Mapishi ya Chakula Dawa kwa ajili ya Afya Bora na Utimamu kimwili

GuDume

JF-Expert Member
Jan 18, 2015
6,652
14,247
Leo nahitaji kushiriki nanyi chakula ambacho mara nyingi mama yangu amekuwa akipenda kutupikia kimekuwa kama ni chakula cha kifamilia na akiweka secret ingredients ambayo hiyo sitoitaja maana inabaki kuwa ni siri ya familia.

Hii ni uji mzito wa vegetables tu ambazo zina nutritions mbali mbali na minerals.

Andaa.
1. Njegere robo kilo
2. Karoti kubwa tatu
3. Hoho mbili
4. Nyanya mbili saga
5. Unga wa mbegu za maboga vijiko vinne vikubwa
6. Vitunguu maji viwili vya wastan
7. Pilipili manga kijiko kimoja kikubwa
8. Unga wa soya kijiko kimoja
9.chumvi kias
10.viazi mviringo vinne vilovyomenywa na kukatwa vidogo
11. Spinach
12. Xxxxxxx
Chemsha njegere zikiiva weka pembeni na maji yake

Chukua sufuria weka maji kiasi tu yakichemka weka vitunguu kaanga kidogo halafu weka nyanya iliyosagwa humo kaanga kidogo then weka viazi...

Vikianza kuiva weka karoti na njegere pamoja..mimina ile supi nya njegere. Weka hoho na unga wa mbegu za maboga,weka soya.. Weka na pilipili manga.

Acha vichemke kiasi.weka hoho na piga kidogo isiiive sana na karoti pia isiive sana. Weka spinach ambayo umekatakata vipande vidogo vidogo. Isiive. Karot,spinach,hoho havitakiw kuiva sana. Weka chumv kiasi.

Ipua subiri ipoe kiasi....unaweza weka kwenye blender ukasaga... Utapata ladha tamu na harufu ya kuvutia.ikishalainika weka kwenye moto iwe ya moto kiasi utakacho au moja kwa moja weka kwenye thermos au hotpot.

Tayari kwa kuliwa na chapati, yenyewe peke yake au na spaghetti.

Ni mlo mzuri kiafya usio na madhara.unafaa wamama wajawazito,waliojifungua soon, wababa kuongeza nguvu,kurudisha nguvu kwa wagonjwa,watoto ,watu wazima. Kabla na baada ya tendo la ndoa.

Karibuni sana. Kama kuna maswali niulizeni.
 
Mkuu GUDume tunashukuru kwa kutojali wanajamii wenzio.Lakini pia tungefurahi kama ukituambia hizo''secret ingredients ambayo hiyo sitoitaja''' na pia no12xxxx
 
Mkuu GuDume nina wasi wasi bila hiyo dawa ya kuzuia kuharisha hapo #12 watu wataharisha kunakotukuka. Hivyo basi ni vyema kwa moyo wa upendo tuu ututajie hiyo ingredient 12 ili tusiharishe mara baada ya kunywa hiyo safisha tumbo ya mama yako.
 
Mlo huu wamekula watu tofaut tofaut kma mlo maalum pasipo kuharisha. Ni mapishi tu...mwingine hta akila mayonnaise anaharisha. Au akila mhogo ... Ni chakula salama na nimewapikia sana wanawake walezi... Nami ninapokuwa na mech nying kwa wakati mmoja hutumia hii kitu
 
Sasa Mkuu huoni bila hiyo namba 12 hutamudu hizo mechi nyingi? Tuwekee basi na sisi wenye jukumu la kucheza mechi tatu kwa siku mara moja kwa mwezi tuweze kumudu.
 
hata bila hata hiyo namba 12 mambo yanaenda vizuri tu maana sawa sawa tu. hii ni kwa ajili ya flavor zaidi ila pata huo mlo then pumzika kama nusu saa.. nenda kapige game na mtu yeyote ambaye unadhani kiwango chake ni cha kimataifa... halafu utakuja kunambia mwitikio wake.

Sasa Mkuu huoni bila hiyo namba 12 hutamudu hizo mechi nyingi? Tuwekee basi na sisi wenye jukumu la kucheza mechi tatu kwa siku mara moja kwa mwezi tuweze kumudu.
 
mkuu nawajali sana ila kukoseana hii hakubadilishi chochote maana ni kwa ajili tu ya flavor.... i wish siku ukija kunitembelea nikutengenezee kitu kama hiki. nawajali sana ndo maana nawapa siri ya ushindi.... hii kitu ni balaa ndugu yangu asikwambie mtu....
Mkuu GUDume tunashukuru kwa kutojali wanajamii wenzio.Lakini pia tungefurahi kama ukituambia hizo''secret ingredients ambayo hiyo sitoitaja''' na pia no12xxxx
 
Back
Top Bottom