Mapishi ya chapati za kumimina

Napenda kupika mno kuosha vyombo sasa hiiiiiiiiiiii (on saint magu voice) ingekuwaga unasema vyombo kuwa visafi na vikawa napenda kupika kitu kipya natamani hata nimvute yule dada wa mapishi wa azam nimweke ndani
 
Ukipata muda uweke namna ya kuchoma chapati za kusukuma.

Kuna siku nimechoma zikawa ngumu kama nimechanganya saruji na unga wa ngano.
Chapati za kusukuma rahisi sana, shida yangu ipo kwenye za kumiminia zinatoka zimekatikakatika
 
Ukipata muda uweke namna ya kuchoma chapati za kusukuma.

Kuna siku nimechoma zikawa ngumu kama nimechanganya saruji na unga wa ngano.

Ulikanda mwenyewe?

Kuna mbinu mbili tatu

Moja kukandia mafuta
Mbili kukandia maji ya baridii

Kukanda muda mrefu

Kuacha unga uumuke

Kupakaza kando mafuta kabla haujalifanya chapat
 
Kwa wale vijana wa kiume na wakike ambao huwa mnapika chapati za kumimina simple simple yaani chapati unakula lakini hata ladha huifurahii.

Hebu pitia hizi njia hapa then utakuja kunishukuru baadaye...

Maandalizi ya awali...

Unga wa ngano nusu kilo
Mafuta ya kupikia
Maji masafi
Fraying pan moja
Iriki pakiti 6 zile za sh. 50
Mayai ya kienyeji/kisasa matatu
Sukari vijiko viwili vya chakula
Chumvi kijiko kimoja na nusu cha chakula
Pilipili hoho/ kama hutumii haina haja
Vitunguu maji viwili vikubwa vya wastani
Karoti moja ya size ya kawaida
Sufuria ya size ya kati kwa ajili ya kuchanganya mchanganyiko

Mapishi sasa yenyewe!!
1) Chukua unga wako weka kwenye sufuria, weka chumvi na sukari koroga huo mchanganyiko.

2)Kata vitungu maji, hoho, na karoti katika size ndogo ndogo kisha changanya kwenye huo mchanganyiko hapo juu!

3) Chukua iriki zile zitwange kwenye kinu ziwe kama unga unga kisha weka kwenye huo mchanganyiko hapo juu

4) pasua mayai yako kisha koroga kwenye chombo pembeni halafu changanya kwenye huo mchanganyiko hapo juu.

5) chukua maji anza kumimina kwenye huo mchanganyiko mpaka uone unga umechanganyika vizuri na angalia usizidishe maji unga ukaleta uji uji mwepesi sana unatakiwa uwe mzito kiasi na usiwe mzito saaana.

6) Baada ya kukoroga na kupata mchanganyiko mzuri acha kwa dakika 5 kisha anza kuwasha jiko na weka fraying pan yako jikoni ianze kupata moto na mafuta kiasi weka.

7) baada ya fraying pan kuwa tayari anza kumimina mchanganyiko wako kwa kiasi. Angalizo Moto usiewe mkali sana....

Ahsante na mapishi njema
kwa style hii hatuoi ng'oooo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom