Mapishi ya chapati za kumimina

thomas_360

JF-Expert Member
Oct 11, 2015
1,459
1,428
Kwa wale vijana wa kiume na wakike ambao huwa mnapika chapati za kumimina simple simple yaani chapati unakula lakini hata ladha huifurahii.

Hebu pitia hizi njia hapa then utakuja kunishukuru baadaye...

Maandalizi ya awali...

Unga wa ngano nusu kilo
Mafuta ya kupikia
Maji masafi
Fraying pan moja
Iriki pakiti 6 zile za sh. 50
Mayai ya kienyeji/kisasa matatu
Sukari vijiko viwili vya chakula
Chumvi kijiko kimoja na nusu cha chakula
Pilipili hoho/ kama hutumii haina haja
Vitunguu maji viwili vikubwa vya wastani
Karoti moja ya size ya kawaida
Sufuria ya size ya kati kwa ajili ya kuchanganya mchanganyiko

Mapishi sasa yenyewe!!
1) Chukua unga wako weka kwenye sufuria, weka chumvi na sukari koroga huo mchanganyiko.

2)Kata vitungu maji, hoho, na karoti katika size ndogo ndogo kisha changanya kwenye huo mchanganyiko hapo juu!

3) Chukua iriki zile zitwange kwenye kinu ziwe kama unga unga kisha weka kwenye huo mchanganyiko hapo juu

4) pasua mayai yako kisha koroga kwenye chombo pembeni halafu changanya kwenye huo mchanganyiko hapo juu.

5) chukua maji anza kumimina kwenye huo mchanganyiko mpaka uone unga umechanganyika vizuri na angalia usizidishe maji unga ukaleta uji uji mwepesi sana unatakiwa uwe mzito kiasi na usiwe mzito saaana.

6) Baada ya kukoroga na kupata mchanganyiko mzuri acha kwa dakika 5 kisha anza kuwasha jiko na weka fraying pan yako jikoni ianze kupata moto na mafuta kiasi weka.

7) baada ya fraying pan kuwa tayari anza kumimina mchanganyiko wako kwa kiasi. Angalizo Moto usiewe mkali sana....

Ahsante na mapishi njema
 
Ukipata muda uweke namna ya kuchoma chapati za kusukuma.

Kuna siku nimechoma zikawa ngumu kama nimechanganya saruji na unga wa ngano.
Daaah!! Katika vitu ambavyo sijajifunza mpaka Leo ni hizo chapati za kusukuma isee mpaka kesho sidhani kama nitaweza kuja kujua labda mke wangu atakuja kunifundisha....
 
IMG_20190812_173521.jpg
 
Dada zetu kazi wanayo siku hizi maana tumeanza kubobea sekta nyeti ya mambo ya jikoni. wao tutakuwa tunawaita kwa shughuli moja tu. vingine tunafanya wenyewe siku hizi.
Yaani mm mke wangu atapata tabu sana akipika chakula kibichi nitakijua, Akizidisha viungo nitajua. Akitoa wali bokoboko nitajua yaani kila chocho ya upishi hanidanganyi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom