Jinsi ya kupika chapati laini na zenye ladha nzuri

X-PASTER

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
11,610
1,809
Vipimo

Unga wa ngano mweupe ................... 1 Kilo
Samli .............................................. 150gm
Chumvi ............................................3 vya chai
Maji ya moto yasichemke lakini ........... Kiasi
Mafuta Ya Zaituni (olive oil) ................ 4 vijiko vya supu
Samli tena ....................................... 200 gms
Iliki iliyosagwa ...................................1 kijiko cha chai

Namna ya Kutayarisha na kupika

1.Tia unga kwenye sinia au bakuli kubwa lililo na nafasi, changanya na chumvi, mafuta ya zaituni, samli 150g, iliki, mimina maji ya moto kwa kipimo cha kikombe kila unapovuruga unga.

2.Unga uwe mwepesi unapoganda kuwa donge moja kubwa. Uwache kwa muda wa dakika 20 30 ukiwa umeufinika ili unga ulainike.

3.Katakata madonge makubwa yenye ukubwa wa chungwa ili uweze kutoa kila donge chapati mbili. Ukimaliza hapa weka madonge kwa muda wa dakika 15 ukiwa umefunika bila ya kuingia upepo ndani.

4.Sukuma donge ukiwa umelimwagia unga mkavu juu, liwe mviringo. Unaweza kutumia kifimbo hata chupa kusukumia madonge ikiwa huna kifimbo juu ya meza au kwenye kibao maalumu cha chapati.

5. Sukuma donge moja mpaka liwe duwara jembamba.

6. Paka samli kama kijiko kimoja cha kulia, ukihakikisha umepaka duwara lote.

7. Kunja lile duwara kama mfano wa kamba, huku unazungusha kama kamba ili iwe ndefu kidogo.

8. Zungusha ile kamba iwe mviringo. Funika na kitambaa kisafi cha jikoni ambacho kinamajimaji kidogo.

9. Endelea namna hii mpaka umalize madonge yote

10. Sukuma chapati iwe mviringo kama nchi 7 hivi.

11. Weka chuma cha kuchomea chapati jikoni moto mdogomdogo.

Pika chapati kwenye frying pan, moto uwe wa kiasi. Ikiiva upande mmoja na kuanza kufura, geuza upande wa pili. Tumia kitambaa kisafi cha jikoni kupress na kuzungusha zungusha ile chapati.

Ikiiva upande wa pili, mimina kijiko kimoja cha chakula cha samli na ugeuze chapati tena, zungusha zungusha kisha mimina nusu kijiko cha kulia cha samli na ugeuze upande wa pili kidogo.

Toa chapati uweke kwenye sahani. Ikunje kunje kidogo kisha uifungue vizuri.

Zipange kwenye sahani huku unazifunika, hapa tayari kuliwa kwa mchuzi au mboga yoyote.

========
1590140631714.png


Mahitaji:
  • Unga wa ngano nusu kilo.
  • Siagi vijiko 2.
  • Yai moja.
  • Chumvi kiasi.
  • Hiliki kama unapenda maana wapo ambao hawapendi.
  • Maji ya uvuguvugu kwa ajili ya kukandia.
  • Mafuta ya kupikia.
Jinsi ya kuandaa

Weka unga wa ngano katika bakuli la kukandia, kisha tia chumvi na hiliki na uchanganye kwanza, baada ya hapo tia siagi na uichanganye vizuri na unga mpaka ipotee. Baada ya hapo tia tena yai na uchanganye vizuri.

Mchanganyiko ukishachanganyika vizuri weka yale maji ya uvuguvugu kidogo kidogo huku ukikanda, ukande mpaka uhakikishe haunati ila umekuwa laini.

Kukanda huko kutumie kama dakika 15 hivi ndiyo utalainika vizuri, ukimaliza katakata madonge kulingana na chapati unazotaka, hakikisha saizi inakuwa sawa kwa yote.

Ukimaliza, sukuma donge moja baada ya jingine. Ukishasukuma paka mafuta kisha weka donge pembeni mafuta yale yape nafasi ya kuingia ili kuifanya chapati iwe laini zaidi.

Ukishamaliza madonge yote chukua la kwanza sukuma anza kupika, pika chapati zako kulingana na jinsi ulivyokuwa ukizipaka mafuta moja baada ya nyingine.

Michango ya wadau
Chef mkuu, mimi huweka mafuta ya moto sana kwenye unga wenye chumvi. Lakini nahakikisha nimechekecha unga (to add in air) kabla ya kuutumia. Then nachanganya unga na mafuta kwa kutumia vidole tu (inaitwa rub in, to add more air). Nakanda na maji ya uvuguvugu kiasi.

Nikishasukuma mara ya kwanza na kupaka mafuta kidogo, navuta kwa vidole gently kila upande napata mdabwada wenye unene mdogo sana, kisha nakamata kona moja na kukunja kamba (hapa napata layers nyiingi nyembamba kwenye chapati zangu).

Naziacha kama muda wa nusu saa hivi, kisha nasukuma miduara.
ili zisinyonye mafuta mengi, nakausha pande zote kikaangioni, then naweka mafuta kidogo ( nusu ya tea spoon) juu then naipindua. Inakuwa na rangi nzuri sana, laini na inasasambuka haswaa!
----
Kuna njia tofauti za kukanda chapati zako zikawa laini, lakini siri kubwa ya kupata chapati nzuri ni kuukanda huo unga vizuri na ulainike.

Mahitaji basic:

1. Unga wa ngano
2. Chumvi
3. Sukari kidogo sana kwa ajili ya seasoning
4. Mafuta kidogo ya kukandia kulingana na unga wako, usijaze mafuta kibao
5. Maji - hapa inategemea na ukandanji wako mimi natumia maji ya baridi sana ikiwezekana nayaweka kwenye freeza kidogo yazidi kuwa baridii.

Mhitaji extraa:

Hapa ni kulingana na ufundi na uzoefu wako unaweza kuweka vitu vifuatavyo ukipenda lakini sio vyote waweza chagua kimoja

1. Tui la nazi (waweza kutumia kukandia unga badala ya maji
2. Maziwa - ukitaka kuongeza virutubisho kwenye mlo wako
3. Mayai - Na chapati inakuwa laini kama sufi, kwa sababu mayai hayafanyi chapati iwe ngumu kama ni hivyo basi hata keki zingekuwa ngumu kama jiwe.
4. Vitunguu maji - kwa ajili ya kuongeza ladha
5. Nyama ya kusaga au mboga mboga yoyote ile -kwa ajili ya kubadilisha aina za chapati sio kila siku ni chapati design ile ile tu.

Kwa basic Chapati -Stage 1:

1. Tia unga wako kwenye chombo au mashine yako ya kukandia.
2. Weka chumvi, na sukari kidogo kwa ajili ya seasoning
3. Tia mafuta kwenye unga (kwa mfano kwa unga kilo moja weka mafuta 1/4 kikombe)

4. Changanya vizuri mchanganyiko wako
5. Weka maji yako kwenye unga kidogo kidogo mpaka unga uchanganyike.
6. Unga ukishanyanganyika ukande mpaka ulainike.
7. Ukisha lainika weka kwenye friji kama nusu saa hivi, kama huna friji ufunike mahali pasipo na joto.

Stage 2:

1. Changanya unga wako vizuri kisha ukate madonge madogo madogo kiasi.
2. Chukua donge moja usukume kwenye kibao au juu ya meza iliyo safi.
3. Paka mafuta kidogo juu ya chapati yako uliyoisukuma, waweza kutumia samli au mafuta mazito kama samli.
4 Kunja chapati yako irudi katika umbo la donge tena. Hapa ndio key unaweza kufanya chapati yako ikawa ngumu au ikawa laini yenye layers.
5. Sukama tena donge lako ulilolikunja, anza na lile la kwanza.
6. Weka chapati yako kwenye chuma kikavu (frying pan) kilichopata moto, kisiwe cha baridi wala cha moto sana.
7. Ikiiva upande mmoja igeuze upande wa pili.
8. Ikishaiva pande zote weka mafuta kijiko kimoja tu kikubwa cha chakula kwenye chapati yako upande wa chini.
9. Ikunje hiyo chapati na uigeuze pande zote ipate mafuta, au waweza kuisuguasugua na kijiko chako kukahikisha upande zote zinapata mafuta na kuiva vizuri (inakuwa na rangi ya brownish)

10. Ondoa chapati yako kwenye chuma iko tayari kwa kuliwa.

Waweza kula peke yake, na chai, mchuzi wa aina yoyote ile au hata na maharagwe.

NB:
Waweza kukanda unga kwa kutumia mashine kama bread maker unachagua dough, kisha unaumonitor unga ukishakandika tu ndani ya 30 minutes unautoa ndani ya mashine na kuuweka kwenye friji kwa nusu saa. Au unaweza kukanda unga kwa kutumia mixer zile kubwa na unatoa dough maker.
Hii ni kwa wale wenye hizo mashine kama mimi. Kama huna mashine basi utaukanda unga wako kwa mikono hadi ulainike vizuri. Kulainika hapa sio kujaza maji, bali kutumia viganja vyako kuulainisha mpaka unga ukiupiga unavutika. Kisha unauacha uendelee kulainika kwa kuuweka kwenye friji.

ILANI: Mkishajaribu msinisifie mie maana hata mi nimeipata kwa KIJARUBA!
----
Yaani mimi hakuna mlo naupika fasta na fresh kama chapati!
just maji ya baridi,mafuta ya baridi,chumvi kiasi,pilipili manga ukipenda,kijiko kimoja cha blue band,unga kg 1

mix vyote,weka maji nusu kikombe(unaweza kukandia tui la nazi kwa ladha ya ukweeen!)kanda kwa dk kadhaa!

ukishalainika uache kidogo kama dak 10 hv!
gawa madonge(kg ya unga inatoa chapati 9 kubwa)
kisha sukuma huku thn weka mafuta yasambaze kwa kijiko kisha kunja kama tairi hvi!

maliza madonge yote thn anda chuma chako(kwa uzoefu wangu kile chuma cheusi kile ndo hatareee kwa chapati nzuri sio fyrn pan zenu zile za supermarket)
weka chapati yako kavu bila mafuta,ikishageuka rangi pande zote mbili weka mafuta,mafuta kidogo wakati wa kupika ndo ulaini wa chapati utakavokuwa long last!)

NB
unga unavokuwa mlaini ndo chapati zinakuwa ngumu!
ukiwa mgumu ndo chapati zinakuwa laini!

maji ya moto yaivisha unga unakuwa kama umechemshwa!(nionavyo mimi)
unga ukiwa wa kuvutika unatengeneza chapati zinakuwa kama unakula bg gee!kwa mpishi unajua tu nimechemsha!
wasalaam!
-----
Yaani mimi hakuna mlo naupika fasta na fresh kama chapati!
just maji ya baridi,mafuta ya baridi,chumvi kiasi,pilipili manga ukipenda,kijiko kimoja cha blue band,unga kg 1

mix vyote,weka maji nusu kikombe(unaweza kukandia tui la nazi kwa ladha ya ukweeen!)kanda kwa dk kadhaa!

ukishalainika uache kidogo kama dak 10 hv!
gawa madonge(kg ya unga inatoa chapati 9 kubwa)
kisha sukuma huku thn weka mafuta yasambaze kwa kijiko kisha kunja kama tairi hvi!

maliza madonge yote thn anda chuma chako(kwa uzoefu wangu kile chuma cheusi kile ndo hatareee kwa chapati nzuri sio fyrn pan zenu zile za supermarket)
weka chapati yako kavu bila mafuta,ikishageuka rangi pande zote mbili weka mafuta,mafuta kidogo wakati wa kupika ndo ulaini wa chapati utakavokuwa long last!)

NB
unga unavokuwa mlaini ndo chapati zinakuwa ngumu!
ukiwa mgumu ndo chapati zinakuwa laini!

maji ya moto yaivisha unga unakuwa kama umechemshwa!(nionavyo mimi)
unga ukiwa wa kuvutika unatengeneza chapati zinakuwa kama unakula bg gee!kwa mpishi unajua tu nimechemsha!
wasalaam!
 
jamaniii napenda chapatiiiii ziwe za kusukumaa.....au kumimina......wallah zinashuka vizuri mauongoni....ladha yake murua mdomoni....cant wait chai time! Thanks to mpishi kwa kunitengenezea appetite:A S 465:
 
Chapati


Vipimo


• Unga wa ngano mweupe ................... 1 Kilo
• Samli .............................................. 150gm
• Chumvi ............................................3 vya chai
• Maji ya moto yasichemke lakini ........... Kiasi
• Mafuta Ya Zaituni (olive oil) ................ 4 vijiko vya supu
• Samli tena ....................................... 200 gms
• Iliki iliyosagwa ...................................1 kijiko cha chai


Zipange kwenye sahani huku unazifinika, hapa tayari kuliwa kwa mchuzi au mboga yoyote.
Tatizo la chapati zinakula mafuta mengi sana....
 

Similar Discussions

14 Reactions
Reply
Back
Top Bottom