Mapokezi chanjo ya Corona: Ni wakati sasa kutazama utendaji wa Waziri wa Afya

Shujaa Mwendazake

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
3,735
6,291
Nimeliona Bango la mapokezi ya chanjo ya Corona uwanja wa ndege wa J.K Nyerere. Kwanza nilicheka sana baadaye nilipoanza kufikiria juhudi za kupambana na Ugonjwa huu tangu wakati wa mashine za kupigia nyungu na zilivyozinduliwa kwa Mbwewe.

Sasa najiuliza hii chanjo imeshaanza kutumika hapa Tanzania, Huyu Mama anapokea kitu gani tena kama Uzinduzi?

Huyu si ndo jana alilalamika kuwa kuna viongozi wanamuangusha kwa kutotoa ushirikiano kwenye MAPAMBANO ikiwemo mikusanyiko isiyo ya lazima. Sasa hapo anawakusanya Raia kwenye mkusanyiko wa Lazima?

Hii ni kick ama ni kitu gani. Namuwaa huyu Mama kichwani na kujiuliza ni wazo lake au kashauriwa vibaya?

Kwa ujumla tangu alipochukua nafasi ya Ummy Mwalimu huyu mama ameprove unworthy kwa vituko Vingi sana. Ni wakati sasa apimwe kwanza ili aendelee na hii kazi au arudishwe Ndugulile maana kule hakuna cha maana anafanya zaidi ya kuzurura na MWIGULU .



E7Dy2OrWYAID1NA.jpg
 
Tatizo kubwa la Ibilisi anakusindikiza kwenda kuzimu kwa nyimbo & pambio tamu tamu, mbwembwe & manjonjo mengi, shangwe, nderemo, vifijo pamoja na shamrashamra nyingi. Akikuingiza katika 18 zake unajikuta upo peke yako, na hapo inageuka kuwa kilio na kusaga meno.

Hapo ndipo lile neno la kiunabii linapotimia; "Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa"
 
Back
Top Bottom