jambo baya ili kuwafuta machozi wazanzibar. Kutokana na uwananchi wangu wa ukawaida, nimeona ni vyema kukimbia mapema.

Bila Shaka Ninatumaini Wazanzibar Wataishi Katika Zanzibar ya Ndoto Yao.

.
EZQq3w9WsAEhnix.jpg
 
Uchagizi uwe huru na wa haki ili kama CCM wanaona wananchi wanakosea kuchagua upinzani,basi lawama zije kwa wanachi,kuliko kutangaza isivyo ikitokea Upinzani umeshinda.
 
Uchagizi uwe huru na wa haki ili kama CCM wanaona wananchi wanakosea kuchagua upinzani,basi lawama zije kwa wanachi,kuliko kutangaza isivyo ikitokea Upinzani umeshinda.
Sawa kwa hakika Maalim atashinda. Lakini Jecha yupo!
 
Anayewachagulia rais ni ccm bars, hayo mengine wanapoteza muda tu.

Pia; kwa wanautaka Urais wakubali kumwaga damu kama kipindi cha kumtoa mkoloni
 
Sisi tulipiga mkwara na kuweka daftari kwa watumishi wa umma waje kumpokea mgombea wetu
 
Back
Top Bottom