Mapokeo ya Umma kwa Mijadala Bungeni Wiki Hii LIVE on Star TV this Morning | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mapokeo ya Umma kwa Mijadala Bungeni Wiki Hii LIVE on Star TV this Morning

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Yahya Mohamed, Jun 19, 2011.

 1. Yahya Mohamed

  Yahya Mohamed Verified User

  #1
  Jun 19, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 270
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mapokeo ya Umma kwa Mijadala Bungeni Wiki Hii LIVE on Star TV this Morning
  Hatukuweza kuipost mada hii kutokana na kuwepo mijadala kama hiyo ikiendelea katika thread nyingi kama zilivyokuwa zimeanzisha na washiriki akina GHOST RYDER na wengine kwa hiyo tumejielekeza huko na kupata base ya mjadala huu ambao pia unazungumzwa katika maeneo mengi nchini kwa sasa ambapo Umma umekuwa ukipata nafasi ya kujadili masuala ya kisiasa.

  Michango ya mpaka saa 1 na dk 20 nado ina nafasi ya kutupa nyongeza katika mjadala wa leo Tuongee Asubuhi unaoanza saa 1 na dk 30 asubuhi hii.

  Michango mingine kupitia mobile 0717 000 013 itawezesha nyingeza hiyo katika mjadala LIVE

  Nawasilisha ​
   
 2. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #2
  Jun 19, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  We are monitoring...Tatizo huu mgao moto umeshinda kutwa ya jana ila sina shaka njia mbadala ipo kuweza kupata kinachojiri katika Luninga

  Aluta Continua
   
 3. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #3
  Jun 19, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Aaah sasa huyu Baruani vipi kama mnsema mnazungumzia hii mada kwa nini asisome hayo maoni ya Mhariri anayezungumzia kushuka kwa Heshima ya Bunge walau tujue anareflect nini sambamba na Mada yenu muda mfupi kutoka sasa au hajui kinachoendelea??????????????????
   
 4. z

  zebeya Member

  #4
  Jun 19, 2011
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 42
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  startv tunaomba pia mpatikane live online ili hata ambao wako mbali na TV waweze kuchangia mijadala kama hii.
   
 5. segwanga

  segwanga JF-Expert Member

  #5
  Jun 19, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 2,790
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Nionavyo mimi bunge hili linaharibiwa na spika.Ni wazi kabisa kuwa anakandamiza hoja kutoka kambi ya upinzani mfano mzuri alipojichukulia sheria mkononi na kuwa msemaji wa waziri mkuu siku ya alhamis alipoulizwa na mh Lissu na mh Matiko kuhusu suala la polisi kuua raia.Yeye alikurupuka kusema kwamba suala hilo liko mahakani kitu ambacho sio kweli.
  Pili uwezo wake kuridhibiti bunge ni mdogo,wabunge wamekuwa wakionyesha dharau ya wazi hata anaposema order watu bado tu wanaongea tu.
  Pili heshima ya waziri mkuu inashuka kutokana na kukosa umakini katika kujibu maswali mfano haiingii akilini waziri mkuu kusema hajui waziri anayeishi hotelini kwa muda mrefu na pia alipotetea malipo haramu ya posho kwa kusema kwamba wanapotoka mlangoni huwa wanawakuta wapiga kura wao wanasubiri kupewa hizo hela.
   
 6. Mr. Mwalu

  Mr. Mwalu JF-Expert Member

  #6
  Jun 19, 2011
  Joined: Feb 4, 2010
  Messages: 812
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 60
  vp tuunge mkono kauli ya spika mstaafu msekwa kwamba moja ya qualification ya kuwa spika iwe uanasheria? Maana inaonekana mhe anakigugumizi kwenye kutafsiri sheria ama ni mbinu za kuibeba serekali iliyo madarakani!
   
 7. segwanga

  segwanga JF-Expert Member

  #7
  Jun 19, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 2,790
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Tatizo kubwa ni kuwa na mawazo ya kuegemea upande mmoja.Hata kama mtu ni mwanasheria kama akiamua kuwa upande fulani anaweza ndio maana kisheria mtu anaweza akaua kwa makusudi akatetewa na mawakili akashinda kesi.Kwa sababu yeye katika mind set yake ni kuitetea ccm ataendelea kuchukua uamzi ambao unamgharimu baadaye.Najua hata yeye nafsi inamsuta anapochemka lakn kwa sababu anatimiza malengo ya waliomweka pale afanye nini!
   
 8. Mtanzania haswa

  Mtanzania haswa JF-Expert Member

  #8
  Jun 19, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 665
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  YAHYA Mohamed tafadhari usome hizi post zetu wana JF. Namuunga mkono segwanga mia kwa mia. Spika ndio kikwazo kikubwa bungeni na kusababisha haya yote yanayotokea kwa kutoweza kuwa balanced
   
 9. N

  Ngonini JF-Expert Member

  #9
  Jun 19, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 2,024
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Speaker ni kiongozi mkubwa sana kwa mjibu wa katiba yetu lakini yeye halijui hili! Hajui kuwa anaweza kuwa Rais kwa muda kisheria! Hajui kuwa yeye na Rais wanaongoza mihimili tofauti na mhimili wa speaker ndiyo wananchi ambao ndo wa ajri wa Raisi. Kimsingi speaker anapashwa kuwa mtu anayekubalika sana maana ndiye mwakilishi wa wananchi katika kuhakikisha mtu waliye mchagua(Raisi) anasimamamia rasilimali zao kama wananvyotaka wao.

  Haingii akilini speaker anakuwa kama ndo ameteuliwa na Raisi anafanya yale ambayo serikali inataka. Tatizo hapa pengine ni Rais kuwa pia mkiti wa chama chake. Huyu mama anafuata maelekezo ya mkiti wa chama chake kuendesha bunge.

  Mimi naona katiba ibadiliki ili viongozi wa mihili hii miatu(serikali,bunge,mahakama) ikiwezekana wachaguliwe kwa kupigiwa kura na wananchi wote kama ilivyo kwa Raisi ili serikali isiwe na influence kwenye mihimili mingine. Mgawanyo wa budget za kuendesha(kwa maana ya expenses) mihimili hii mitatu iainishwe kwenye katiba ili kila mhimili ujitegemee.
  Hapa kutakuwa na uwajibikaji kwa wananchi kwa mihimili yote mitatu.

  Nawasilisha.
   
 10. fige

  fige JF-Expert Member

  #10
  Jun 19, 2011
  Joined: Jul 4, 2010
  Messages: 376
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tatizo kubwa la Bunge letu kwa sasa ni kulinda masilahi ya vyama kuliko masilahi ya Nchi na wananchi.

  Mfano ,mbunge anasimama anakosoa bajeti kwa sentensi kumi na anaunga mkono kwa pointi moja ,na kusema anaunga mkono asilimia mia
   
 11. Japhari Shabani (RIP)

  Japhari Shabani (RIP) R I P

  #11
  Jun 19, 2011
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 721
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Nakubaliana nawe mkuu.Bunge la sasa tatizo kubwa ni Speaker hana uwezo wa kuliongoza bunge hili kwau ukosefu wa uzoefu,upeo wa upembuzi wa mambo au kwa makusudi hii inalipelekea bunge kukosa mwelekeo ingawa lina wabunge makini hasa wa CHADEMA ambao wanajiaandaa kwa hoja zao na kuzifanyia utafiti wa kina tofauti na wabunge wa CCM ambao wananyimwa uwezo na chama chao kutoa mawazo yao au kukosoa kwa maana hiyo kunawanyima morali wa kuzifanyia uchunguzi hoja zao ingawa kuna wabunge makini pia.

  Kazi ya wabunge wa CCM inabaki kupiga kura kuidhinisha miswada iliyoandaliwa na serikali bila kujali inatija au la kwa taifa na kwa vile ni wengi inapita.Na kwa Mawaziri akiwemo Waziri mkuu hawajisumbui kutafakari maswali na majibu wanayoyatoa bungeni kwani jibu lolote kwani wana ulinzi wa Speaker na wabunge wengi wa CCM.Matokeo yake tunapata majibu mepesi kwa maswali mazito na majibu mazito kwa maswali mepesi.Bunge lisilo na mijadala ya kidemokrasia linazaa miswada mibovu
   
 12. L

  LAT JF-Expert Member

  #12
  Jun 19, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  i wish speaker wa bunge letu angekuwa Rev Christopher Mtikila
   
 13. m

  mwamagunda Member

  #13
  Jun 19, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tatizo kubwa hapa ni ukale wa mawazo ya viongozi wetu. Bado wanaamini kuwa mtu kuwa kiongozi maana yake ana akili kuwazidi wote anaowaongoza, hali ambayo si sahihi hata kidogo (na ndiyo iliyotufikisha hapa tulipo kama taifa).

  Kazi ya kiongozi wa leo ni kukusanya mawazo ya wale anowaongoza, na yeye kuwa dira katika kuyatekeleza kwa manufaa ya wote. Kinyume cha hapo ni fujo. Hiki kinachotokea leo ni ishara kuwa watu (wanaoelewa na ambao siyo wanafiki) wamechoka. Hali hii ikizidi kupuuzwa, kama wafanyavyo viongozi wetu, wakisaidiwa na wabunge wanaokitetea chama badala ya wananchi, TAIFA HILI LITAVUNJIKA!
  Mtu mwenye njaa hamazishwi kwa kejeli na vijembe, hasa kama anajua kuwa sababu ya njaa yake ni mtu mwingine!
  MUNGU IBARIKI TANZANIA
   
 14. Mkiliman

  Mkiliman JF-Expert Member

  #14
  Jun 19, 2011
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 957
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  Kweli Madam Speaker anaharibu bunge kwa kuzuia wenye hoja nzito na zenye maslahi kwa taifa kutoongea kwa kina. Utaona anasema: Waziri unaweza kujibu au usijibu,au jibu kwa ufupi, vinginevyo speaker anajibu mwenyewe...! huyu bibi anashusha hadhi ya bunge!

  pia wabunge wa CCM ndio vimeo kabisaaa utaona anasema: mh. spika nakushukuru wewe,Rais, ccm, n.k,pia nampongeza Rais kwa kushinda...porojo kibao, naunga mkono hoja ya bajeti 100%, anakosoa mara kumi! je kweli wanajua wanalofanya hawa?
   
 15. t

  tumpale JF-Expert Member

  #15
  Jun 19, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 201
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  tambueni tabia za mtu anayewekwa mahali kwa upendeleo, mwenye uwezo dhaifu. kimsingi maadam spika ni dhaifu dhahiri.
   
 16. K

  Kiluvya2011 JF-Expert Member

  #16
  Jun 19, 2011
  Joined: Feb 18, 2011
  Messages: 215
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Bibi kiroboto kazi imemshinda,...uwezo wake unanitatiza maana sijui kama anatumia oblongata yake au ni remote ya ****** ndoo inamuongoza.
   
Loading...