Mapochopocho yamuokoa aliyefukiwa na kifusi siku 11 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mapochopocho yamuokoa aliyefukiwa na kifusi siku 11

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Bujibuji, Jan 26, 2010.

 1. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #1
  Jan 26, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,263
  Likes Received: 21,991
  Trophy Points: 280
  PORT-AU-PRINCE,Haiti

  WAOKOAJI nchini hapa wamemuokoa mwanamume mmoja kutoka chini ya kifusi ikiwa ni siku 11 tangu tetemeko la ardhi liukumbe mji huu na kusababisha maafa makubwa.

  Habari kutoka mjini hapa zimeeleza kuwa watu wengi walipigwa na butwaa baada ya mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 24 kuokolewa kwenye kifusi cha hoteli moja iliyopo mjini hapa.

  Tayari Serikali ya nchi hii imekwishakata tamaa baada ya kusimamisha rasmi juhudi zozote za kuwatafuta manusura.

  Imeelezwa kuwa,walioshuhudia walijawa na furaha na kupiga makofi wakati Wismond Exantus aliponyanyuliwa kutoka ndani ya vifusi vya hoteli iliyokuwa ikifahamika kwa jina la Napoli.

  Baada ya kuokolewa Exantus aliwaambia waandishi wa habari kwamba kwa siku hizo zote alikuwa akitegemea soda na vitafunio vidogo vidogo.

  “Nilikuwa nikitumia Coca-Cola na vitu vingine vidogo vidogo,” amesema Exantus na kuongeza kuwa kila siku alikuwa na matumaini ya kwamba atanusurika.

  Imeelezwa kuwa waokoaji kutoka Ugiriki, Ufaransa na Marekani walitumia zaidi ya saa mbili na nusu wakijaribu kumwokoa.

  Mmoja wao kutoka Ufaransa, Luteni Kanali Christophe Renou amelifananisha tukio hilo kama muujiza.
   
 2. Sumbalawinyo

  Sumbalawinyo JF-Expert Member

  #2
  Jan 26, 2010
  Joined: Sep 22, 2009
  Messages: 1,286
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  ana bahati alikuwa alipatwa na maafa alipokuwa kwenye mgahawa.
  pole zangu za dhati ziwafikie wale waliokuwa wakijihelp kwenye vyoo vya shimo, maana hakika walidumbukia kwenye shimo la choo.
   
Loading...