Mapokezi ya Freeman Mbowe yatikisa Musoma Mjini

Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe amekiri kuwa kushindwa kwa Chadema kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 kulitokana na kuweka wagombea dhaifu kwenye nafasi mbalimbali ikiwemo uraisi na hivyo wamejifunza na uchaguzi ujao wataweka wagombea wenye nguvu na ushawishi watakaozunguka nchi nzima kunadi sera na ajenda za wanachi.

Mbowe amesema Chadema haijawahi kuishiwa ajenda za kupambana na ccm.


My take.

Watakiri yote waliyomsingizia mwendazake laana ya kumtukana imeanza kuwatafuna.

Kumbe waliweka wagombea dhaifu alafu wakasingizia wameibiwa kura na mwendazake. Hovyo kabisa.

Umeogeza chumvi, Katika hiyo nukuu uliyoweka kutoka gazeti la Mwananchi Mbowe hakutaja nafasi ya uraisi, nanukuu
"Mwanza. Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe amekiri kuwa walikuwa na baadhi ya wagombea ambao hawakuwa wakikubalika kwenye maeneo waliyogombea nafasi mbalimbali ikiwemo ubunge na madiwani katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020."
 
Back
Top Bottom