Mapishi

Kimbweka

JF-Expert Member
Jul 16, 2009
8,597
1,683
Wajuao jinsi ya kuuandaa muhogo kwa ajili ya mapishi naomba mjitokeze kuwafundisha na wengine.
Leo niliuandaa muhogo wangu lakini aliyeula alisema umekuwa mchungu sikuuandaa vizuri
 
Labda umeupika na maganda yake nae kaula na maganda, cku nyingine umenye shehe
 
Wajuao jinsi ya kuuandaa muhogo kwa ajili ya mapishi naomba mjitokeze kuwafundisha na wengine.
Leo niliuandaa muhogo wangu lakini aliyeula alisema umekuwa mchungu sikuuandaa vizuri

Dahh nilikumis kweli leo maana jana ulinifanya niwe active sana usipotee hivyo na wewe bwana. aaaa Huo muhogo hukuuosha viruzi halafu uliweka chumvi kabla unatakiwa unaweka chumvi ukishaanza kuiva hautakuwa mchungu
 
Wajuao jinsi ya kuuandaa muhogo kwa ajili ya mapishi naomba mjitokeze kuwafundisha na wengine.
Leo niliuandaa muhogo wangu lakini aliyeula alisema umekuwa mchungu sikuuandaa vizuri

Wakati mwingine inategemea na aina ya muhogo ulio tumia, baadhi ya mihogo ni michungu kiasi, hiyo si mizuri kwani kwenye mihogo ambayo ina uchungu kuna sumu ambao si nzuri kiafya. Mihogo michungu husababisha matatizo mengi ikiwemo kupata goiter, nerve-damaging disorder au ugonjwa unao itwa Konzo.

Jinsi ya kupika Muhogo:

Vipimo.

Muhogo................................. Nusu kilo

Tui La Nazi............................2 vikombe

Chumvi.....................................kiasi

Pilipili mbichi...............................2

Mafuta........................................1 kijiko moja

Kitunguu maji..............................1 kidogo

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

1. Chambua muhogo ukatekate au tumia iliyo tayari.

2. Chemsha muhogo katika sufuria kwa maji kidogo na chumvi, funika uive muhogo.

3. Karibu na kukauka maji tia tui, kitunguu maji ulichokatakata na pilipili mbichi.

4. Unaupika moto mdogo mdogo hadi ukauke tayari kuliwa na samaki au kitoweo chochote kingine.
 
Kama hajaelewa chukua fimbo chapa kisha rudia tena
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom