Mapokezi makubwa yamsubiri Kikwete Comoro

Mtu wa Pwani

JF-Expert Member
Dec 26, 2006
4,184
671
Mapokezi makubwa yamsubiri Kikwete Comoro na manyerere jackton, anjouan, comoro

SERIKALI na wananchi wa Comoro, hasa Kisiwa cha Anjouan, wamemwandalia Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU), Rais Jakaya Kikwete, mapokezi makubwa.

Habari zilizopatikana kutoka ndani ya Serikali ya Mpito ya Kisiwa cha Anjouan, zilisema Rais Kikwete, anatarajiwa kuwasili hapa siku yoyote mwezi huu.

Rais wa Muungano wa Visiwa vya Comoro, Ahmed Sambi, anatarajiwa kuwasili hapa leo, tayari kumlaki mgeni wake, Rais Kikwete.

Kanali Bacar, na wafuasi wake wasiozidi 10, walikimbia kwenda mafichoni baada ya kuzidiwa nguvu na majeshi ya Umoja wa Afrika (AU).

Serikali imesema Rais Kikwete anakuja Anjouan akiwa Mwenyekiti wa AU, chombo kilichoidhinisha matumizi ya nguvu dhidi ya Kanali Bacar.

Uwanja maalumu umeandaliwa kwa ajili ya mapokezi hayo. Maeneo kadhaa yamepambwa mabango ya kuipongeza Tanzania.

MTANZANIA jana ilishuhudia baadhi ya ofisi za umma, zikiwa zinatundika katika kuta, picha ya Rais Sambi, ambayo awali iliamuriwa na Kanali Bacar, isionekane mahali popote.

Wakati hayo yakiendelea, hali ya utulivu imeendelea kuwapo mitaani, ingawa kuna milio michache ya risasi katika maeneo ya milimani. Jeshi la AU, limedhibiti hali ya usalama. Shughuli zimerejea katika hali ya kawaida.

Hadi juzi, mateka 250 walikuwa wamejisalimisha na shehena kubwa ya silaha. Wengine waliojificha, wameanza kujisalimisha. Mitaa inakuwa na watu nyakati zote, kitu ambacho wenyeji wanasema hakikuwapo wakati wa utawala wa Kanali Bacar.

Hata hivyo, hali ya maisha ni ngumu, kwani bei za vitu zimepanda maradufu, hasa mafuta ya petroli

mtanzania
 
Lord lo** anakwenda huko kwa bajeti na kodi ya nani?
 
Ningependa kumpa Hongera Mwenyekiti wa AU Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kwa maendeleo yanayotokea Comoro !
 
Tupeleke walimu wa kiswahili Comoro. Wakati nchi zikiwa katika uhusiano mzuri, ndiyo wakati wa kubadilishana utamaduni, biashara, elimu nk. Inapendeza inapotokea nasi tunategemewa, siyo kutegemea wengine siku zote.
 
Ningependa kumpa Hongera Mwenyekiti wa AU Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kwa maendeleo yanayotokea Comoro !

nilijua utatoa hongera tu hapa jf kumbuka hapendwi mtu watu tuna machungu na muelekeo wa nchi yetu!!
 
Tupeleke walimu wa kiswahili Comoro. Wakati nchi zikiwa katika uhusiano mzuri, ndiyo wakati wa kubadilishana utamaduni, biashara, elimu nk. Inapendeza inapotokea nasi tunategemewa, siyo kutegemea wengine siku zote.

Imekaa vizuri hii
 
Hili ni wazo zuri. Lakini sijui kama 'Sirikali' yetu tukufu itakubaliana nalo. Maana wanatakiwa wawashawishi wa-comoro kwanza.
 
Tupeleke walimu wa kiswahili Comoro. Wakati nchi zikiwa katika uhusiano mzuri, ndiyo wakati wa kubadilishana utamaduni, biashara, elimu nk. Inapendeza inapotokea nasi tunategemewa, siyo kutegemea wengine siku zote.

ARE U SERIOUS??? KIJIJINI KWENU HAO WALIMU WAPO WANGAPI?? KILA KUKICHA USIKII WAKILALAMIKA MISHAHARA NDO UNATOA MAWAZO KUPELEKA WALIMU COMORO?? ona mbali aloo sio kulopoka tuu...
 
Kuna baadhi ya nafasi za kiutendaji mtu ukiwa nazo lazima kwa kiasi fulani iendane na hadhi yako sasa kuuliza eti Kikwete anakwete kwa kodi ya nani ilhali ukijua ni mkiti wa AU, ni rais wa Inchi tuulize maswali yenye mantiki, Once ur the Prsd ur there 4 it!
 
Endeleeni kumponda anaetoa wazo la kupeleka walimu Comoro wakati wakenya na warundi wanajaa huko wakilipwa hela nzuri na kiswali chao kibovu,
 
Vijana wetu ni mashujaa huko Comoro, hii ndiyo JWTZ!

comoro070408.jpg

4024.jpg
 
Mwenyekiti wa AU nakuomba sana tena sana safari inayokuja iwe ni Darfur...kabisa na kwa moyo mmoja tukapambane ili kama kweli tuna nia ya ukombozi wa walio wengi na haki basi tukawatoe wadhalimu waliopo Darfur...hapo mimi nitakuwa radhi na sifa zoote kwa mwenyekiti nitakupa.......somalia achana nako kwanza maana historia kule ni ngumu kidogo...ila nako ikibidi na muda ukienda sana tutaleta hoja kuwahamisha wasomali woote tuwatawanye dunia nzima pale pajengwe makao makuu UN,AU<UN ORG HQ>...kanda ya AFRICA kusini jangwa sahara.tumalize uhasama wa kooo hizoo...
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom