Mapokeo ya wazazi tamko la Rais JPM kwamba hakuna kuchangia chochote kwenye Elimu

Aug 8, 2017
72
84
Kuna wazazi walijiwekea utaratibu wao wa kuchangishana Hela kwa ajili ya CHAKULA kwa watoto wao, Ila baada ya tamko hilo wameacha Kuchangia kwa kusema Raisi amekataza.

Kuna wazazi walijiwekea utaratibu wao wa kuchangishana Hela kwa ajili ya USAFIRI kwa watoto wao, Ila baada ya tamko hilo wameacha Kuchangia kwa kusema Raisi amekataza.

Kuna wazazi walijiwekea utaratibu wao wa kuchangishana Hela kwa ajili ya STUDY TOUR kwa watoto wao, Ila baada ya tamko hilo wameacha Kuchangia kwa kusema Raisi amekataza.

Kuna wazazi walijiwekea utaratibu wao wa kuchangishana Hela kwa ajili ya MOTIVATION (Hamasa kwa wale wanaofaulu Vizuri) kwa watoto wao, Ila baada ya tamko hilo wameacha Kuchangia kwa kusema Raisi amekataza.

Kuna wazazi walijiwekea utaratibu wao wa kuchangishana Hela kwa ajili ya KUSAFIRI KIMICHEZO kwa watoto wao, Ila baada ya tamko hilo wameacha Kuchangia kwa kusema Raisi amekataza.

Nashauri wazazi wenzangu Tuwe tunafafanua Matamshi ya Raisi ili Tuwape amani na furaha watoto wetu...
 
Yaan dah, nawaza tu wale waliokuwa wanachanga hela ya chakula na watoto wanakula shule. Kwa tamko hilo wataacha kuchanga hivyo huduma ya chakula haitakuwepo tena.
Je mahudhurio yatakuwaje?
Usikivu darasani kwa masaa ya mchana utakuwepo?

Ngoja tuendelee kuwa watazamaji tu.
 
Shule nyingi hazina vidurufu hii inasababisha waalimu kushindwa kutoa test au mitihani mara kwa mara kumbuka enzi hizi ni vigumu waalimu kuandika mtihani ubaoni kwa chaki

Wazazi kupitia kamati za shule waliona bora wachange ili watoto wapate mitihani au test ili kujipima na kuboresha taaluma zao

Hatuwazi hayo tunataka tu sifa za majukwaani mkielimika nyie hamtaki wenzenu waelimike ili muwatawale kibabe tu
 
Hawajaelimika hao, wamehitimu tu masomo.
 
Me Nahc Mkuu Mwenyewe Alipaswa Aseme Ni Michango Gan Haitakiwi Maana Ukiweka Katazo Tu Bila Kufafanua Wigo Wa Hilo Katazo Watu Watashindwa Kuelewa May Be Hata Hyo Michango Ya Chakula, Michezo, Tours, Nayo Haitaki Sasa Tupo Dilema,
 
Mh.Rais yuko sawa kabisa na wazazi tupo sawa kabisa,nina imani Ikulu itatoa tamko au itafafanuwa zaidi.Ni mara nyingi tumekuwa na tabia ya kutokumuelewa Mh.Rais anamaanisha nini na Ikulu ikatupa ufafanuzi.Muhimu tufanye subra na tuwe wenye kutii sheria bila shuruti.
 
FB_IMG_15156007436997007.jpg
 
Uendeshaji wa shule hizi umekuwa ni MGUMU kupindukia na sidhani hata kama mawaziri waliokutama naye juzi walemweleza changamoto hiyo (wanamuogopa). Lakini hizi shule na watendaji wake hawapo mbinguni wapo miongoni mwetu ma kwenye jamii zetu na ni shule zetu tunaona hali halisi hata tukibisha.

Bure kabisa ina gharama zake na gharama za hii sera ya huyu bwana italipwa kwa vizazi vingi vijavyo. Yaani chaki zikiisha sometimes isibiriwe wiki 3 hadi fungu lije. Madawati yoote tuliyochangishwa kitemi yamegeuzwa kuni na materials za seremala vijijini maana shule hazina pesa za kulipa walinzi, kinachokuja hakikidhi gharama zote.

Sote tunafahamu ni jinsi gani chakula shuleni kiliongeza mahudhurio na tunakiri serikali HAIWEZI kumudu hili peke yake n.k.

Huyu bwana ni shit hole, maana haiwezekani kwa upande mmoja unakataa kupeleka chakula maeneo yenye majanga kwa sababu eti hakuna chakula cha bure halafu upande mwingine una-discourage juhudi na utamaduni wa wananchi uliokuwa umeanza kujengeka wa kujitegemea na kuchangia maendelelo ya elimu ya watoto wao.
 
Me Nahc Mkuu Mwenyewe Alipaswa Aseme Ni Michango Gan Haitakiwi Maana Ukiweka Katazo Tu Bila Kufafanua Wigo Wa Hilo Katazo Watu Watashindwa Kuelewa May Be Hata Hyo Michango Ya Chakula, Michezo, Tours, Nayo Haitaki Sasa Tupo Dilema,
Mbona aliitaja, alisema iwe chakula hataki kusikia hizo habari.
 
Yaan dah, nawaza tu wale waliokuwa wanachanga hela ya chakula na watoto wanakula shule. Kwa tamko hilo wataacha kuchanga hivyo huduma ya chakula haitakuwepo tena.
Je mahudhurio yatakuwaje?
Usikivu darasani kwa masaa ya mchana utakuwepo?

Ngoja tuendelee kuwa watazamaji tu.

Shida ilikuja pale WAZAZI wengine walipokosa hizo fedha watoto wao walirudishwa nyumbani.
 
Wachangie kwa mkurugenzi mkuu, au ww ni mwalim mkuu nini! Too much michango shule ziligeuzwa fursa ww hujui tu.

Sufuria la kukologea uji limetoboka tunachangia elf 2, shule ina wanafunzi 500.
Kisha linanunukiwa sufuria moja no one ask.
 
Huyu rais ni msomi wa PhD hivi hajui kweli audience itapokeaje ujumbe wake, kila mara lazima kutokewe ufafanuzi wa kauli zake kweli? Hii sio haki kwa mtu mwenye hadhi ya PhD.
 
Me Nahc Mkuu Mwenyewe Alipaswa Aseme Ni Michango Gan Haitakiwi Maana Ukiweka Katazo Tu Bila Kufafanua Wigo Wa Hilo Katazo Watu Watashindwa Kuelewa May Be Hata Hyo Michango Ya Chakula, Michezo, Tours, Nayo Haitaki Sasa Tupo Dilema,
Mimi binafsi nadhani mkuu alikataza michango ya lazima ambayo ilifanya wazazi wengi kushindwa kupeleka watoto wao shule. Michango ya hiyari ni sawa kwa ajili ya maendeleo lakini kumlazimisha mzazi asiekua na uwezo si vizuri.
 
Je, kulikuwa kuna ulazima w kuitamka yeye, kwanini asingemuagiza waziri wa elimu???
 
Habari waungwana ,mm ni mkuu shule ya msingi hapa mkoani Tanga jana baruaimetoka kwa mkurugenzi inayonitaka kuandika jina na kula kiapo na kusaini kama ntatoza mchango yoyote ni fukuzwe kazi.Barua imekataza kutoza mchango yote kama mchango wa mlinzi,mitihani ya majaribio,ujenzi wa miundo mbinh,utengenezaji wa samani,ujenzi wa uzio,mahafali ya wanafunzi,ununuzi wa T shirt,nembo ya uniform, ziara za kitaaluma,uandikishaji,picha za kadi za maendeleo ya wanafunzi.

Ukweli ni mzuri kuliko kitu chochote elim tunaimaliza rasm,kwa kuizika kabisa ,nasikitika wazazi wanashangilia kana kwamba hela tulikuwa tunazila waalim ,wazazi wengne hata jana wamekuja kutupa moyo kuwa tusikate tamaa watajaribu kwenda kwa mkurugenzi kuongea nae,ila mm nimewaambia walim wangu wawe wanakuja na kufundisha tu.

Hata watoto wachekechea walikuwa wanakunywa uji nimesema wasome hivyo hivyo ,kwahiyo kauli ya Raisi ni mbaya katika msitakabali wa elim,naamini muda utaongea
 
Back
Top Bottom