Tetesi: Mapokezi makubwa yamsubiri January Makamba jimboni mwake Bumbuli

Tunakoelekea watatajana mabaya yao yote...hata hizo kura za urais 2015 kuna watu wanajua mchezo mzima ulivyofanyika hopefully.

Kumpata mtu msafi ndani ya CCM ni kazi kubwa; ni bora upewe kazi ya kutenganisha punje za sukari na mchanga toka kwenye gunia la kilo 100.
exactly
 
Hivi anashindwa nini kuiga "busara" za wenzake waliokuwa mawaziri na kisha kutumbuliwa na kukaa zao kimya?....akikubali huu ushauri wa "kuandaliwa" mapokezi basi lazima awe na plani moja kati ya hizi....(i) Kuhamia upinzani au (ii) kuachana kabisa na siasa za awamu hii nakwenda zake "masomoni"
Ila nakumbuka hata Mwigulu Nchemba wanyiramba waliandaa mapokezi manene, mazito, marefu, makubwa
 
Mngekuwa na akili,mngejiuliza ni kwanini kila uchaguzi kura za wagombea uraisi wa CCM zinashuka sambamba na idadi ya wabunge wa CCM huku upinzani ukijiongezea kura za wagombea wake wa uraisi na kuongeza idadi ya wabunge wake.

Kwa sasa chama chenu kina-survive kwa msaada wa dola tu kwani kimeshapoteza political legitimacy kwa kiwango kikubwa kuliko Mlima Kilimanjaro!!

Endelee na kiburi chenu na ulevi wenu wa madaraka na ndio maana awamu hii imekuwa ni mateso karibu kwa kila kundi katika jamii kuanzia watumishi wa umma,wafanyabiashara,wavuvi,wanasiasa mpaka na wawekezaji kutoka nje ya nchi!!

Tegemeni majeshi yalinde masilahi ya CCM kama alivyosema mwenyekiti wenu tena hadharani!!!
that is the way its..
 
Imearifiwa wakati Mbunge wa Bumbuli Mheshimiwa January Makamba akitarajiwa kuwasili jimboni humo mwanzoni mwa mwezi ujao, wapiga kura wake wanajiandaa kumpa mapokezi ya kishindo.

Tuombe sana jeshi la polisi wasiwekee figisu zoezi hili kwani ni haki ya wana Bumbuli kupokea mwakilishi wao na kumtia nguvu.

Mapokezi hayo yatafuatiliwa na ziara ya kukagua miradi ya maendeleo jimboni Bumbuli.
Makamba simuelewagi Kabisa yuko upande wa siasa za aina gani?.
Kwanza kisiasa yupo hoi
 
kuwa na panaldol karibu ili maumivu ya kichwa yakizidi ya kufikiri kilichowezekana unywe
Yaani mbunge wa CCM kupokelewa kwao yeye apate maumivu ya kichwa?
Pambaneni na hali zenu zilizogubikwa na usanii, visasi na uongo
 
kwani magufuli alichaguliwa kihalali? yule wa zanzibar alivhaguliwa kihalli? nyumba ni sifa ya mtu kuwa mbunge? wabunge wangapi hawakai kwenye majimbo yao?
Mimi nimesema alichaguliwa kihalali? Ipo siku na haiko mbali watatuambia walichofanya kule Masaki. Naichukia CCM kama ninavyomchukia sheitwan.
 
Kura zipi mkuu? Mbona kila uchaguzi Chadema wanaingia gizani?

Weweendelea tu kuficha kichwa mgongo ukiwa wazi. Huo ndio uhalisia bila dola mshindi huwa anajulikana. Naujue hii haiwezi kuwa milele kuna mifano mingi ya tawala kuporomoka ikiwa na dola.
 
Sijui Mshauri wa January Makamba ni nani lakini mambo mawili ni hakika
1. Hamshauri vyema ama January hashauriki
2. Wote wawili mshauri na mshauriwa hawajaweza kusoma alama za nyakati.

January Makamba amefika alipofika kwa sababu ya baba yake na mkono wa Jakaya, ni muda Sasa wa yeye kusimama yeye mwenyewe.
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom